armanisankara
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 283
- 49
Kuna pesa zimetolewa na United Nations kuhusu program ya mabadiliko ya Climate Change (siku hizi wanaita mabadiliko ya tabia nchi climate change).
Pesa hizi zinafika mabilioni ya shillings za TZ na madhumuni yake makubwa ni kutoa kwa nchi kama Zanzibar nchi za visiwa (Island states) ambazo kimaumbile ndio zinazoathirika zaidi. Naam Zanzibar kweli imeathirika sana katika suala hili la climate change.
Pesa hizi zinatakiwa wapewa SMZ na zifanyiwe program katika idara kama Mazingira, kilimo, Idara ya hali ya hewa, taasisi kama za viwanda n.k ni pesa nyingi na zinafika billions.
Hizi wamzikalia akina Membe, hazina na taasisi za Fedha za Tanganyika.
Kadhalika, kuna component ya pesa kama hizi kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ziliidhinishwa katika mkutano wa climate change adaptation uliofanyika, Kampala Uganda, March-April 2012.
Katika Mkutano huo, wajumbe kutoka Tanganyika walisema wazi wazi kuwa Zanzibar haina foreign accounts/ na haiwezi kuwa signatory katika suala hili so pesa hizi ziingiawe katika account ya Tanganyika hazina au popote pale. Hizi pia ni bilions.
Wapo wajumbe kutoka zanzibar waliohudhuria vikao kama hivyo kutoka mazingira, kilimo na hata idara ya maafa Zanzibar.
Ukiachilia zile alizozikalia Membe, hizi walizikalia akina Jumanne Maghembe, au nani na nani sijui, wote mafirauna kwa Zanzibar. Hili suala la mambo ya pesa cabinet ya Zanzibar, SMZ wanalizungumza kila wanapokutana, but no solution na haipatikani aslan abadan.
source: mtandao wa kizenji Mzalendo.net .