Limekuwa jambo la kawaida sasa kwa vijana kujitafutia wake kupitia mitandao ya kijamii. Inawezekana wapo wanaobahatika kupata wake wema lakini binafsi nadhani si jambo jema sana. Asilimia kubwa ya wanaotafuta wake kupitia mitandao huishia kudumbukia katika matatizo lukuki na hivyo hujuta kwanini alimuoa aliyemuoa. Nashauri vijana tumtegee Mungu katika swala la kutafuta mchumba kwani ni muhimu ukapata mtu mnayeendana kwa mambo mengi. Vijana tumrudie Mungu, tumtangulize Mungu katika maisha yetu kwani yeye ndiye jibu la mahitaji yetu yote ya kimwili na kiroho. Ameni.