Kusema Rais anashauriwa vibaya ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana akili; naona ni ukosoaji wa kinafiki

Kwema Wakuu!

Hakuna Jambo ambalo linanikera kama kumsikia MTU akisema Rais anashauriwa vibaya na washauri wake. Watu wengi wanaosema hivyo ni Watu wasioweza kueleza mambo bayana. Ni Watu wakupindisha pindisha maneno. Wasioweza
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Rais ndiye muamuzi wa mwisho, anapewa ushauri, lakini halazimiki kuukubali.

Pia, ana nyenzo na taasisi zote, zilizo rasmi na zisizo rasmi, kuhakiki ushauri wowote kabla ya kuukubali.

Kwa hiyo, akikubali ushauri mbaya, lawama ni zake.

Miaka ya 1970s Rais Nyerere alishauriwa na washauri wake rasmi wa uchumi kutaifisha maduka yote Tanzania. Mpaka maduka madogo kabisa ya mitaani.

Rais alikuwa anafikiri sana kuhusu suala hili, washauri wake rasmi walimshauri hivyo, lakini yeye alikuwa na shaka. Akamuita mzee mmoja wa Dar, Tabu Mangala. Huyo mzee hakuwa mchumi, hakuwa msomi, alikuwa ni mzee alwatan wa mjini tu (aliingia kwenye uongozi Yanga). Nyerere akamuuliza Tabu Mangala, akamwambia kuwa kashauriwa na washauri wake kutaifisha maduka yote, mzee Tabu Mangala anaona vipi suala hilo?

Mzee Tabu Mangala akamwambia Mwalimu Nyerere, chonde chonde baba, usifanye hivyo, utatuadhiri vibaya sana watu wa chini. Nyie taifisheni viwanda vikubwa, huku chini haya maduka ya mtaani tuachieni.

Nyerere akaacha ushauri wa washauri wake rasmi, wasomi wa uchumi, akachukua ushauri wa Tabu Mangala.

Habari hii inatufundisha nini?

Washauri hata wakiwa wasomi, wakati mwingine wanakosea.

Si lazima rais akubali ushauri wa washauri rasmi kila wakati.

Rais ana mkono mrefu unaoweza kupata ushauri kutoka sehemu mbalimbali zilizo rasmi na zisizo rasmi.

Hivyo, rais akipokea ushauri mbaya na kuufanyia kazi, of course washauri wana makosa, lakini wajibu wa mwisho ni wa rais, rais ana uwezo wa kupokea au kukataa ushauri wowote.

Rais Harry Truman wa Marekani alikuwa na kibao kwenye meza yake White House.

Kibao kile kiliandikwa "The Buck Stops Here".

Alisema kwamba kazi ya kuongoza nchi ina tatizo la watu kutupiana lawama sana, lakini, lawama zote zinaishia kwake, yeye ndiye anachukua lawama zote.
 
Hutaki Nyerere atajwe?
Tatizo we kinachokusumua ni udini. Nilikuaga nahisi utakua mtu wa maana hapa jukwaani kumbe debe tupu.

Kadri unavyozidi kufungua kinywa ndo unaonekana empty. Mleta mada hajampoint kiongozi yoyote kwa jina lake bali kaizungumzia taasisi ya Urais.

Mbona Taasisi ikifanya jambo zuri mnakimbilia kumpongeza kiongozi si mngekua mnawapongeza washauri?
 
Umeandika vyema kabisa.
Hicho ndicho nilikuwa nazungumzia. Ingawaje wengine wataingiza mambo yao
 
Nimeona kuwa, katika utamaduni wetu wa kuongea kwa tafsida, utamaduni wa mkubwa hakosei na baba hajambi, kauli ya "rais ana nia nzuri, lakini washauri wake ndio wanamuangusha" na nyingine kama hizo, aghalabu hutumika kitafsida na watu wanaotaka kusema rais kakosea, lakini wabaki wameitunza heshima ya rais.

Yumkini, rais kuwa na washauri wanaomshauri vibaya, washauri aliowateua yeye mwenyewe, ni kosa lake pia, kwa nini ana washauri wanaomshauri vibaya? Kwani hajui kuchagua washauri wazuri?

