Kusua sua ujenzi uwanja wa ndege Mwanza ni vita ya Utalii, Siasa na Ubaguzi?

Manelezu,

..suala lingine ni kwamba tunategemea MISAADA kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu.

..sasa hawa wafadhili wana mitizamo tofauti kuhusu vipaumbele vya nchi hii na wakati mwingine haviendani na shauku ya maendeleo ya wananchi wa mikoa ya "pembezoni."

..kwa mfano, sasa hivi ADB wanatoa kipaumbele kwa miradi ya miundombinu inayounganisha nchi majirani.

..ndiyo maana umeona juzi Raisi amefungua mradi wa barabara ya Tz-Ky kule Arusha ambayo imepata fedha toka ADB na JICA.

..kwa hiyo wakati mwingine siyo suala la upendeleo kwa mikoa ya kaskazini bali matokeo ya utegemezi wetu kwa fedha za wafadhili, na mitizamo ya wafadhili hao kuhusu mradi gani wanaona utarudisha pesa zao kwa haraka.

..ndiyo maana sisi wengine tunasema ni vema serikali yetu ikatafuta namna bora zaidi ya kupata fedha za miradi mikubwa ya miundombinu kuliko wanavyofanya sasa hivi ili utekelezaji wa miradi hiyo uendane na vipaumbele vyetu sisi wenyewe.

..tunaweza kulaumu mawaziri tukifikiri wanapendelea au hawajali shida za wananchi wa maeneo fulani, lakini hali halisi ndiyo hiyo niliyoielezea hapo juu.

..kama serikali ingetegemea wafadhili wetu wa kawaida kupata fedha za ujenzi wa barabara ya kusini wananchi wangekuwa bado wanasubiri mpaka leo.

..Ilibidi watafutwe wafadhili wapya wa KUWAIT FUND ambayo wametoa msaada mkubwa kwa ujenzi wa barabara ya kusini. Barabara ya kusini ingeisha mapema wakati wa utawala wa Raisi Mwinyi, tatizo kulitokea vita vya ghuba ambapo Saddam Hussein aliwavamia Kuwait matokeo yake msaada wa fedha za ujenzi wa kusini nao ukasimama kwa muda.

NB:

..nadhani Saudi Fund nao walisaidia ujenzi wa barabara ya kusini.
Incredible analysis
 
Back
Top Bottom