Kupotea kwa Ben Saanane: Hoja za wananchi, kinachoendelea na maoni ya Waziri Mwigulu

Mkuu Mwugulu mimi nikiri tuu kwamba viongozi wengi mnafanya kazi chini ya ufanisi. Swala la Ben chukulia limefikisha mwezi sasa, hamkuonesha kulijali hill awali mpaka wananchi tupige kelele sana ndio mmejigusa sasa.
Mimi sioni ubaya wa technically kwa kuwa ndio njia mnayopenda msemwe nayo, wizara nzima ndio mtoke usingizini. Na nakuhakikishia usingetoka hapa pengine hizo tuhuma ungezibeba kwa mikono miwili.
Swali Ni kwanini wizara yako haiko active kutuupdate, juu ya maswala ya msingi kama hayo kuchukulika vina saba vya miili hio?. Je huu uzembe unatuahidi nini ukiwa kama waziri mwenye dhamana kwenyw wizara husika?
Je kulikuwa na ugumu gani kwa serikali kusikia kelele za familia husika toka mwanzo, kwa kupotelewa Ben vp unahisi hili halileti mgawanyiko katika jamiii kwa kuna labda hapewi kipaumbele sababu ni mpinzani?.
 
Sijaridhishwa na ufafanuzi wako kuhusu Lwakatare , lakini nina hoja kuhusu Ben , hivi kama wewe ni Waziri mwenye dhamana ya Usalama wa raia na mali zao kwanini usijiuzulu baada ya kushindwa kumpata Ben , ili upishe wengine wenye weledi kukushinda , ambaye unaonekana unafaa zaidi kwenye fitina za chama cha Mapinduzi kuliko uongozi wa serikali ?
Jaribu kuwa mkomavu kifikra! ...yaan Waziri ajiuzulu kwa kupotea mtu! ...mbona kila leo ITV wanatangaza waliopotea sasa kama huo ndo mwendo si kila siku kungekuwa na kujihudhuru!
 
Mkuu Mwugulu mimi nikiri tuu kwamba viongozi wengi mnafanya kazi chini ya ufanisi. Swala la Ben chukulia limefikisha mwezi sasa, hamkuonesha kulijali hill awali mpaka wananchi tupige kelele sana ndio mmejigusa sasa.
Mimi sioni ubaya wa technically kwa kuwa ndio njia mnayopenda msemwe nayo, wizara nzima ndio mtoke usingizini. Na nakuhakikishia usingetoka hapa pengine hizo tuhuma ungezibeba kwa mikono miwili.
Swali Ni kwanini wizara yako haiko active kutuupdate, juu ya maswala ya msingi kama hayo kuchukulika vina saba vya miili hio?. Je huu uzembe unatuahidi nini ukiwa kama waziri mwenye dhamana kwenyw wizara husika?
Je kulikuwa na ugumu gani kwa serikali kusikia kelele za familia husika toka mwanzo, kwa kupotelewa Ben vp unahisi hili halileti mgawanyiko katika jamiii kwa kuna labda hapewi kipaumbele sababu ni mpinzani?.
"Hawakuonesha??
Kvp?

~Cmb
 
Mh. Waziri umeandika kwa uchungu sana, nakupa pole
kwa sababu hawa ndiyo vijana
tulionao leo kwenye hili jukwaa.

Bahati mbaya sana vijana wengi humu
wanatumia vichwa vyao kufugia
nywele, hatumii vichwa vyao kwenye kufikiri, hili ni kosa.

Binafsi
nimefarijika sana kusoma utetezi
wako hapa, Mungu akubariki!

Unafki huo, kwanini asiulizwe ww km unasifia sifia acha wenzio wamhoj na kumponda
 
Mhe. Mwigulu, tatizo letu sisi tunaendeshwa na kitu kiitwacho DHANA, inayoendeshwa ushabiki UCHWARA! Hatufanyi UHAKIKI Wa jambo kabla ya KUKURUPUKA kusema ya UWONGO na kulazimisha jamii iamini kuwa ni UKWELI. Basi WAPOTEZEE!!
Na Mwigulu alikua na dhana kuwa Lwakatare ni GAIDI,labda umesahau hilo,
 
Faru john anabamba kuliko Ben SAA nane .tumezoea sasa ikionekana kunatukio ambalo mnaona mtachafuka nyie viongozi na likaonekana linasambaa kwa kasi kubwa mnaibua jingine ili la kwanza lipoteee.MF.miili saba ya watu na Ben sanane.naona kinaibuka kwa mbele faru john duh.nimtazamo wangu tu jamani
 
Mbona siasa sio uadui? Kusema nilimsaidia? Mbona hata niliogombea nao 2010 wa oposition niliwapa mafuta ili kampen ziendelee! Shida wengine mnadhan kwenye siasa hatuongei
Imekuwa ni bahati kweli, kwamba wahanga wote hapo wametokea kuwa marafiki wa Mh. Mwigulu Nchemba.

Mimi hili la Mh. Lwakatare ni la siku nyingi, lakini bado nina mashaka nalo. Kama kumbukumbu zangu ni sahihi, suala hilo lilimgusa sana Mh. Mwigulu, hadi pale bungeni!

Rejea baadhi links hapa chini:-

Sakata la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Rwezaula kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, limeibua mvutano mkali bungeni huku wabunge wakishambuliana kwa maneno makali. | PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''

Na

Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare | MATUKIO NA VIJANA

Sasa leo, Mh Lwakatare ni rafiki yake, sipati picha!
 
Kuna tatizo kubwa la mawasiliano kati ya nyinyi viongozi na wananchi,huwa hamtoi mirejesho inayojitosheleza mpaka mambo yanakuwa mazito
 
Imekuwa ni bahati kweli, kwamba wahanga wote hapo wametokea kuwa marafiki wa Mh. Mwigulu Nchemba.

Mimi hili la Mh. Lwakatare ni la siku nyingi, lakini bado nina mashaka nalo. Kama kumbukumbu zangu ni sahihi, suala hilo lilimgusa sana Mh. Mwigulu, hadi pale bungeni!

Rejea baadhi links hapa chini:-

Sakata la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Rwezaula kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, limeibua mvutano mkali bungeni huku wabunge wakishambuliana kwa maneno makali. | PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''

Na

Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare | MATUKIO NA VIJANA

Sasa leo, Mh Lwakatare ni rafiki yake, sipati picha!
Nipo hapa nasoma comments za wachangiaji sio utetez mfu wa Mwigulu Nchemba.
Kuhusu ugaidi wa Lwakatare dunia ilimskia na hakuwah kukanusha,watu wengine sijui kwenye nyumba za ibada huwa wanaenda kufanya nini?kumtuhumu mtu ni gaidi na unasema ushahidi unao na huutoi ni udhalilishaji mkubwa sana,sasa naanzaje kumsikiliza anachokisema huyo mtu.
 
Mwigulu Nchemba
Hivi yale mabomu ya Soweto wewe si ulihusika kwa 100%?

Vipi kuhusu ule ushahidi wako wa duniani hata mbinguni uliomsingizia Lwakatare, hebu tuwekee hapa duniani JF japo kidogo.

Kijana mwenye roho katili na ya kinyama hapa duniani mmojawapo unayejiona hii T z ni mali uliyoachiwa urithi na baba yako.

Hebu tueleze kijana
 
Hata siku moja pumba haziwezi kuwa mchele...!!!kuna mwenye dunia yeye ndio anajua nini kinaendelea kwenye dunia yake
 
Ndugu Nchemba nilikuuliza jana na leo nakuuliza Tena,

1) Je unahusika na Kupotea kwa Ben Saanane?
2) Je ujumbe wa Kitisho ailioupata kabla ya Kutoweka ulitoka kwako?
3) Kwa hatua ya Kushangaza umefanya juhudi kubwa kueleza Kuwa Ben Saanane alikuwa Rafiki yako, Je kwanini unafanya hivyo sasa?
4) Kama Ni rafiki yako hivyo na Kwa bahati nzuri wewe Ni waziri wa Mambo ya Ndani, Ni mara ngapi umepiga simu kwa familia kuwahakikishia kuwa unahangaika kusaidia kumtafuta rafiki yako?
5) Je binafsi umeshampigia Mzazi wake simu, wakati wanahangaika kumtafuta Ben, uone kama walihitaji msaada wowote kwako kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Rafiki wa Karibu.
6) Je unahusika na Kutoweka kwa Ben? Yes or No
7) Je umeshahusika na Kudhuru au Kuua au kuagiza mtu yeyote auawe kwa Faida za Kisiasa au chama chako? Yes or No!
8) Na labda nikuulize je hivi wale polisi wanne waliouawa bank na watu, uliosema wenye pikipiki, Unadhani walikuwa ni Majambazi?
9) Je umeshajisikia amashaka moyoni kuhusu vifo vile?, kama ndio Kwanini na Kama hapana Kwaninj?
10) Na hivi ile siku ya Vifo vya wale Polisi? Taarifa ulipewa na nani muda gani, na ulikuwa wapi muda huo, Je nini Kilikusukuma Kuvaa Magwanda ya Kipolisi usiku ule? What you wanted to achieve wearing the costumes?
 
WanaJF,

Nimeamua (kama member wa JF) kuandika kwa masikitiko makubwa sana kufuatia uzi wa technically:

Mwigulu Nchemba ndiye suspect namba moja kupotea kwa Ben Saanane?

Vijana wenzangu, tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuaondika mambo makubwa yasiyo na utani bila kujiridhisha na tunachokiandika. Sio kitu kizuri kuandika jambo kubwa hivi kwa taarifa za kuungaunga na ufahamu wa kuungaunga.

1) Moja anasema watu wamezikwa bila kutambuliwa: Ni kweli watu hao miili ilishaharibika na hatua iliyokuwa inasitahili ilikuwa kuzikwa. Hata hivyo tumechukua sampuli kwa kila mwili nawe ukitaka kuitambua unaruhusiwa. Mpaka sasa haijulikani sana uhakika kuwa hao ni nani, lakini sisi tulisema kuna uhusiano mkubwa wa watu hao na wahamiaji haramu ambao waliokotwa 81 wakiwa mahututi eneo hilohilo na wiki hiyo hiyo.

Hatujasema kuwa ni kwa asilimia 100 ni wahamiaji haramu, tunasema huenda wakawa ni wao maana kama hao 81walikuwa hoi wiki hiyo hiyo huenda kati yao kukawa na baadhi yao ambao walishapoteza maisha na tukasema tuendelee na kutafuta undani zaidi, lakini wewe unasema tumezika bila kutambuliwa, hivi ni nani angewatambua? This is not fair.

Wapo wakadiriki hata kusema watu hao waliuwawa na Polisi, la hasha hata wakiwa wahamiaji haramu hawaruhusi kuuawa ndio maana Polisi ilipowaokota wale mahututi wakiwa hwawezi kuongea wala kusema iliwapikia uji na wengine kuwapeleka hosipitali.

Tunaongelea miili iliyookotwa, kumekuwa na kawaida ya wasafirisha watu kutupa miili hovyo, sishangai huenda hata wakawa walikuwa zaidi ya 81 wameokotwa saba, huenda wengine wakawa wamepelekwa baharini, ndio maana tunaendelea kutafuta undani.

2) Pili unasema kifo cha Mbagala kahusika Mwigulu, Eti alifika wa kwanza.

Si kweli, sikufika wa Kwanza. Angalia, kwanza tukio lilifanyika saa moja kwenda saa mbili hivi, akaenda OCD saa moja hivi, saa tatu akaenda RPC, saa nne akaenda Siro na IGP. Mimi nilienda Saa sita usiku na nimemkuta RPC na Kamanda Siro na video zipo. Niliwakuta na ndio walikuwa wananielekeza tukio lilipo. Unasema niliwatangulia polisi? Jitafakari. Yaani yote hayo ni kutaka kuhalalisha fikra potofu na kuchafua taswira ya mtu, kwanini unaandika kwa uhakika wakati ni vitu vya kusikia?

3) Tatu unasema swala la Lwakatare. Kwa sasa Lwakatare ni mbunge na ni rafiki yangu na anajua ukweli wa yote yale yaliotokea na tunaongea mara kwa mara. Nitakupa namba yangu, hebu tafuta siku tukakae na Lwakatare mimi nawe akisema nilimsingizia nitaacha ubunge na uwaziri.

Jana tu, tar 20/12/2016 ilikuwa kesi hiyo hiyo wewe unasema kesi ilienda mpaka ikaisha! Uwe unapata ukweli kabla ya kuandika. Jambo hili halijaisha jana ilikuwa kesi, lakini Lwakatare anajua hili jambo, tunaongea mara kwa mara nadhani ungeacha tu jambo hili liishe liliko kwenye mkono wa sheria, usilichokonoe hata Lwaka hangependa ulichokonoe kama unavyofanya kwani yeye anajua ukweli, namba yangu ni 0714008888

4) Unasema nilisema nitatoa ushahidi wa mauaji ya SOWETO. Ndugu, kapitie upya kumbukumbu zako. Nenda kaongee na Lema hata sasa kulekule alipo, muulizie maana naye mwanzo alikuwa na mtazamo kama wa kwako.

Ushauri wangu: Kuandika hapa jamvini suala serious kama hili ni vyema ukafanya fact finding kidogo

Sasa kuhusu suala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu
Ningekomenti kitu..ila kwa leo bado nna hasira sana ila basi tu Mungu anajua na malipo ni hapa hapa Duniani.!
Time will tell.
 
1.jpg
!!!!!!!
 
Back
Top Bottom