Kushuka ufanisi wa utendaji kazi tume ya nguvu za atomiki Tanzania

Feb 3, 2018
13
6
Tuwashukuru tena wasomaji wetu wa nyaraka hizi za “Nani atakayeiokoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania” kwa muda wenu mnaoutumia kusoma na kutusaidia kupeleka ujumbe wetu kwa wanaohusika na kuiokoa Tume hii. Kwa kweli mmekuwa msaada mkubwa maana wanaohusika kwa nafasi tofauti wameanza kuchukua hatua za awali kuiokoa Tume hii pamoja na ustawi wetu wafanyakazi. Aidha kumekuwa na kuongezeka kwa vitisho kwetu wafanyakazi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri, pamoja na timu yake ya Mwanasheria na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kama tulivyokwisha kueleza katika waraka wetu wa kwanza. Badala ya kutekeleza maagizo yanayotolewa na wasimamizi wao kwa kufuata taratibu za utumishi wa umma wameanza kutisha wafanyakazi kwa kuanza kutafuta na kuhisi wafanyakazi wanaotoa na kuandaa taarifa hizi. Wafanyakazi tunaomba kuwajulisha viongozi wetu wa Tume wanaoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuwa tumezoea kuishi katika maisha ya vitisho kama swala wa porini ila hali hii tumeichoka ndio maana tunapaza sauti zetu kwa wenye mamlaka watusaidie kutuokoa katika mateso haya. Tupo tayari kutoa ushahidi wa mambo haya popote tutakapoitwa endapo tu tutahakikishiwa usalama wa ajira zetu kama tulivyoeleza kwenye sehemu ya pili ya mfululizo wa nyaraka hizi. Wafanyakazi hatuwezi kuacha kutimiza wajibu wetu wa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kwa sababu ya kuogopa vitisho vya watu wanaotumia vibaya madaraka yao katika ofisi za umma. Wafanyakazi tulieleza vizuri katika sehemu ya kwanza ya waraka huu kuwa mambo haya yanahitaji uchunguzi wa karibu sana kwa kuwa Mwanasheria wa Tume Ndg. Allen Kitutu ameshikilia vitengo karibu vyote vya Tume, huku ukiacha kazi zake za msingi yeye ni Afisa Rasilimali watu, Afisa manunuzi (Procument Officer), Mtaalamu wa maabara ya kupima viwango mionzi kwenye vyakula na mazingira, Afisa usafirishaji, Afisa majengo (Estate Officer) n.k kwa kweli huyu anaingia sekta zote bila hata kujali ushauri kutoka kwa wataalamu husika hivyo amesababisha Tume kupoteza mwelekeo wa kuundwa kwake na hata kukatisha tamaa ya wafanyakazi kufanya kazi zao.

Tunaomba tujikumbushe kidogo Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni nini?

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeundwa kwa Sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2003, yaani, “The Atomic Energy Act No. 7 of 2003.” Kulingana na Sheria hii, Tume imepewa mamlaka ya kisheria kwa niaba ya Serikali ya kusimamia na kudhibiti na kuhamasisha/kukuza (promote) matumizi salama ya vyanzo vya mionzi kwa usalama wa jamii na maendeleo ya Taifa. Tume inaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti chini Mkurugenzi Mkuu, Tume inazo Kurugenzi tatu zinazoongozwa na Wakurugenzi.

Kulingana na kifungu Na. 7(4) cha Sheria ya Nguvu za Atomiki yaani Kurugenzi ya Fedha na Utawala, Kurugenzi ya Udhibiti wa Mionzi Ayonisha na Kurugenzi ya Teknolojia ya Nyuklia zimeundwa.

Majukumu ya TUME ni yafuatayo: -

(a) Kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini;

(b) Kuhamasisha (promote) matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na

(c) Kuishauri Serikali kuhusiana na mikataba ya kimataifa kuhusu matumizi salama na uhamasishaji wa teknolojia ya nyuklia.

Katika waraka huu wa tatu yapo mambo ambao wafanyakazi tunaomba wanaohusika na usimamizi wa Tume kulingana na kifungu Na. 7 (1-4) cha sheria inayoongoza Tume, wayafanyie uchunguzi kutokana na maelezo tutakayo yaeleza ili kuwa na utendaji kazi wenye mafanikio katika Tume kwa kuwa kwa sasa Tume inaelekea kupoteza mwelekeo wake kutokana na aina ya viongozi tulionao kujali maslahi yao binafsi na kusahau kabisa kusudi la uundwaji wa Tume na kuelekeza nguvu kubwa katika upimaji wa mionzi kwenye vyakula na ukusanyaji wa fedha na kusahau usalama wa mionzi katika maeneo mengine kama vile Viwanda (mabati, nondo, vinywaji na uundaji na uunganishaji wa mabomba ya gesi na mafuta), Migodini, kwenye utafiti wa gesi na mafuta, Viwanja vya ndege, Ujenzi wa barabara na Mahospitalini ambako athari za mionzi ni kubwa kuliko kwenye vyakula ambako umekuwa mkazo mkubwa wa uongozi wetu.

Mambo yafuatayo tunaomba yafanyiwe uchunguzi ili kubaini kwa nini yanatokea katika Tume;

a) Uteuzi na uthibitishaji wa Wakurugenzi wa kurugenzi usiofuata taratibu zilizopo kwenye sheria kifungu na. 7 cha Sheria iliyounda Tume

b) Upimaji wa uonevu na usiokuwa na tija kwenye fomu za OPRAS kwa wafanyakazi

c) Kutokuwa na mpango wa kukaa na wafanyakazi wanaoajiriwa na wale waliopo katika Tume “retention scheme of workers”

d) Kuzuiwa wafanyakazi wanaopata ufadhili wa masomo ya juu kwenda masomoni bila sababu za msingi

e) Uuzaji wa liquid nitrogen gas inayozalishwa kwa matumizi ya maabara zilizopo makao makuu ya Tume, Arusha

f) Matumizi mabaya ya madaraka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu

g) Uhalisia wa gharama zilizotumika katika ukarabati wa nyumba za Tume na maabara ya wet Chemistry

h) kutoshiriki Wafanyakazi Kwenye Shughuli na Sherehe za Kitaifa

i) Sababu za Kushuka kwa Utendaji Ndani Ya Tume

Uteuzi na Uthibitishaji wa Wakurugenzi wa Kurugenzi Usiofuata Taratibu Zilizopo Kwenye Sheria Kifungu Na. 7 cha Sheria Iliyounda Tume

