Wasalam wana jamvi,
Takribanni wiki moja imepita tangu tangazo kwa vyombo vya habari ilipotolewa na ofisi ya mkurugenzi wa jiji la Arusha kuhusu kuwasimamisha kazi wakuu wa shule, kwa kuwa imesemekana kuwa katika shule hizo wamo wanafunzi hewa.
Sasa maswali ya kujiuliza...
Je, ni uchunguzi gani wa kisayansi umefanyika hata ukathibitisha taarifa hizo za uwepo wa hao wanafunzi hewa?
Je, ni kweli fedha zilizotumwa na serikali zimetafunwa na hao wakuu wa shule?
Je, bodi za shule hizo pia si zingetakiwa kuwajibishwa kwa kuvunjwa kwa kuwa zinahusika moja kwa moja kupitisha matumizi ya fedha zinazotumwa na serikali.
Je, suala la wanafunzi wanaohamia shule nyingine kama za serikali au binafsi limeangaliwa vipi, na vile vile wanafunzi wanaoacha shule kwa kupata ujauzito, utoro kifo na kadhalika limetolewa muongozo gani ili fedha zao zinazotumwa zirudishwe serikali?
Je, Serikali imetuma auditing team kuthibitisha kuwa kuna fedha zinazosemekana za wanafunzi hewa kuwa zimetafunwa?
Mambo ni mengi ya kujiuliza, lakini inaonekana uamuzi umefanyika kwa uonevu ili baadhi ya kundi fulani waonekane wamefanya kazi ya maana kumbe ni kutafuta umaarufu kwa uonevu.
Pia maamuzi haya yatasabisha kikubwa kuyumba kwa maendeleo ya elimu ususani jiji la Arusha.
Mtazamo wangu, taarifa za mwaka jana zilizotumika kuwahukumu na kuwasimamisha kazi wakuu wa shule ni za kiuonevu.