Kushindwa kusalimisha silaha kwa hiari Jela miaka 15 au Faini Milioni 10 au vyote kwa pamoja

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
58eff134-5006-4ec6-b61c-3eb2463af65b.jpeg
Jeshi la Polisi nchini linapenda kuwakumbusha wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuendelea kutumia vizuri msamaha uliotolewa na Serikali ambapo atakaye salimisha kwa hiari hatachukuliwa hatua yeyote wala kuulizwa maswali. Silaha hizo ni pamoja na zile za wamiliki waliofariki ambazo ndugu zao bado wanazo majumbani.

Msamaha wa kusalimisha silaha kwa hiari ulianza toka Septemba 1, 2023 na mwisho ni Oktoba 31, 2023. Hivyo hadi sasa zimebakia siku 27 za usalimishaji.

Aidha, wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wanaposalimisha kwa hiari, faida
yake ni kutokukamatwa na kufikishwa mahakamani, hivyo kumpa fursa ya
kuendelea na shughuli za kujitafutia maendeleo.

Endapo silaha hizo hazitasalimishwa katika muda wa msamaha uliotolewa na Serikali, operesheni ya nchi nzima itakapoanza wanaomiliki silaha hizo watakamatwa na kufikishwa mahakamani na wakipatikana na hatia kifungo chake ni miaka 15 jela au faini ya shilingi milioni 10 au vyote kwa pamoja.

Hasara nyingine mbali na kifungo ni kutengana na familia wakati wa kutumikia kifungo pamoja na kukosa fursa yakuendelea na shughuli za kujiletea maendeleo. Kumbuka Wakati wa kutumia fursa ya Msamaha ni sasa hadi Oktoba 31, 2023, Usichelewe.
 
Back
Top Bottom