Itakumbukwa kuwa tangu Kaimu Mkurugenzi Mkuu aletwe na Wizara Septemba 2016 kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya kwanza ya waraka huu ameachwa kufanya teuzi na kuthibitisha Wakurugenzi bila kufuata taratibu zilizopo. Tangu Februari 2017 amefanya mabadiliko mara tatu ya wakurugenzi bila sababu za msingi ikiwa ni pamoja na kuondoa wale ambao wanakuwa wadadisi kwa mambo ambayo yeye binafsi pamoja na timu yake wanapendelea yafanyika kwa kulazimisha kuyapitisha katika vikao mbalimbali.

Alipoingia katika Tume aliwakuta wakurugenzi wafuatao;

i. Innocent Mapendo …………. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Finance and Adminstration)

ii. Dkt. Mwijarubi Nyaruba …………. Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia (Nuclear Technology)

iii. Dkt. Wilbroad Muhogora ………… Mkurugenzi wa Uthibiti wa Mionzi Ayonisha (Radiation Control)

Wakurugenzi hao wote watatu waliondolewa kwa kigezo tu kuwa utendaji wao wa kazi uko chini ya kiwango kwa kupewa alama (5) katika OPRAS zao za mwaka 2016 kwa tathmini aliyoifanya mwezi Februari 2017 japo kuwa katika ripoti zilizokuwa zinapelekwa katika Bodi ya Wakurugenzi na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ilikuwa inaonyesha utendaji wa kazi za Tume unaimalika tangu Septemba 2016 alipokabidhiwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, kinyume na utendaji wa wasaidizi wake wa karibu yaani wakurugenzi kuonekana utendaji wao umeshuka na ni mbovu. Hizi zilikuwa ni mbinu tu zakuondoa wakurugenzi walikuwa wanaijua miundo mbinu ya utawala uliokuwepo na kuweka utawala wake ili awezekutimiza malengo yake. Alifanya uteuzi mpya na kuweka Makaimu wakurugenzi wapya katika kurugenzi zote tatu (3) hapa hatujua kama hata Bodi ya Wakurugenzi ilishirikishwa au la, wafuatao aliwateua kuwa wakurugenzi;

i. Naiman Mchomvu …… Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Finance and Adminstration)

ii. Dkt. Firmi Banzi …………. Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia (Nuclear Technology)

iii. Dkt. Justine Ngaile ………… Kaimu Mkurugenzi wa Uthibiti wa Mionzi Ayonisha (Radiation Control)

Ijulikane wazi kuwa wakurugenzi hawa waliondolewa walirudi kwenye nafasi zao kulingana na utaalamu wao walioajiriwa nao, jambo ambalo lilionyesha wafanyakazi hawa kukata tamaa ya kufanya kazi. Kutokana na mabadiliko haya Innocent Mapendo alirudi kwenye nafasi yake ya awali ya mkaguzi mkuu wa hesabu za ndani ambayo alikuwa ameikaimisha kwa mfanyakazi mwingine ambaye pia hakuwa na sifa za kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu tu. Aidha ijulikane wazi kuwa Naiman Mchomvu ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa idara ya fedha (Chief accountant) nafasi ambayo ilikaimishwa kwa Hamida Mkunga ambaye hana utaalamu wa uhasibu kwa kuwa yeye aliajiriwa kama Afisa Uchumi na Mipango wa Tume (Economist and Planning officer). Mabadiliko haya ukiyangalia yalikuwa na jambo ndani yake maana baada ya muda si mrefu mkaguzi wa ndani Innocent Mapendo alihamishwa makao makuu ya Tume na kupelekwa ofisi ya Zanzibar ambako anatumika kama mhasibu wa kawaida mpaka wakati waraka huu unaandikwa na wafanyakazi wa Tume. Hatujui kama mabadiliko haya ya mkaguzi wa ndani yalibarikiwa na Bodi ya wakurugenzi au Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, pia jambo hili tunaomba lifanyiwe uchunguzi kwa kuwa nafasi ya mkaguzi wa ndani na msimamizi mkuu wa uhasibu/fedha zinatia mashaka sana kwa usitawi wa Tume. Baada ya mabadiliko hayo uongozi wa wakurugenzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu alifanya mabadiliko ya wakurugenzi hao kwa kumthibitisha Naiman Mchomvu kuwa mkurugenzi wa fedha na utawala na kumuondoa Dkt. Justine Ngaile na kumpeleka ofisi ya mpaka wa Namanga hivyo kufanya orodha ya wakurugenzi kuwa kama ifuatavyo mpaka wakati waraka huu unaandikwa;

i. Naiman Mchomvu …………. Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Finance and Adminstration)

iii. John Ngatunga …………Kaimu Mkurugenzi wa Uthibiti wa Mionzi Ayonisha (Radiation Control)

Wafanyakazi tunaamini mabadiliko ya namna hii yanaondoa kujiamini katika utendaji kazi kwa viongozi wanaoteuliwa hivyo inapunguza ubunifu katika utendaji wao wa kazi, mabadiliko haya kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu yamekuwa yakifanyika pia kwa wakuu wa idara mbalimbali ikiwa ni pamoja na idara ya Mionzi Ayonishi, Idara ya kupima viashiria vya mionzi kwenye chakula na mazingira, Ofisi ya mpaka ya Namanga na Ofisi ya kanda ya Dar es salaam. Kuongezeka kwa mabadiliko haya ya mara kwa mara kunatia wasiwasi kwa wafanyakazi na viongozi wanaoteuliwa hivyo kufanya utendaji kazi kushuka tofauti na inavyoripotiwa na utawala wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi tangu septemba, 2016. Tunaomba wanaohusika kufanya uchunguzi katika jambo hili na kumshauri Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuwaamini watu anaowateua ili Tume iwezekufanya kazi zake kulingana na sheria iliyoiunda na kwa mafanikio.