Katika utamaduni huu wa heshima zinazotuumiza, lazima kuwe na mtu anaitwa "fall guy". Fall guy ndiyo yule Msabaha alimwita bangusilo, scapegoat, mbuzi wa kutolewa kafara, mtu wa kubeba lawama ikiwa maamuzi yataonekana mabaya.

Utamaduni huu ni mbaya kwa sababu kadhaa.

Unamfanya rais kuwa kama Mungu mtu, asiyeweza kufanya makosa wala kuwajibika. Rais akijua hili, anaondoa umakini fulani. Anakuwa anajua kwamba, makosa yoyote atakayoyafanya, kutakuwa na mtu wa kubeba msalaba wake. Kutakuwa na mtu wa kuchukua lawama.

Utamaduni huu pia, kwa kujua ama kutokujua, unamdogosha rais. Yani hata kama lengo ni kumlinda rais asipate lawama, matokeo yake ni kumfanya rais kuwa kama zuzu anayeendeshwa kwa remote control na wasaidizi wake bila kujua mambo.

Utamaduni huu pia, unatuondoa kwenye uwazi na ukweli, tunakuwa watu wa kufanya mambo kwa hila, kuficha hoja kwenye tafsida, kusema kwa mzunguko. Hayo ni mambo ya kizamani. Kama rais kakosea, tuseme kakosea tu. Hata yeye mwenyewe tutakuwa tumemsaidia kujirekebisha huko mbele.
 
Ni utamaduni WA kinafiki.
Utamaduni wa kudhorotesha Maendeleo.
Utamaduni WA kitapeli, dhulma na uminyaji wa Haki.
Utamaduni wa kimungu MTU.

Ni utamaduni wa Watu wasiokubali ukweli. Utamaduni Mbaya Mno.

Ni moja ya sababu yanayoifanya Afrika isiendelee.

Utamaduni ambao Mzazi hawezi kuomba Msamaha watoto
 
Hilo mimi nimeshalisema siku nyingi sana.

Nimeshahoji kuwa kwani Rais yeye hana akili zake mwenyewe?

Rais hana discernment?

Rais haulizi maswali? Yote anayoshauriwa yeye anayakubali tu?

Kama tuna Rais wa hivyo basi huyo hafai kabisa.

Hatuhitaji kuwa na Rais zumbukuku asiye na akili.

Rais wa hivyo yupo mkuu. Sio kitendawili.
 
Kwema Wakuu!

Hakuna Jambo ambalo linanikera kama kumsikia MTU akisema Rais anashauriwa vibaya na washauri wake. Watu wengi wanaosema hivyo ni Watu wasioweza kueleza mambo bayana. Ni Watu wakupindisha pindisha maneno. Wasioweza kutamka nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.

Rais kama kakosea sema kakosea. Inatosha. Mambo ya kuanza kumtetea kuwa kashauriwa, sijui washauri wake ni wabaya ni kujaribu kumnasua na Matendo anayoyafanya. Ni kama unajaribu kueleza kuwa Rais Hakosei Jambo ambalo ni Uongo. Hakuna binadamu asiyekosea.

Kusema Rais anashauriwa vibaya kunatoa tafsiri na maana nyingi kama ifuatavyo;

1. Woga na unafiki.
Unashindwa kuongea moja Kwa moja kuwa hapa Rais kakosea. Yaani kiufupi unashindwa kuwa mkweli. Watu Wanafiki wanatabia ya kutaka kuongea lakini wakiongea hushindwa kusema Ukweli. Wanakuwa na kiherehere na uchawa au upambe. Huo ni unafiki.
Wakweli wananamna mbili ya kufanya, ni aidha aseme ukweli wote pasipo kufichaficha au kunyamaza Kabisa. Sio kutoa mambo nusunusu.

2. Inamaanisha Rais Hana Akili ya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi.
Rais sio Mtoto Mdogo, kusema Rais anashauriwa vibaya yaani anadanganywa ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana Akili.

Kwamba yeye akipewa ushauri anaufanya pasipo kufikiri. Kiufupi ni matusi kusema Rais anashauriwa vibaya.
Mbali na hivyo ni kujaribu kusema wapo Watu wanaomdharau Rais na kutokumheshimu(kutokumuogopa) ndio maana wanauwezo WA kumshauri vibaya(kumdanganya). Hiyo sio tuu kumtukana Rais Bali kutukana Taasisi nzima ya Urais.

3. Inamaanisha Rais NI Mbaya na muovu.
Yaani waje Watu wakushauri hapo twende tukaibe, au tupige dili alafu ukakubali alafu atokee mtu aseme umeshauriwa vibaya.

Kikawaida washauri hutoa ushauri kulingana na MTU alivyo. Ukiwa Mbaya utapewa ushauri Mbaya. Ukiwa mzuri ni ngumu sana washauri kukupa ushauri Mbaya Kwa sababu wanakujua fika. Tena Kwa nafasi ya Rais ni ngumu MTU akakushauri vibaya ilhali anajua wewe ni Mwema.

Haya unashauriwa vibaya alafu unatenda Ule ushauri Mbaya. Alafu wasingiziwe washauri. Huo ni Uongo.
Kikawaida mtu hujaribiwa Kwa tamaa, matamanio yake. Ubaya wa mtu upo ndani ya MTU na ndio unaojaribiwa. Ubaya siku zote hautoki nje kwenda ndani ya MTU. Bali unatoka ndani ya mtu kwenda nje.
Nazungumzia Kwa Watu wazima.

Uovu au uhalifu mara nyingi haunaga kisingizio. Kama ulivyo Wema nao hauna kisingizio.

Ukiona jitu ni jizi, fisadi, jambazi, Muuaji, mbakaji, na dhambi zingine jua Yale ayafanyayo yanatoka ndani yake na hakuna sababu ya nje inayoweza mfanya MTU kuwa Mtu Mbaya.

Ukiona MTU ni Malaya anafanya ukahaba ili ajipatie fedha, umaskini anaosema ndio Sababu, huo ni Uongo. Ila yeye ndani yake ndio Yuko hivyo.
Narurudia, ubaya wa mtu upo ndani yake na kamwe ubaya hautoki nje. Vinavyotokaje ni vichocheo tuu.

Hata hivyo, Mtu huweza kudanganywa na kupotoshwa kuhusu Jambo Fulani. Lakini mpotoshaji, na anayepotoshwa wote wanakuwa katika nafasi Sawa pale watendapo Kosa Hilo. Tena mtendaji anakuwa ndiye mkosaji Square.

Chagua Watu waadilifu, Wema na wapenda HAKI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kwahiyo wale washauri wake binafsi aliowateua hakujitambua.
 
Rais ndiye muamuzi wa mwisho, anapewa ushauri, lakini halazimiki kuukubali.

Pia, ana nyenzo na taasisi zote, zilizo rasmi na zisizo rasmi, kuhakiki ushauri wowote kabla ya kuukubali.

Kwa hiyo, akikubali ushauri mbaya, lawama ni zake.

Miaka ya 1970s Rais Nyerere alishauriwa na washauri wake rasmi wa uchumi kutaifisha maduka yote Tanzania. Mpaka maduka madogo kabisa ya mitaani.

Rais alikuwa anafikiri sana kuhusu suala hili, washauri wake rasmi walimshauri hivyo, lakini yeye alikuwa na shaka. Akamuita mzee mmoja wa Dar, Tabu Mangala. Huyo mzee hakuwa mchumi, hakuwa msomi, alikuwa ni mzee alwatan wa mjini tu (aliingia kwenye uongozi Yanga). Nyerere akamuuliza Tabu Mangala, akamwambia kuwa kashauriwa na washauri wake kutaifisha maduka yote, mzee Tabu Mangala anaona vipi suala hilo?

Mzee Tabu Mangala akamwambia Mwalimu Nyerere, chonde chonde baba, usifanye hivyo, utatuadhiri vibaya sana watu wa chini. Nyie taifisheni viwanda vikubwa, huku chini haya maduka ya mtaani tuachieni.

Nyerere akaacha ushauri wa washauri wake rasmi, wasomi wa uchumi, akachukua ushauri wa Tabu Mangala.

Habari hii inatufundisha nini?

Washauri hata wakiwa wasomi, wakati mwingine wanakosea.

Si lazima rais akubali ushauri wa washauri rasmi kila wakati.

Rais ana mkono mrefu unaoweza kupata ushauri kutoka sehemu mbalimbali zilizo rasmi na zisizo rasmi.

Hivyo, rais akipokea ushauri mbaya na kuufanyia kazi, of course washauri wana makosa, lakini wajibu wa mwisho ni wa rais, rais ana uwezo wa kupokea au kukataa ushauri wowote.

Rais Harry Truman wa Marekani alikuwa na kibao kwenye meza yake White House.

Kibao kile kiliandikwa "The Buck Stops Here".

Alisema kwamba kazi ya kuongoza nchi ina tatizo la watu kutupiana lawama sana, lakini, lawama zote zinaishia kwake, yeye ndiye anachukua lawama zote.
The Boss
Soma kipande cha Kiranga.
 
2. Inamaanisha Rais Hana Akili ya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi.
Rais sio Mtoto Mdogo, kusema Rais anashauriwa vibaya yaani anadanganywa ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana Akili.
... kimsingi hawajui iwe kikawaida au kwa makusudi kwanini Katiba ya nchi inataka rais awe at least 40yrs.

Sio tu ni mtu mzima kwa maana ya umri wa kisheria wa 18 ila has experience ya kutosha pamoja na kujua nini maana ya wanafiki na malicious motives zao kwenye uongozi wa nchi.

Kama rais akiendekeza machawa hakuna namna ya kumsaidia; abebe furushi lake mwenyewe badala ya kusingizia machawa ambao ana uwezo wa kuyaondosha akaweka wenye akili ya kulipeleka taifa mbele.

Nimekuelewa sana!
 
Kwema Wakuu!

Hakuna Jambo ambalo linanikera kama kumsikia MTU akisema Rais anashauriwa vibaya na washauri wake. Watu wengi wanaosema hivyo ni Watu wasioweza kueleza mambo bayana. Ni Watu wakupindisha pindisha maneno. Wasioweza kutamka nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.

Rais kama kakosea sema kakosea. Inatosha. Mambo ya kuanza kumtetea kuwa kashauriwa, sijui washauri wake ni wabaya ni kujaribu kumnasua na Matendo anayoyafanya. Ni kama unajaribu kueleza kuwa Rais Hakosei Jambo ambalo ni Uongo. Hakuna binadamu asiyekosea.

Kusema Rais anashauriwa vibaya kunatoa tafsiri na maana nyingi kama ifuatavyo;

1. Woga na unafiki.
Unashindwa kuongea moja Kwa moja kuwa hapa Rais kakosea. Yaani kiufupi unashindwa kuwa mkweli. Watu Wanafiki wanatabia ya kutaka kuongea lakini wakiongea hushindwa kusema Ukweli. Wanakuwa na kiherehere na uchawa au upambe. Huo ni unafiki.
Wakweli wananamna mbili ya kufanya, ni aidha aseme ukweli wote pasipo kufichaficha au kunyamaza Kabisa. Sio kutoa mambo nusunusu.

2. Inamaanisha Rais Hana Akili ya kujua kibaya ni kipi na kizuri ni kipi.
Rais sio Mtoto Mdogo, kusema Rais anashauriwa vibaya yaani anadanganywa ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana Akili.

Kwamba yeye akipewa ushauri anaufanya pasipo kufikiri. Kiufupi ni matusi kusema Rais anashauriwa vibaya.
Mbali na hivyo ni kujaribu kusema wapo Watu wanaomdharau Rais na kutokumheshimu(kutokumuogopa) ndio maana wanauwezo WA kumshauri vibaya(kumdanganya). Hiyo sio tuu kumtukana Rais Bali kutukana Taasisi nzima ya Urais.

3. Inamaanisha Rais NI Mbaya na muovu.
Yaani waje Watu wakushauri hapo twende tukaibe, au tupige dili alafu ukakubali alafu atokee mtu aseme umeshauriwa vibaya.

Kikawaida washauri hutoa ushauri kulingana na MTU alivyo. Ukiwa Mbaya utapewa ushauri Mbaya. Ukiwa mzuri ni ngumu sana washauri kukupa ushauri Mbaya Kwa sababu wanakujua fika. Tena Kwa nafasi ya Rais ni ngumu MTU akakushauri vibaya ilhali anajua wewe ni Mwema.

Haya unashauriwa vibaya alafu unatenda Ule ushauri Mbaya. Alafu wasingiziwe washauri. Huo ni Uongo.
Kikawaida mtu hujaribiwa Kwa tamaa, matamanio yake. Ubaya wa mtu upo ndani ya MTU na ndio unaojaribiwa. Ubaya siku zote hautoki nje kwenda ndani ya MTU. Bali unatoka ndani ya mtu kwenda nje.
Nazungumzia Kwa Watu wazima.

Uovu au uhalifu mara nyingi haunaga kisingizio. Kama ulivyo Wema nao hauna kisingizio.

Ukiona jitu ni jizi, fisadi, jambazi, Muuaji, mbakaji, na dhambi zingine jua Yale ayafanyayo yanatoka ndani yake na hakuna sababu ya nje inayoweza mfanya MTU kuwa Mtu Mbaya.

Ukiona MTU ni Malaya anafanya ukahaba ili ajipatie fedha, umaskini anaosema ndio Sababu, huo ni Uongo. Ila yeye ndani yake ndio Yuko hivyo.
Narurudia, ubaya wa mtu upo ndani yake na kamwe ubaya hautoki nje. Vinavyotokaje ni vichocheo tuu.

Hata hivyo, Mtu huweza kudanganywa na kupotoshwa kuhusu Jambo Fulani. Lakini mpotoshaji, na anayepotoshwa wote wanakuwa katika nafasi Sawa pale watendapo Kosa Hilo. Tena mtendaji anakuwa ndiye mkosaji Square.

Chagua Watu waadilifu, Wema na wapenda HAKI.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kulialia ni jadi ya mtanzania, huwa siku zote anatazama upande mbaya tu. Huko mtaani frames zimeanza kupangishwa.

Yale majengo makubwa yaliyokuwa yakigeuka magofu siku baada ya siku hivi sasa mafundi wanaonekana wakiyamalizia, maana yake watu wamepata pesa baada ya mzunguko kuwa mzuri.

SSH analaumiwa kuwapendelea matajiri lakini hao maskini wanaendelea kuzungukwa na umaskini iwapo matajiri wanakwenda kukwama kiuchumi.

Trickle down effect haikwepeki kwenye uchumi haswa huu wa kwetu.
 
*Rais Hichilema kasha wahi sema kusema kwamba "kiongozi ana shauri vibaya ni uongo kwa sababu hao viongozi wanao mshauri humuhakisi(reflection) huyo kiongozi mwenyewe" hivyo naweza sema kwamba ni mjinga pekee ndio huwa na imani ya hiyo ya rais kushauri vibaya.

Pia Mwalimu Nyerere alisha wahi sema "mtu akikupa ushauri wa kipumbavu nawe ukajua niwa kipumbavu na ukaufanyia Kazi ushauri huo basi ana kudharau"

Ni ngumu sana kuupata ukweli kama ulivyo hasa toka kwa wanasiasa bali kwa wanasiasa Kuna ukweli kama unavyo jitokeza.*
 
Tatizo we kinachokusumua ni udini. Nilikuaga nahisi utakua mtu wa maana hapa jukwaani kumbe debe tupu.

Kadri unavyozidi kufungua kinywa ndo unaonekana empty. Mleta mada hajampoint kiongozi yoyote kwa jina lake bali kaizungumzia taasisi ya Urais.

Mbona Taasisi ikifanya jambo zuri mnakimbilia kumpongeza kiongozi si mngekua mnawapongeza washauri?

So nikisema chochote kuhusu Nyerere inakuwa tumetaja dini?

Mleta mada hajataja jina kwani haijulikani sasa hivi Rais ni nani?
Au asipotaja basi ndo tujifanye hatujui Rais wa sasa ni nani?..
Huwezi jadili lolote sasa kuhusu Taasisi ya Urais bila kumgusa Rais wa sasa...
Na kama tukitoa mifano ya Nyerere ndo inatufanya tuwe wenye "udini"..basi be free hukumu Kwa kadri ya upeo wako unavyo kuruhusu
 
Hilo mimi nimeshalisema siku nyingi sana.

Nimeshahoji kuwa kwani Rais yeye hana akili zake mwenyewe?

Rais hana discernment?

Rais haulizi maswali? Yote anayoshauriwa yeye anayakubali tu?

Kama tuna Rais wa hivyo basi huyo hafai kabisa.

Hatuhitaji kuwa na Rais zumbukuku asiye na akili.
Risi mwenyewe ni mnafik tu alisema akina kabudi wapo ilkulu kwa ajili ya kurekebisha mikataba lakin aakaWaacha hapo akaenda dubai kuanguka sain kinyemela ,sasa anawapa ccm wakati mgumu wa kujitetea
 
Back
Top Bottom