Kutoswa kwa Bashe na Kingwangala NEC ni dalili za kurudi kwa Lucas Selelii?

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
603
340
Wa JF Kumekuwa na mnyukano mkali sana katika ulingo wa siasa za CCM Wilaya Nzega,kati ya Hussein Bashe na mbuge wa sasa Hamisi Kigwangala.Wamekuwa wakishutumiana kwa wazi mpaka kutishiana maisha kwa bastora.Kitendo hiki kimewafanya wote kwa pamoja kutoswa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ujumbe wa Nec kupitia wilaya ya Nzega. Aliyekuwa mbunge wa zamani Lucas Selelii hasikiki ktk duru hizi za siasa za CCM Nzega.Ikizingatiwa kwenye kura za maoni alishika nafasi ya pili nyuma ya Bashe aliyekuwa wa kwanza na juu ya Kigwangala aliyeshika nafasi ya tatu. Je ugomvi wa Bashe na Kigwangala utamrudisha Selelii kwenye siasa za nzega tena? Maoni kwenu wadau.
 
Hawezi! Huu mnyukano ni kati ya Lowassa na Sitta. Vivuli vyao ndoo vinavoitikisa Nzega. Selelii baada ya kuwa nje ya ulingo wa Bunge kabaki Simba wa Karatasi!
 
Back
Top Bottom