Upimaji wa uonevu na usiokuwa na tija kwa wafanyakazi kwenye fomu za OPRAS

Tangu ateuliwe Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kumekuwa na ukatishaji tamaa mkubwa sana kwa wafanyakazi na kupunguza morali kwa kiwango cha juu sana. hili linatokana na kuwepo kwa vitendo vya kutuambia wafanyakazi hatufanyi kazi ilikuwa ripoti mbalimbali wanazoziandika kwenye mamlaka husika zinakuwa zikionyesha kuwa utendaji kazi katika Tume umeongezeka pamoja na kuwa hatuelewi ni vipimo gani vinatumika katika kutoa na kupata takwimu hizo. Aidha wafanyakazi tulikatishwa tamaa zaidi kipindi ambapo tathmini ya kazi zetu ilifanyika kwa kupitia kazi ambazo kila mmoja wetu alizijaza kwenye fomu za OPRAS na kuambiwa ni wafanyakazi wanne tu ambao walikuwa wamefikia viwango vya ufanyaji kazi ambavyo alikuwa ameviweka Kaimu Mkurugenzi Mkuu na wengine wote tulikuwa chini ya wastani hivyo hawa wafanyakazi wanne ndio walikuwa wanastahili kupandishwa daraja. Wafanyakazi hao ni Naiman mchovu( Mkurugenzi Fedha na Utawala), Allen kitutu (Mwanashria wa Tume), Hamida Mkunga(Kaimu Msimamizi wa uhasibu) na Abel Ntwa (Mkuu wa Idara ya maabara ya upimaji wa Mionzi kwenye vyakula na Mazingira). Ukweli jambo hili linatukatisha tamaa wafanyakazi, tunaomba wanaohusika na usimamizi wa utendaji kazi wa Tume walisimamie na kulikemea jambo hili kwa kuwa linapunguza ustawi kwa wafanyakazi. Aidha tunaamini kwamba tathmini katika mfumo huu wa OPRAS ni wa mwendeleo na si wa wakati mmoja hali ambayo kama kulikuwa na kutokuwajibika kwa wafanyakazi kungekemewa na kushauriwa mapema badala ya kusubiri na kutoa tathmini za aina hii. Tunaamini kuwa pamoja na kukatishwa tamaa kwa kiwango hiki wafanyakazi tumeendelea kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu pamoja na kuwa na mazingira hatarishi katika utumishi wetu. Wizara husika na Bodi ya wakurugenzi tunawaomba mfanyie uchunguzi jambo hili ili kutujengea wafanyakazi mazingira salama katika utumishi wetu.

Kutokuwa na mpango wa kukaa na wafanyakazi wanaoajiriwa na wale waliopo “retention scheme of workers”

Ukisoma taarifa nyingi sana za Tume kwenda Bodi ya wakurugenzi na Wizarani kumekuwa na malalamiko mengi ya kuwa Tume ina upungufu mkubwa wa wafanyakazi, ni kweli Tume ina upungufu wa wafanyakazi hasa maeneo ya utaalamu hili linatokana na unyeti wa taaluma yenyewe “ Nguvu za Atomiki” ambapo sio wataalamu wengi wanaosoma masomo ya Fizikia, Kemia, Biolojia na Hisabati katika ngazi za Elimu ya juu zikiwemo Teknolojia ya Nyuklia. Aidha hili lililoelezwa ni kwa upande mmoja bali hata hawa wataalamu wanapopatikana ofisi ya Mkurugenzi Mkuu imekuwa haina mpango wa kukaa nao na kuwaendeleza kwa makusudi na hili limekuwa tatizo kubwa zaidi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu “Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri” tangu alipoteuliwa na wizara Septemba, 2016. Tunaomba tutoe mifano michache tu katika jambo hili, Kaimu Mkurugenzi Mkuu alimkataa Bw. Atumaini Makoba aliyekuwa ameajiriwa kupitia Tume ya Utumishi, Ofisi ya Raisi na Menejimenti ya utumishi wa umma kama Mtaalamu wa Fizikia ya Mionzi daraja la I na kumrudisha manispaa ya Temeke alikokuwa ameajiriwa awali bila sababu za msingi. Pili mahakama ilimurudisha kazini mfanyakazi ambaye alikuwa amefukuzwa kazi bila kosa la msingi Didas Shao na Kaimu Mkurugenzi huyu akamkataa Didas Shao ambaye alikuwa ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Nyuklia daraja la I pamoja na kuwa mpaka sasa hataki kumlipa haki zake. Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu amewahamisha wafanyakazi wawili kwenda Wizara ni ambao ni Edwin Konzo – mtaalamu wa Fizikia ya Mionzi daraja la II na Ebenezer Kimaro Mtafiti wa Sayansi ya Nyuklia daraja la I bila kuombwa na wizara husika, jambo ambalo tunajua ni kwa sababu tu za kuwa viongozi wa chama cha wafanyakazi ambayo tumeyaeleza vizuri katika waraka wa kwanza na wa pili wa Nani atakayeikoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania. Kutokana na sababu za vitisho na matumizi mabaya ya madaraka na kutokujali utaalamu wa wafanyakazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu alisababisha Sadiki Mutabuzi kuamua kuacha kazi katika Tume, huyu alikuwa ni mtaalamu mwandamizi daraja la I katika matengenezo ya vifaa vinavyotoa Mionzi ayonishi nchini ikiwa ni pamoja na mashine za X-ray, CT Scanner, Mashine za kupimia kansa ya Matiti nk. Hii ni mifano michache tu ambayo tumeona tuitoe, tunaamini uchunguzi ukifanyika katika jambo hili mengi yatajulikana ambayo yanafanya wafanyakazi kukataliwa, kuhamishwa, kufukuzwa na wengine kuacha kazi au kuomba kuhamishia utumishi wao kwa waajiri wengi. Ifahamike kuwa mifano hiyo yote imetokea kati ya Septemba, 2016 na sasa yaani kipindi ambacho Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akiisimamia Tume. Vyombo vinavyosimamia Tume tusaidieni kuiokoa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.

