Kushuka Thamani Shilingi: Sasa Benki zichunguzwe

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
Ukiacha sababu nyingi zinazotajwa kuchangia kushuka kwa thamani ya shilingi ya kitanzania; baadhi ya watu, akiwamo Zitto Kabwe walizungumzia ushiriki wa benki za kigeni, katika kushusha thamani shilingi yetu. Ni wakati muafaka wa hili kuchunguzwa, na pale penye kosa benki husika zilipe hasara.

Zitto Kabwe aliandika hivi kwenye blog yake:
Mabenki makubwa ya kigeni nchini, inasemekana, katika miezi ya karibuni yamefanya currency manipulations na kupelekea dola chache kukimbizwa na shilingi nyingi na hivyo bei ya dola kupanda bei. Hii inatokana na ukweli kwamba Benki zetu kubwa tatu zinazoongoza zinaendeshwa na wageni. Inasemekana biashara hii hufanyika kati ya matawi ya Benki za kigeni hapa nchini na makao makuu yao. Kuporomoka kwa shilingi kunakotokea hivi sasa hakuendani na kuporomoka kwa miaka ya nyuma kipindi kama hiki (ambacho ki kawaida ni miezi shilingi hushuka thamani kwa sababu ya watalii kuwa wachache na mauzo ya bidhaa nje kuwa madogo sana). Wastani wa miaka 10 iliyopita inaonyesha kuwa kipindi hiki shilingi hushuka kwa kati ya 8% mpaka 13% na sio kuporomoka kwa zaidi ya 20% kulikotokea hivi sasa. Kwa mfano mwaka 2011 miezi kama hii ( Februari ? Mei) Shilingi iliporomoka kutoka shs 1,380 kwa dola 1 mpaka shs 1,570 sawa na mporomoko wa 12%. Hata hivyo kuanzia mwaka huo mpaka mwaka 2014 shilingi imekuwa ikishuka thamani kwa kiwango kidogo sana. Mwaka 2013 thamani ya shilingi ilishuka kwa wastani wa asilimia 1.7 tu.

Uchambuzi huu wa thamani ya sarafu yetu unaonyesha kuwa kuna zaidi ya nguvu ya soko kunakotokana na mauzo yetu nje kuwa machache. Vile vile kupanda kwa thamani ya dola ya marekani duniani hakutoshi kuelezea mporomoko huu wa kasi wa shilingi kuanzia mwezi Disemba mwaka 2014 mpaka sasa. Tuhuma za mabenki kuwa yanahujumu shilingi (currency manipulations) zaweza kuwa na ukweli.
 
Back
Top Bottom