Kupunguza umasikini nchini kila familia ipeleke kijana mmoja ughaibuni akapambane huko

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,101
36,063
Kama hujasafiri utasema Tanzajia ina maisha mazuri.ndio.ina maisha bora kwa kulinganisha na nchi zilizotuzunguka ila ukienda duniani huko sisi hatuishi bali tunadumu.

Ili kuboresha uchumi wa familia nivema serikali ikalegeza masharri ya passport vijana wakatafute maisha huko ughaibuni.

Kila familia ikiwana kijana katika nchi zilizoendelea mwisho wa mwezi vijana hutuma reminttences nyumbani mambo huwa safi,somalia,kenya na wrst africa countries wanafanya hivyo.

Kwa Tanzania bara ni Tanga pekee yenye diaspora wengi pamoja na zanzibar ndio maana utakuta hizo sehemu watu husema ni wavivu lakini wanaishi standard life kuliko mikoa wanayoshinda mashambani.

Serikali haina ajira za kutosha kwa vijana wetu,huko kwa wenzetu unskilled labor ni nyingi na zinatafuta Vijana,pili vijana wakienda nje wanapata exposure na ujuzi fulani wakirudi nchini,mwisho serikali nayo inafaidika kupitia kodi inayotumwa kama remittence,mfano kundi la ramadhan brother baada yakushinda serikaliimekata income taxi yake bila kutoa jasho.

NB.huwezi kuelewa uzi huu mpaka uwe umesafiri au ujue kuwa serikali inafanya makusudi vijana wasisafiri nje wasije kuamka usingizini wakawatoa madarakani,ukiishi ulaya utawachukia tu watawala wetu kwa nin hawajali maisha ya raia wao,labda na wewe uwe sehemu ya system.
 
Fafanua hapo kwa Tanga na Zanzibar kua na diaspora wengi unamaanisha Hao ndio wanapewa kipaumbele sana kwenye Visa au unamaanisha nini?
Hizo sehemu tajwa vijana wameanza kwenda ughaibuni kitambo sana,iwe kwa kuuza unga,kuzamia au kihalali au ndugu zao waliokimbia madhila ya Mapinduzi ya Zanzibar na machafuko ya kisiasa Zanzibar pia intetmarriage ya mikoa hiyo na waarabu imechangia pakubwa, huwezi kwenda Ulaya, Arabuni au Amerika ukakosa vijana wa hayo maeneo na wanasaidia sana familia zai
 
Ukimleta pep guardiola afundishe stars atafeli tu,ila ukileta vijana wengi wanaocheza ligi kuu kubwa duniani hata mgunda anaweza kuwatrain wakachukua kombe la africa

Pep atawabadili kina samatta kuchezac navyopaswa. Obama akiazimwa hawezi kuwa na issue uchwara kama za magoli ya mama, demokrasia itashamiri, nk .. tutapiga hatua kwenye mambo ya msingi.
 
Ndo nataka niende State nikaanze hata kuendesha ma truck nilipiga hesabu kama za matikiti nikagundua nikifanya hiyo kazi naweza kutengeneza dollar 1,900/= kwa wiki, napiga kazi nonstop uhakika wa kutengeneza Tsh million 20 kwa mwezi upo.
 
Hizo sehemu tajwa vijana wameanza kwenda ughaibuni kitambo sana,iwe kwa kuuza unga,kuzamia au kihalali au ndugu zao waliokimbia madhila ya mapinduzi ya zanzibar na machafuko ya kisiasa zanzibar pia intetmarriage ya mikoa hiyo na waarabu imechangia pakubwa,huwezi kwenda ulaya ,arabuni au amerika ukakosa vijana wa hayo maeneo,na wanasaidia sana familia zai
Zanzibar Visa hawasumbui hata kidogo shida huko Bara Visa ni mtifuano process kibao mizungusho kibao wanazuia vijana wasiende nje maana wakaenda hawarudi sasa Nchi itajengwa na nani km wote wakakimbia nje, hata Nyerere alisema hilo kwenye hotuba zake kwamba kijana akienda nje akaona Maisha ya kule nje yalivyo akilinganisha na hapa anaona Bora abakie kule kule tu
 
Mkuu sijakurupuka ,serikali haiwezi kuinua famiia yako bali mtajiinua wenyewe,angakia hata mtaani kwenu familia zenye vijana nje ziko vizuri kiuchumi,
Sijasema umekurupuka mkuu!

Ila familia mpaka inakuwa na uwezo wa kupeleka kijana nje, let say America, Europe etc, hiyo familia tayari inajiweza, kilichobaki ni kujazia jazia tu!

Hapa hapa Tanzania tu kuna familia mikoani hazina uwezo wa kusafirisha kijana kutoka mkoani kumleta mjini, itakuwa nje ya nchi?
 
Back
Top Bottom