Kuzuiwa wafanyakazi wanaopata ufadhili wa masomo ya juu

Ni jambo la kisheria kwa mwajiri kuwaendeleza wafanyakazi wake kimasomo ili kuongeza uwezo wa wafanyakazi katika utendaji wa kazi kwa ufanisi. Wafanyakazi tunatoa malalamiko yetu kwa uongozi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume kwa tabia iliyojitokeza katika kipindi cha utawala wake kutoruhusu wafanyakazi kwenda masomoni wanapopata nafasi hizo za masomo ya juu mara nyingi bila hata kupewa sababu za kuzuiwa. Ifahamike wazi kuwa wafanyakazi tunasema haya baada ya zaidi ya wafanyakazi watano (5) kutopewa ruhusa ya masomo ya masters degree na wengine wawili (2) Phd degree wakiwa na udhamini wa masomo hayo kwa muda wote wa masomo. Aidha wafanyakazi walioko masomoni ulikuwepo utaratibu wa kupewa baadhi ya allowance ambazo zilikuwa zinatolewa na mwajiri kama vile house allowance wanapokuwa masomoni kulingana na taratibu za Tume. Kaimu Mkurugenzi Mkuu amezifuta ili kujenga mazingira magumu kwa familia za wafanyakazi waliopo masomoni. Mambo haya yanatokana na kutokuwepo kwa utaratibu unaofahamika na wafanyakazi wa kuwaendeleza kimasomo (Training Scheme for workers). Kwa wakati huu wapo wafanyakazi waliopo masomoni ambao ruhusa za masomo walipewa wakati wa Mkurugenzi Mkuu aliyepita. Umuhimu wa wafanyakazi wa Tume kujiendeleza kimasomo unatokana majukumu iliyonayo Tume hii kwa maendeleo tarajiwa ya taifa kwa ujumla katika nyanja za viwanda na miundombinu. Tunaomba Bodi ya Wakurugenzi na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuchunguza uhalisia wa mambo haya ili kuongeza ustawi wa wafanyakazi na Tume kwa ujumla.

Uuzaji wa liquid nitrogen gas inayozalishwa kwa matumizi ya ofisi

Kwenye waraka uliotangulia wafanyakazi tulieleza matumizi mabaya ya Madaraka ya viongozi wa Tume hasa timu iliyoundwa kati ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa fedha na utawala na Mwanasheria wa Tume. Kumekuwa pia na ukaribu unaotia wasiwasi kati ya Mwanasheria wa Tume na Mkuu wa Idara inayosimamia maabara ya upimaji wa mionzi kwenye vyakula ambayo pia ndio inazalisha gesi ya liquid nitrogen ambayo inatumika katika mitambo inayotumika katika upimaji wa viasili vya mionzi kwenye sampuli za chakula cha binadamu na mifugo. Mtambo unaotumika katika uzalishaji wa gesi hii ni sehemu ya vifaa vilivyoletwa chini ya mradi mkubwa wa umoja wa nchi za ulaya “European Union” ambao ulianza kuratibiwa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu aliyepita, marehemu Iddi Mkilaha Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, kutoka na Tume kununua gas kwa wazalishaji wengine nchini tangu miaka ya 1998 Tume ilipoanza kutoa huduma ya upimaji vyakula. Uzalishaji wa gesi hii katika Tume ilichukuliwa pia kama mradi wa uzalishaji fedha kwa ajili ya kuimalisha matengenezo ya vifaa vya maabara ili kuwe na huduma ya uhakika na yenye kuendelea kwa usalama wa wananchi kwa ujumla. Wafanyakazi tunaamini kuwa mipango ya uuzaji wa gesi hii umewekewa taratibu nzuri ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa Tume na Taifa kwa ujumla. Kumekuwa na mwenendo unaoonyesha kuwa Mkuu wa Idara na Mwanasheria wa Tume wamekuwa wakiuza gesi siku za jumamosi na jumapili mara kadhaa jambo ambalo linaleta wasiwasi mkubwa kama uuzaji huu unafuata taratibu zilizowekwa maana katika siku hizi ofisi zingine za Tume kama uhasibu huwa zimefungwa. Tunashauri taratibu za uuzaji gesi hii zifahamike, uchunguzi kwa wahusika ufanyike japo kuwa inawezekana kukawa na ugumu kulingama na mfumo wa uongozi uliopo kama tulivyoeleza hapo juu kuwa uongozi unawekwa kwa matakwa ya kundi fulani kwa manufaa binafsi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu na washirika wake.

Matumizi mabaya madaraka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu kupanga vizuri safu yake ya madaraka kwa jinsi ilivyompendeza imetengeneza mianya ya kufanya anavyotaka katika matumizi na malipo katika mali na fedha za Tume. Wafanyakazi tunaona tuwajulishe wasimamizi wa Tume mambo machache yanayofanyika na Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri.

· Amekuwa akiondoka na gari la Tume kwenda katika likizo zake za mwaka na dereva kwa wakati wote wa likizo yake, dereva amekuwa akilipwa pesa ya kujikimu wakati wote wa likizo ya Mkurugenzi Mkuu, rejea likizo yake ya Januari 2018. Ambapo katika kipindi hicho cha likizo gari mbili za Tume aina ya Nissan zimepata ajali zikiwa katika harakati za kutumika wakati wa likizo.

· Mkurugenzi huyu anaishi katika nyumba ya serikali ambayo inahudumiwa kwa gharama zote ikiwemo umeme, maji na mlinzi kwa gharama ya Tume pamoja na kupewa huduma ya usafiri muda wote anapokuwa katika majukumu yake ya kazi jambo linaloshangaza ni kwamba kila mwezi analipwa tena allowance ya mafuta, nyumba na utility ambazo hatuamini kuwa anasitahili kulipwa. Tunaomba jambo hili liweze kuchunguzwa kama halipo sawa kwa kuwa linaitia hasara Tume isio ya lazima.

· Kutokana na unyeti wa taaluma ya nguvu za Atomiki (Teknolojia ya Nyuklia) Shirikika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) linaendesha semina nyingi kwa viongozi na wafanyakazi wa Taasisi zinazofanana na Tume duniani. Kutokana na ukweli huu baada ya mwongozo wa serikali kuhusu kutokujihusisha na ulipaji wa gharama za safari za nje ya nchi kwa sehemu kubwa. Menejimenti ya Tume ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu iliamuru kuwa viongozi na wafanyakazi watashiriki kwenye mafunzo na semina hizo bila kuwa na malipo yeyote ya ziada kutoka kwenye Tume isipokuwa gharama zote zitagharamiwa na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) na si vinginevyo na ndivyo imekuwa ikifanyika kwa kuwa mafunzo haya hufanyika mara nyingi kwa wafanyakazi na viongozi duniani kote kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na matumizi salama kwa vyanzo vyote vya mionzi duniani. Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akijilipa tofauti ya fedha ya kujikimu (Perdiem allowance) nje ya nchi tofauti na makubaliano aliyoyaweka kwa safari zake zote za nje. Jambo hili tunaomba lichunguzwe na wasimamizi kama lipo kinyume cha utaratibu kwa kuwa IAEA huwa katika malipo unayopewa muhusika wa mafunzo inahusiwa pia perdiem allowance kulingana na nchi ambayo mafunzo, semina, kongamano au mkutano unapofanyika.

· Kutokana na mfumo wa uongozi aliouweka kama tulivyoeleza hapo juu yaani wa Kurugenzi ya Fedha na Utawala pamoja na mwanasheria Kaimu Mkurugenzi Mkuu amekuwa akilipwa fedha za safari za kikazi hata anapokuwa likizo, kwa mfano kuna malipo ya safari ya kikazi Dodoma ya 16/01/2018 wakati alikuwa likizo tangu mapema Januari, 2018 mpaka 29 Januari, 2018 alipomaliza likizo yake.

· Kwa mujibu wa taaluma yake ya kijeshi tunaamini anastahili kujilinda wakati wote, lakini tunaamini pia jambo hili linatakiwa kufanyika kwa usiri hasa anapokuwa ofisini akitimiza majukumu yake ya Mkurugenzi Mkuu kwa kuwa amekuwa akija na bastola ofisini na wakati mwingine akiwa na uniform za kijeshi. Wafanyakazi tunaomba apunguze haya maana tunaheshimu na kufahamu taaluma yake hii muhimu kwa usitawi wa taifa letu. Vifaa hivi visitumike kama sehemu ya utisho kwa wafanyakazi kudai haki zao wakati wakiwa wametimiza wajibu wao.

Uhalisia wa gharama zilizotumika katika ukarabati wa nyumba za Tume

Tume inamiliki nyumba nne (4) kwa makazi ya watumishi ikiwa ni pamoja na nyumba ya Mkurugenzi Mkuu iliyopo eneo la SDA Njiro, Nyumba mbili za watumishi zipi eneo la Nalopa Njiro na nyumba moja ipo eneo la sokoni Mbauda. Nyumba hizi zote wanaishi watumishi wanazilipia kodi kwa kila mwezi. Mwanzo mwa mwaka huu umefanyika ukarabati wa nyumba mbili zilizopo Nalopa Njiro, ukarabati huu unakadiliwa kutumia takribani 117,000,000/= kwa taarifa, ikijumlisha ukaratabati wa wet chemistry lab ambayo tunaamini itakuwepo kwenye jengo jipya linalojegwa kwa hiyo hakuna ulazima wa kupoteza gharama zingine kwenye kukarabati vyumba ambavyo vinaweza kutumika kwa kazi zingine. Kufikia wakati huu waraka unaandikwa kiasi cha shilingi 40,000,000 zilikuwa zimeshalipwa kwa ajili ya hiyo kazi. Wafanyakazi tunaomba uchunguzi wa gharama hizi ufanyike kwa kuwa hazina uhilisia na kilichofanyika. Aidha ukumbukwe fedha ilitumika bila uthibitisho wa Baraza la wafanyakazi na Bodi ya wakurugenzi. Kumekuwa na ukarabati tofauti tofauti ukiendelea hapa ofisi ambao wafanyakazi unatumika na watawala katika kuiba fedha za Tume kwa kuwa mipango ya karabati hizi hupangwa na watu watatu tu kwa kweli hapa panakuwa na kitu cha tofauti.

Kutoshiriki Wafanyakazi Kwenye Shughuli na Sherehe za Kitaifa

Kutakana na Brigedia Jenerali Fulgence Simon Msafiri kuchukia uwepo wa chama cha wafanyakazi eneo la kazi imefikia mahali kwamba ushiriki wawafanyakazi kwenye sherehe za kitaifa zinazoratibiwa na vyama vya wafanyakazi duniani imekuwa kama hisani kwa wafanyakazi mpaka inafikia mahali pa kuzuwia kushiriki kwenye shughuli na sherehe hizo. Tunaomba kutoa mfano wa hivi karibuni ambapo mwaliko wa ushiriki wa wafanyakazi wanawake katika maandalizi ya siku ya wanawake duniani yaani (8/3/2018) ulipoletwa katika Tume Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu aliukataa eti kwa sababu tu viongozi wa Halmashauri ya Chama cha Wafanyakazi haikuwepo ili hali uongozi wa wanawake katika Tume upo na unajitegemea ila Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi hutumia wajumbe wake kama sehemu ya ushirikishwaji wa wanawake katika mambo ambayo vikao vya Chama hujadili kwa ajili ya wafanyakazi. Aidha kwa sababu hiyo kutokuwepo kwa viongozi wa Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi hakukuwa sababu ya msingi kwake kuwazuia wafanyakazi wanawake kushiriki katika siku yao muhimu “Siku ya Wanawake Duniani”.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu anajua sababu za kwanini Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi kutokuwepo katika Tume kulikotokana na unyanyasaji wake kwa viongozi wa Chama cha wafanyakazi kama tulivyoeleza kwenye nyaraka zilizopita, unyanyasaji huu wa viongozi ndio ulipelekea kumufukuza kazi mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi ndugu Barnaba Chimatila bila sababu za msingi baada ya kuwa ndio kiongozi peke yake wa Chama cha wafanyakazi aliyekuwa amebaki baada ya wengine kuhamishwa nje na ndani ya Tume na wengine kuchukua hatua za kujiuzulu kutokana na manyanyaso ya wazi kwa viongozi wa Halmashauri ya Chama cha wafanyakazi, ambayo yalihusisha kulazimishwa kushiriki kwenye vikao ambavyo havikuwa halali, baada ya kufukuzwa kwenye vikao hivyo Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha wafanyakazi. Tukitoa mifano tu ya viongozi wa Halmashauri waliopewa manyanyaso ya wazi kwa kulazimishwa kushiriki vikao hivyo ni Christina Nyakyi na Agrey Kitosi ambao baadae kama mwendelezo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya wanawake Christina Nyakyi alimhamisha makao makuu ya Tume kwenda kituo cha Tarakea mpakani na Kenya ambako yupo mpaka wakati waraka huu unapoandikwa. Tuendelee kuwaomba Bodi ya wakurugenzi na Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia mtusaidie ili tuweze kuwa na nafasi za ushiriki katika matukio ya kitaifa yanahusisha wafanyakazi wote duniani maana hii inatupa dalili za sisi wafanyakazi kutoshiriki sikukuu za Meimosi 2018 labda kwa sababu hizi hizi zilizotolewa kwa wanawake kutokushiriki Sikukuu ya wanawake duniani.

Sababu za Kushuka kwa Utendaji Ndani Ya Tume

Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika vikao vyake na wafanyakazi vya tarehe 7/3/2018, 8/03/2018 na 9/03/2018 alikiri kushuka kwa utendaji kazi katika Tume, ambao kwa maelezo yake mwenyewe, uzorotaji huu wa utendaji umeanza kipindi cha mwaka 2016 hadi sasa japokuwa alikiri pia kuwa hapa katika utendaji ulipanda kidogo na kuanza kushuka tena. Ikumbukwe kwamba Mkurugenzi huyu aliletwa hapa kwenye Tume ili kuboresha utendaji wa Tume ambao ulikuwa umezorota kwa mujibu wa waliomleta. Lakini kinyume chake utendaji wa Tume umezidi kuzorota zaidi katika kipindi chote ambacho ameongoza Tume hii. Lakini uzorotaji huu wa utendaji kazi katika kipindi hiki sio jambo la kushangaza hata kidogo kutokana na mambo kadhaa yaliyojitokeza katika kipindi chake. Mambo haya yamejitokeza kutokana na yeye (Kaimu Mkurugenzi mkuu) kutegemea kupewa ushauri na “akili ndogo” (Mwanasheria wa Tume na Mkurugenzi wa fedha na utawala) ambazo hazina uzoefu wowote na majukumu ya msingi ya Tume kwa mujibu wa sheria iliyounda Tume ama kwa makusudi ili kumharibia na kujineemesha wao au kwa ujumla wao wa kutokujua makujumu ya msingi ya Tume kama yalivyoelezwa kwa ufupi hapo mwanzo mwa waraka huu. Mkurugenzi huyu amekuwa akitumia ushauri wa watu hawa wawili na kuacha kusikiliza ushauri unaotolewa na viongozi (wataalam) wengine waliopo kwenye Menejimenti/wafanyakazi wenye uzoefu wa kutosha, tena wakiwamo ambao wana uzoefu wa kitaalam uliobobea katika majukumu ya msingi ya Tume kwa muda mrefu. Katika kusikiliza ushauri wa “akili ndogo” Mkurugenzi huyu amekuwa akihamisha hamisha wafanyakazi pasipo kuzingatia ufanisi wa majukumu ya Tume. Mkurugenzi huyu tangu ameletwa hapa kwenye Tume ameshahamisha wafanyakazi zaidi ya 12 na kufukuza wafanyakazi watatu na kuhamisha nje ya Tume wafanyakazi watatu bila kuzingatia mahitaji halisi ya Tume katika kuboresha utendaji kazi kwa ufanisi. Aidha itakumbukwa kuwa kumekuwa na upungufu wa wafanyakazi wataalam makao makuu kwa muda mrefu kulingana na ripoti mbalimbali za Tume. Hamisha hamisha hii ambayo imefanyika kama adhabu kwa walengwa ukiifuatilia utakuta kuwa washauri wakuu wa hamisha hii ni wale wale “akili ndogo”. Kwa mujibu wa kifungu cha sita (6) cha sheria namba 7 ya nguvu za atomiki ya mwaka 2003, Tume ina majukumu (functions)takribani 5 yenye vipengele vingi hasa lile jukumu la kwanza, lakini kimsingi ni kipengele kidogo kimoja cha jukumu namba moja lenye vipengele 24 kinachopewa kipaumbele katika hivyo 24 ambacho ni udhibiti wa vyanzo vya mionzi katika vyakula vinavyoingia na kutoka nchini. Jukumu hili kimsingi halina umuhimu kuzidi majukumu mengine, kusababisha kupeleka wasimamizi kwenye mipaka kwa kiwango kilichofanyika mpaka sasa. Katika hamisha hamisha hii isiyokuwa na tija, Tume imejikuta ikiwahamishia mipakani wanasayansi (wataalam) waliobobea, wengine wakiwa na shahada za uzamifu (PhD) kwenda kutekeleza majukumu ambayo hata mtu mwenye Stashahada (Diploma) angeweza kuyatekeleza kwa ufanisi. Wataalamu hawa wangetumika kufanya tafiti na kutumia vizuri maabara za Tume ambazo zimepatiwa vifaa vya kutosha wangewezesha utendaji wa Tume kuwa wa kiwango cha juu sana kuliko kuwatumia kama wakusanya mapato mipakani. Mifano ya wafanyakazi waliohamishiwa mipakani huku utaalam wao ukihitajika zaidi kwenye majukumu mengine makubwa ya Tume pamoja na viwango vyao vya elimu kwenye mabano ni pamoja na:

1. Justine Ngaile (PhD in Nuclear Physics) ambaye ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 aliyehamishiwa mpaka wa Namanga

2. Ebenezer Kimaro (MSc Physics) uzoefu wa zaidi ya miaka 15 aliyekuwa amehamishiwa mpaka wa Sirari na baadae kuhamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kile kilichoitwa kuwa ni kutokana na umuhimu wa kazi wizarani.

3. Lazaro Meza (MSc ) uzoefu wa zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa mpaka wa Tunduma

4. Mungubariki Nyaki (MSc Physics) uzoefu zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa bandari ya Tanga

5. Sadiki Mutabuzi (MSc. Eng) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyehamishiwa mpaka wa Holili, lakini aliacha kazi kutokana na kutokubaliana na uhamisho huu

6. Christina Nyakyi (MSc in Electronic and Telecommunication) uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyehamishiwa mpaka wa Tarakea

7. Hilal Hussein (MSc) uzoefu zaidi ya miaka 6 aliyehamishiwa mpaka wa Horohoro

8. Leonid Nkuba (MSc in Physics) uzoefu zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa mpaka wa Mtukula

9. Tunu Kaijage (Postgraduate Diploma in Radiation Protection) uzoefu zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa mpaka wa Sirari

10. Erasto Kayumbe (MSc IT) uzoefu zaidi ya miaka 3 aliyehamishiwa mpaka wa Holili

11. Goodchance Mboya (BSc) mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 10 katika utaalam wa Dosimetry aliyehamishiwa Mtwara

12. Mchibya Matulanya (MSc ) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa Mtwara

13. Miguta Ngulimi (…) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa Songea

14. Edwin Konzo (BSc) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kilichosemekana kuwa ni kutokana na umuhimu wa kazi Wizarani hapo.

15. Wilson Kitara (….) ambaye ana uzoefu wa miaka 5 aliyeajiriwa kama Nuclear Instrumentation technician amehamishiwa kituo cha mpaka wa Rusumo

16. Fadhili Msumali (….) mwenye uzoefu wa miaka 5 ambaye aliajiriwa kama Nuclear Instrumentation technician aliyehamishiwa kituo cha Namanga

17. Innocent Mapendo (MBA+CPA(T)) mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 7 aliyeajiriwa kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani (Chief Internal Auditor) alihamishiwa ofisi ya Kanda Zanzibar kama mhasibu wa kawaida. Uhamisho huu ulikuwa ni kama adhabu kutokana na kuonekana kuingilia maslahi ya hawa watu wawili (Mwanasheria na DFA).

18. Alex Muhulo (Msc) uzoefu wa zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa katika ofisi ya Dar es Salaam

19. Wilson Ngoye (Msc in medical radiograph) uzoefu wa zaidi ya miaka 10 aliyehamishiwa ofisi ya Dar es Salaam

20. Amasi Aloyce (Msc) uzoefu wa zaidi ya miaka 5 aliyehamishiwa katika ofisi ya Dar es Salaam

21. Atumain Makoba (Msc Physics) ambaye aliajiriwa kwa taratibu za Tume ya Utumishi wa umma ofis ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kutoka Manispaa ya Temeke kama Mtaalamu wa Fizikia ya Mionzi daraja la I, baada ya muda wake wa matazamio (Probation period) ya Mwaka mmoja pamoja na maendeleo mazuri aliyokuwa akionyesha katika ufanyaji kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu alimrudisha kwa mwajiri wake wa awali bila sababu za msingi eti alikuwa hamtaki kumuona akiwa mfanyakazi wa TAEC.

Wasimamizi wa Tume mnaweza kuona kuwa hamisha hamisha hii ambayo imefanyika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyu ambaye hajafikisha hata miaka miwili (2) ndani ya Tume, ikifuatiliwa kwa karibu itagundulika kuwa hazikufanyika katika muktadha wa kuimarisha utendaji kazi wa Tume, zaidi ya kuendelea kuzorotesha utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Tume. Kwa sababu nyingi ya hamisho hizi zilifanyika katika kuwakomoa wahusika aidha kutokana na misimamo yao katika kusimamia maslahi ya wafanyakazi na maslahi ya Tume kwa ujumla wake. Hivyo basi, Mkurugenzi Mkuu anaposema utendaji wa Tume umeshuka inabidi na yeye ajitathmini kama kweli anafaa kuendelea kuongoza Taasisi hii muhimu katika nchi. Hivi alitegemea utendaji na ufanisi katika Tume baada ya kuhamisha wataalamu wote hawa waliosomeshwa kwa fedha za walipa kodi wa nchi hii? Halafu leo hii Mkurugenzi mkuu huyu huyu analalamika kuwa Tume haina wafanyakazi wa kutosha, wakati kuna wafanyakazi wenye uzoefu wa kutosha anawahamishia Wizarani bila hata ya kuombwa na Wizara husika kwa madai ya kwenda kuongeza ufanisi wizarani. Leo hii baada ya kufanya madudu kwa muda wote aliokabidhiwa Tume anatafuta mchawi aliyemloga wakati wachawi anao hapa hapa wamemzunguka. Inabidi ajitafakari na kujitathmini kama kweli ana uwezo wa kuvaa viatu vya kuongoza Taasisi hii muhimu kwa maendeleao ya Taifa. Wasimamizi wa Tume hii liangalieni hili kwa makini na kulichunguza ukweli wake. Maana hawa watu wawili waliitajwa hapo juu yaani Allen Kitutu na Naiman Mchomvu wana mpango wa makusudi wa kuiua hii Tume kwa maslahi yao binafsi.

WAFANYAKAZI TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA
 
hawa wanajeshi waloteuliwa ni tatizo sana sio kwenu tuu....waltakiwa wawe ma rc na ma dc bhaaas

bodi haiyaoni hayo? mtaften member 1 wa bodi mumpe hizo taarifa in details
that's one
mbili..
tafteni mwandishi wa habari wa magazeti(sio tv wala radio)itasaidia kutia presha
kwa wasimamizi!!!!!
 
Justine Ngaile (PhD in Nuclear Physics) ambaye ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 aliyehamishiwa mpaka wa Namanga

watu kama hawa nchi za wenzetu kama RUSSIA wanakuwa washauri wa rais namna kuendeleza taifa kwa nuclear I wonder bado kuna mijitu eti inaogopa technology ya umeme wa nuclear, cause hawajui faida zake .
Tanzania wanamtupa mpakani how come akafanye nini kule kweli ndio maana trump anatuita nini vile ,

JUSTINE >>>>>>
If one of our positions matches your goals and expertise, please submit your cover letter, résumé and salary requirements, along with the NEI employment application to resumes@nei.org. Indicate the job title of the vacant position. Please, no phone calls. You also can mail your information to:

Nuclear Energy Institute
Human Resources Director
1201 F Street, NW, Suite 1100
Washington, DC 20004
 
Shithole countries
 
Shithole countries
EWAAAAA

CHEKI WENZETU HAPA CHINI UTAELEWA NA HAO NDIO WANATUAMINISHA KWAMBA NI HATARI WAO WANATUMIA KWA BIDII SANA.

U.S. electricity production costs from 2000 to 2014, by source (in cents per kilowatt hour)*

184712-blank-100.png

Costs

• Coal 3.29
• Gas 4.12
• Nuclear 2.34
• Petroleum 21.56

© Statista 2018

Duuh!
Mbona hii Tume ina RASILIMALI watu ya kutosha kabisa, nadhani hao wataalam wangetumiwa vizuri ili kuipaisha hii sera ya MAENDELEO YA VIWANDA.
 
kibongo bongo watu wakipewa vyeo wanageuka kuwa miungu watu yapo kila sekta kila idara.... tukomae tu tupambane na hali zetu ...ngawa inavunja moyo sana
 
Chapa kazi ndg acha majungu, hao wapo hapo kwa kazi maalumu.
 
hawa wanajeshi waloteuliwa ni tatizo sana sio kwenu tuu....waltakiwa wawe ma rc na ma dc bhaaas

bodi haiyaoni hayo? mtaften member 1 wa bodi mumpe hizo taarifa in details
that's one
mbili..
tafteni mwandishi wa habari wa magazeti(sio tv wala radio)itasaidia kutia presha
kwa wasimamizi!!!!!

Huyu Kaimu Mkurugenzi Mkuu aliletwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ana zaidi ya mwaka ana act hiyo nafasi.

Bodi ya wakurugenzi kuna baadhi ya mambo tunaamini inayafahamu vizuri na inao uwezo wa kuyafanyia kazi kwa haraka sana.
 
Justine Ngaile (PhD in Nuclear Physics) ambaye ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 aliyehamishiwa mpaka wa Namanga

watu kama hawa nchi za wenzetu kama RUSSIA wanakuwa washauri wa rais namna kuendeleza taifa kwa nuclear I wonder bado kuna mijitu eti inaogopa technology ya umeme wa nuclear, cause hawajui faida zake .
Tanzania wanamtupa mpakani how come akafanye nini kule kweli ndio maana trump anatuita nini vile ,

JUSTINE >>>>>>
If one of our positions matches your goals and expertise, please submit your cover letter, résumé and salary requirements, along with the NEI employment application to resumes@nei.org. Indicate the job title of the vacant position. Please, no phone calls. You also can mail your information to:

Nuclear Energy Institute
Human Resources Director
1201 F Street, NW, Suite 1100
Washington, DC 20004

Haya mambo yakichunguzwa ukweli wake uko wazi na tutatoa ushirikiano, mtu kama huyu hapendi mambo ya kona kona wala mambo ya chini ya meza na huwa anapenda kutendea haki kila mtu sasa wenyewe watu wa namna hii hawawataki hata kidogo badala yake utahamishiwa mpakani ukakate invoice kwa ma-clearing agents.
 
EWAAAAA

CHEKI WENZETU HAPA CHINI UTAELEWA NA HAO NDIO WANATUAMINISHA KWAMBA NI HATARI WAO WANATUMIA KWA BIDII SANA.

U.S. electricity production costs from 2000 to 2014, by source (in cents per kilowatt hour)*

U.S. electricity production costs from 2000 to 2014, by source (in cents per kilowatt hour)*
184712-blank-100.png

Costs

• Coal 3.29
• Gas 4.12
• Nuclear 2.34
• Petroleum 21.56

Statista 2018

Uko sahihi ndugu na asante kwa takwimu maridhawa. Hii Taasisi ni muhimu sana kuelekea kwenye uchumi wa viwanda kama Mh Rais anavyotaka pamoja na usalama wa nchi ila watu wamepageuza sehemu ya kupigia dili na kunyanyasa wengine.
 
Duuh!
Mbona hii Tume ina RASILIMALI watu ya kutosha kabisa, nadhani hao wataalam wangetumiwa vizuri ili kuipaisha hii sera ya MAENDELEO YA VIWANDA.

Tatizo la kuongozwa na hizo tunazoita akili ndogo kwa sababu hawaoni umuhimu wa hii Taasisi
 
Nilipata habari za hii tume tangu alipoingia huyo mjeshi kama mkurugenzi mkuu yani ni shida tena Sheedah kweli kweli..!
 
Mimi nina swali moja kwenu tu
Hii commision saivi imeingiza regulations kwenye imports---hasa through airport entry---mnataka sample ya kila mzigo mpime na mnau-charge
Hii kweli ni kuhamasisha/kukuza (promote) matumizi salama ya vyanzo vya mionzi?
Sio pesa tu mnatafuta?
Mnaweka biashara na ajira za watu katika hali tete sana --- ada na bureaucracy mbaya sana
 
Mlifikia wapi na haya madai yenu? Jambo liko very detailed!! Kuna lolote lilifanyika? Kuna watu wana ujinga sana wakipewa vyeo! Yote hayo ni ulafi tu na ulevi wa madaraka! Shenzyie taip
 
Poleni Sana.Hawa Ma-Afande kwenye Corporate Management ni ZERO na nadhani ni wakati muafaka serikali kuwaondoa kote walikobaki kama walivyofanya Medical Stores Department(MSD) ambapo Mej.General Mhidze aliondolewa baada ya kuharibu shirika kwa Menejimenti Mbovu,kuendekeza Majungu,staff competent ambao wako critical kuhamishiwa nje ya Taasisi na kukaimisha hizo nafasi kwa vilaza wanaompigia magoti,Kuto-comply na sheria na miongozo mbalimbali na kutokuwa na focus yoyote.Kwa Maelezo yako mleta mada,Huyo Brigedia Kaimu Mkurugenzi Mkuu ni Mzigo kama aliyekuwa MSD na Takukuru ambao walisharudishwa jeshini wakafanya kazi zao za medani kuliko kupuyanga huku kwenye Corporates.
Natumaini Mamlaka husika ziko hapa zitafanya uchunguzi na kuchukua hatua sitahiki
 
Back
Top Bottom