Kutamani vyakula vya aina fulani baada ya ugonjwa.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,598
215,331
Mara nyingi inakutokea baada ya kuugua homa mfano malaria kali, umelala kitandani siku mbili, siku ya kwanza ulishindwa kula kabisa, baada ya kutumia dawa ulitoka jasho sana, na sasa unasikia nafuu, siku ya pili umekula kwa kujilazimisha lakini siku ya tatu umeamka unatamani kula supu ya nyama, unatamani vyakula kama nyama, mayai hata maziwa.

Pamoja na dawa ulizokunywa, mwili wako ulifanya kazi kubwa ya kupigana na ugonjwa, na ulitumia protini iliyoko mwilini. Hivyo kutamani kwako ni hali ya mwili kutaka kujirudisha katika hali yake ya kawaida. Hata unapouguza mgonjwa na akitamani kula vitu hivyo, kama una uwezo ni muhimu kuvifanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom