Kupotea kwa Ben Saanane: Hoja za wananchi, kinachoendelea na maoni ya Waziri Mwigulu

Mh. Safi kwa kutujibu umeonesha uthubutu. Mwenyekiti wa chama hajasema chochote. Wala hana muda. Waziri umekuwa active sana kwa kujibu hoja zote za wizara yako na hii ni nzuri.
Bado nahoji kwanini mwenyekiti wa chama amekuwa kimya mpaka Leo. Ni either anajua au hajali watu wake.
 
mi nikupongeze kwa maelezo, ingawa yana uwalakini, sasa kwa nini unachelewa kujibu baadhi ya hoja za humu? na unapelekea baadhi yetu kuaminishwa?

yote kwa yote, big up
 
Huu nao ni ujasiri mkubwa mkuu kutoka na kufafanua hili suala hadharani. Umeonyesha mfano na waheshimiwa wengine wafuate.
Kwa nafasi yako saidia kupatikana kwa our brother Ben Saanane
 
Mwigulu Nchemba
Umeandika kwa ustadi uliojaa ukakasi kwa watu ambao watasoma na kutafakari.

Waziri kutoa taarifa tena za maisha ya watu waliozikwa ambazo hazina uhakika tena zenye hitimisho, ni kosa kubwa.
Yaani mnafuatilia baada ya watu kupiga kelele kutaka kujua zaidi.

Ni bora taarifa hizo zingetolewa na mkuu wa mkoa wa eneo hilo au RPC.

Pili suala la Ben bado hueleweki.
Ulipaswa mseme mlifikia wapi katika kumtafuta kama vyombo vya ulinzi na sio wewe binafsi kutueleze mara ya mwisho kuwasiliana nae.

Njoo na habari za kiofisi kuhusu Ben mmefikia wapi katika uchunguzi wa kumsaka alipo, na sio taarifa zako binafsi wewe na Ben.
sasa akisema wamefikia wapi si upelelezi utakuwa umevuja mda mwingine msijitoe ufahamu.
 
Awali ya yote nikupe pongez kwa kuwa jasir kujitokeza ktk h mada nyeti ambayo watanzania weng walikuwa gizan hasa wanaopitia mitandaon hasa hapa jf,pili napenda kuchukua nafasi adhm ya kukuktana na kiongoz wa juu serikaln ambapo ktk maisha yange nisinge kutana na m2 kama we2 ukiwa mwanajamii wa jf kwan n adim sana kwa viongoz wa vyama hasa ccm kuja humu na kujipambambanua kama we2! Lkn pia nikuombe ndg Nchemba kuwa usimuattack ndg technically kwa uzi wake wa kukususpect bila ya hvyo nanavyowafaham watawal na c viongoz wa nch msingeonekana/usingeonekana hapa,kuna mwl wangu aliniambia kuwa ukitaka kujua hasira za m2 mtuhumu,hvyo kupitia maneno yake umejitokeza kwa wadhfa wako umejitokeza.Ndg Nchemba we2 n kijana mwenzetu regardless 2natofautiana itikad na mitizamo lkn pia uelewa,ukiwa kijana tena msomi mzr kadr watu wanavyokusifia ingawa sikufaham zaid ya kukuona kwena magazeti na tv kwa nadra sana huku kijjn ingawa siamin sana kama u msom wa vyet au kuelimika na kuheshm dignity ya binadamu,kwa uelewa wangu,pt
 
..watu huwa wanabadilika...nawe Mwigulu waweza kufanya hivyo pia....lakini tutakuamini tu endapo utapambana hadi Ben apatikane.....kwa maana serikali mna mkono mrefu na Ben mngetaka angeshapatikana siku nyingi kelele zimekua zinapigwa....Mwigulu utaaminika kwa wengi kama maneno yako haya yataendana na vitendo...jambo ambalo historia yako inapingana nalo....just a matter of time....
 
Amepotea Ben katika mazingira ya kutatanisha hakuna taarifa yoyote kutoka ndani ya serikali,Leo umeguswa wewe kwa masaa machache umeshatoa ufafanuzi.Najiuliza umeamua kujitetea kwa kutetea cheo chako au? Kama ndivyo basi wewe siyo rafiki wa kweli wa Ben kama ambavyo umeeleza ktk post yako.
 
Binafsi nikupongeze kwa kuwa mmoja wa wanafamilia ya JF, pia ahsante kwa ufafanuzi, maana huku mtaani kwetu yanasemwa mengi kuhusu "SIRI.KALI"
 
Mh waziri binafsi nakushukuru kwa kuja hapa kutoa ufafanuzi wa mambo haya, hasa hili la mwanaharakati, kijana mwenzetu, rafiki yetu, mfanyakazi wa chadema na mwanafunzi wa PHD ndugu yetu Ben Saanane. binafsi mh. waziri katika maelezo yako naona mambo wawili.
1.Kama Mwigulu:binafsi kama raia yeyote anaewezakuguswa na uhai wa raia mwenzie nakubaliana na wewe kabisa, umeongea mengi ya kuonyesha kuguswa kama sisi tulivyoguswa, mbali zaidi umeenda mbali kuonyesha kabisa kua umeguswa kuliko hata sisi kwa vile Ben ni rafiki yako na mlikuwa karibu zaaidi kuliko hata baadhi yetu ambao hatujawahi hata kumuona zaidi ya kwenye vyombo vya habari na mitandaoni, katika hili nakubaliana na wewe ndg Mwingulu.
2.Kama waziri: Kama waziri sijakubaliana na wewe katika maelezo yako mh, hapa napata maswali mengi zaidi ya majibu, hapa huwezi kujivua lawama mh na ingekua nchi zilizoendelea kama maziri mwenye dhamana ilibidi ujiuzulu, kujiuzulu si kwamba unahusika moja kwa moja ila ni kwa sababu kama waziri mwenye dhamana mtu kapotea zaidi ya mwezi mmoja na mpaka leo wizara yako haina majibu. lawama huwezi kumuelekezea yeyote hapa zaidi ya wewe mwenyewe, mpaka sasa polisi\wewe mwenyewe mtu kapotea zaidi ya mwezi hamjawahi kujitokeza hadharani kuwaeleza watz upelelezi umefikia wapi, mara ya mwisho aliongea na nani? waliongea nini?akiwa wapi?saa ngapi? suspects ni kina nani? haiwezekani kama serikali mpaka leo msiwe na suspect hata mmoja!
Hitimisho:kama nilivosema mwanzo maswali ni mengi, ila nichoona yawezekana kbs mnaoogopa kwenda kwenye media kwa sababu mnaogopa kutumbuliwa, inaonekana inakuuma ila kuna kitu unajua, yawezekana ulijaribu kufuatilia ukagonga kisiki kwa maagizo kutoka ngazi za juu. INAUMA SANA. pls msifute comment yangu
 
Ni jambo jema kutenga muda na kutoa ufafanuzi juu ya hoja kadhaa zitolewazo na wadau. Kwahilo nakupongeza sana maana nadhani ndiye kiongozi pekee anayefanya hivyo. Najua unaijua JF vizuri sana na nafasi yake katika katika kutoa habari kwa wananchi. Nakusihi uendelee kutoa ufafanuzi na kuwa active member kila inavowezekana maana kunawengine hawaonekani tena huku licha ya kuwa ni members.
Usisahau wizara yake ndio iko mstari wa mbele kuisakama jamii forum. Leo angepata wapi jukwaa la kufafanua hayo. Acha watu waongee na serikali itoe majibu
 
Sijaridhishwa na ufafanuzi wako kuhusu Lwakatare , lakini nina hoja kuhusu Ben , hivi kama wewe ni Waziri mwenye dhamana ya Usalama wa raia na mali zao kwanini usijiuzulu baada ya kushindwa kumpata Ben , ili upishe wengine wenye weledi kukushinda , ambaye unaonekana unafaa zaidi kwenye fitina za chama cha Mapinduzi kuliko uongozi wa serikali ?

Viongozi wa Afrika hawana msamiati unaoitwa "jiuzulu"
 
Labda unaweza kuwa suspect namba moja kwa sababu ni jukumu lako kuwaeleza wananchi what Is real going on,kama minister of police umeshindwa kuja na jibu LA kutosheleza basi ujue something wrong somewhere
Napenda nichukue nafasi hii kukueleza this nation belong to all of us,na kama nchi ni Mali yetu tuna haki ya kuhoji,kuuliza,kutoa maoni,kuwa na hasira nakadhalika
What is about to happen in our country you real going to pay for it!!!!!!
Jibu la uhakika atalitoa baada ya uchunguz kukamilika.
 
WanaJF,

Nimeamua (kama member wa JF) kuandika kwa masikitiko makubwa sana kufuatia uzi wa technically:

Mwigulu Nchemba ndiye suspect namba moja kupotea kwa Ben Saanane?

Vijana wenzangu, tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuaondika mambo makubwa yasiyo na utani bila kujiridhisha na tunachokiandika. Sio kitu kizuri kuandika jambo kubwa hivi kwa taarifa za kuungaunga na ufahamu wa kuungaunga.

1) Moja anasema watu wamezikwa bila kutambuliwa: Ni kweli watu hao miili ilishaharibika na hatua iliyokuwa inasitahili ilikuwa kuzikwa. Hata hivyo tumechukua sampuli kwa kila mwili nawe ukitaka kuitambua unaruhusiwa. Mpaka sasa haijulikani sana uhakika kuwa hao ni nani, lakini sisi tulisema kuna uhusiano mkubwa wa watu hao na wahamiaji haramu ambao waliokotwa 81 wakiwa mahututi eneo hilohilo na wiki hiyo hiyo.

Hatujasema kuwa ni kwa asilimia 100 ni wahamiaji haramu, tunasema huenda wakawa ni wao maana kama hao 81walikuwa hoi wiki hiyo hiyo huenda kati yao kukawa na baadhi yao ambao walishapoteza maisha na tukasema tuendelee na kutafuta undani zaidi, lakini wewe unasema tumezika bila kutambuliwa, hivi ni nani angewatambua? This is not fair.

Wapo wakadiriki hata kusema watu hao waliuwawa na Polisi, la hasha hata wakiwa wahamiaji haramu hawaruhusi kuuawa ndio maana Polisi ilipowaokota wale mahututi wakiwa hwawezi kuongea wala kusema iliwapikia uji na wengine kuwapeleka hosipitali.

Tunaongelea miili iliyookotwa, kumekuwa na kawaida ya wasafirisha watu kutupa miili hovyo, sishangai huenda hata wakawa walikuwa zaidi ya 81 wameokotwa saba, huenda wengine wakawa wamepelekwa baharini, ndio maana tunaendelea kutafuta undani.

2) Pili unasema kifo cha Mbagala kahusika Mwigulu, Eti alifika wa kwanza.

Si kweli, sikufika wa Kwanza. Angalia, kwanza tukio lilifanyika saa moja kwenda saa mbili hivi, akaenda OCD saa moja hivi, saa tatu akaenda RPC, saa nne akaenda Siro na IGP. Mimi nilienda Saa sita usiku na nimemkuta RPC na Kamanda Siro na video zipo. Niliwakuta na ndio walikuwa wananielekeza tukio lilipo. Unasema niliwatangulia polisi? Jitafakari. Yaani yote hayo ni kutaka kuhalalisha fikra potofu na kuchafua taswira ya mtu, kwanini unaandika kwa uhakika wakati ni vitu vya kusikia?

3) Tatu unasema swala la Lwakatare. Kwa sasa Lwakatare ni mbunge na ni rafiki yangu na anajua ukweli wa yote yale yaliotokea na tunaongea mara kwa mara. Nitakupa namba yangu, hebu tafuta siku tukakae na Lwakatare mimi nawe akisema nilimsingizia nitaacha ubunge na uwaziri.

Jana tu, tar 20/12/2016 ilikuwa kesi hiyo hiyo wewe unasema kesi ilienda mpaka ikaisha! Uwe unapata ukweli kabla ya kuandika. Jambo hili halijaisha jana ilikuwa kesi, lakini Lwakatare anajua hili jambo, tunaongea mara kwa mara nadhani ungeacha tu jambo hili liishe liliko kwenye mkono wa sheria, usilichokonoe hata Lwaka hangependa ulichokonoe kama unavyofanya kwani yeye anajua ukweli, namba yangu ni 0714008888

4) Unasema nilisema nitatoa ushahidi wa mauaji ya SOWETO. Ndugu, kapitie upya kumbukumbu zako. Nenda kaongee na Lema hata sasa kulekule alipo, muulizie maana naye mwanzo alikuwa na mtazamo kama wa kwako.

Ushauri wangu: Kuandika hapa jamvini suala serious kama hili ni vyema ukafanya fact finding kidogo

Sasa kuhusu suala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu
Sijawah kumwamini mwanasiasa hata siku moja,ww ndo ulisema una ushahidi BUNGENI leo unawaambia watu wamuulize X sijui Y sijui Z,kwani alosema ana ushahidi si ww au kuna mwingine?
 
Kwanza akamatwe kwa yafuatayo:-
1. Kutumia mtandao usiosajiliwa Tanzania
2. Kutokana na 1 hapo juu, anahusika kuzuia polisi kutopata taarifa zake sahihi kwa kutumia mtandao wenye PTPE (Point To Point Encryption).
3. Alitoa taarifa ya kichochezi pale alipodai kuwa ile miili ni ya wahamihaji haramu.
4. Ahojiwe kama rafiki wa Ben kwani anaweza akawa na taarifa muhimu kuhusu kupotea kwake.

Nawasilisha...
 
hatumsaidii waziri kwa kuonyesha comment za kumsifia tu na kufuta mawazo mengine...acheni uoga
 
WanaJF,

Nimeamua (kama member wa JF) kuandika kwa masikitiko makubwa sana kufuatia uzi wa technically:

Mwigulu Nchemba ndiye suspect namba moja kupotea kwa Ben Saanane?

Vijana wenzangu, tuwe tunatafakari kwanza kabla ya kuaondika mambo makubwa yasiyo na utani bila kujiridhisha na tunachokiandika. Sio kitu kizuri kuandika jambo kubwa hivi kwa taarifa za kuungaunga na ufahamu wa kuungaunga.

1) Moja anasema watu wamezikwa bila kutambuliwa: Ni kweli watu hao miili ilishaharibika na hatua iliyokuwa inasitahili ilikuwa kuzikwa. Hata hivyo tumechukua sampuli kwa kila mwili nawe ukitaka kuitambua unaruhusiwa. Mpaka sasa haijulikani sana uhakika kuwa hao ni nani, lakini sisi tulisema kuna uhusiano mkubwa wa watu hao na wahamiaji haramu ambao waliokotwa 81 wakiwa mahututi eneo hilohilo na wiki hiyo hiyo.

Hatujasema kuwa ni kwa asilimia 100 ni wahamiaji haramu, tunasema huenda wakawa ni wao maana kama hao 81walikuwa hoi wiki hiyo hiyo huenda kati yao kukawa na baadhi yao ambao walishapoteza maisha na tukasema tuendelee na kutafuta undani zaidi, lakini wewe unasema tumezika bila kutambuliwa, hivi ni nani angewatambua? This is not fair.

Wapo wakadiriki hata kusema watu hao waliuwawa na Polisi, la hasha hata wakiwa wahamiaji haramu hawaruhusi kuuawa ndio maana Polisi ilipowaokota wale mahututi wakiwa hwawezi kuongea wala kusema iliwapikia uji na wengine kuwapeleka hosipitali.

Tunaongelea miili iliyookotwa, kumekuwa na kawaida ya wasafirisha watu kutupa miili hovyo, sishangai huenda hata wakawa walikuwa zaidi ya 81 wameokotwa saba, huenda wengine wakawa wamepelekwa baharini, ndio maana tunaendelea kutafuta undani.

2) Pili unasema kifo cha Mbagala kahusika Mwigulu, Eti alifika wa kwanza.

Si kweli, sikufika wa Kwanza. Angalia, kwanza tukio lilifanyika saa moja kwenda saa mbili hivi, akaenda OCD saa moja hivi, saa tatu akaenda RPC, saa nne akaenda Siro na IGP. Mimi nilienda Saa sita usiku na nimemkuta RPC na Kamanda Siro na video zipo. Niliwakuta na ndio walikuwa wananielekeza tukio lilipo. Unasema niliwatangulia polisi? Jitafakari. Yaani yote hayo ni kutaka kuhalalisha fikra potofu na kuchafua taswira ya mtu, kwanini unaandika kwa uhakika wakati ni vitu vya kusikia?

3) Tatu unasema swala la Lwakatare. Kwa sasa Lwakatare ni mbunge na ni rafiki yangu na anajua ukweli wa yote yale yaliotokea na tunaongea mara kwa mara. Nitakupa namba yangu, hebu tafuta siku tukakae na Lwakatare mimi nawe akisema nilimsingizia nitaacha ubunge na uwaziri.

Jana tu, tar 20/12/2016 ilikuwa kesi hiyo hiyo wewe unasema kesi ilienda mpaka ikaisha! Uwe unapata ukweli kabla ya kuandika. Jambo hili halijaisha jana ilikuwa kesi, lakini Lwakatare anajua hili jambo, tunaongea mara kwa mara nadhani ungeacha tu jambo hili liishe liliko kwenye mkono wa sheria, usilichokonoe hata Lwaka hangependa ulichokonoe kama unavyofanya kwani yeye anajua ukweli, namba yangu ni 0714008888

4) Unasema nilisema nitatoa ushahidi wa mauaji ya SOWETO. Ndugu, kapitie upya kumbukumbu zako. Nenda kaongee na Lema hata sasa kulekule alipo, muulizie maana naye mwanzo alikuwa na mtazamo kama wa kwako.

Ushauri wangu: Kuandika hapa jamvini suala serious kama hili ni vyema ukafanya fact finding kidogo

Sasa kuhusu suala la Ben Saanane:

Kwanza tumwombee kwa Mungu awe salama mpaka sasa. Tafadhali usiandike kwa hisia zako.

Ben is my personal friend (Sio katika Siasa) tunakutana na kushirikiana mambo kila mara mpaka ya familia, namfahamu na anaifahamu familia yangu mpaka watoto wangu wanamfahamu. Nilimsaidia kura za maoni ndani ya chama chake, nimewasiliana naye mfululizo mpaka wiki hiyo hiyo. Unamwongelea rafiki yangu na ndugu yangu wa ndani, na sasa nafuatilia kama serikali na kama rafiki.

Tafadhali, tuna mambo ya kisera tunaweza kupigana madongo, lakini hapa tunaongelea maisha ya mtu, an innocent young brother. Usikusanye vitu vya kuungaunga na kuleta katika jambo kubwa ambalo bado lina giza na wengine ni ndugu yao wa damu na wengine ni close friend.

Naamini mimi Ben ni rafiki wa karibu kwangu kuliko kwako mtoa mada maana ungekuwa mtu wake wa karibu ungejua haya ninayokwambia. Fuatilia mawasiliano yangu na Ben tangu mwaka juzi ndio uone who are we. I still believe kuwa Mungu anamlinda Ben na nchi yetu haijafika huko

Mwigulu

Umeandika kwa hekima kubwa sana ukilinganisha na cheo chako.........Umekua sasa kijana wangu sasa hata mji naweza kukuachia kwa maana najua hata wadogo zako utaishinao vizuri hata kama wanakuchokoza..................

UHURU TUMEPATA 1961 SASA MNATAFUTA NINI..........!!!!!????
 
Mkuu mngekuwa mnaongea kama unavyodai basi Wabunge wa UKAWA wasingefanyiwa manyanyaso mbali mbali ya kufukuzwa Bungeni kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu, kuwekwa ndani kwa kipindi kirefu kwa sababu ambazo hazina mashiko na pia kuidharau katika ya nchi pamoja na kuwa sasa hivi nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi.

Kama haya uliyoyaandika yana ukweli basi tungependa kuona juhudi zako za kubadili upepo wa kutisha nchini uzifanye hadharani badala ya kuja humu kwa kuwa tu umetuhumiwa.

Mbona siasa sio uadui? Kusema nilimsaidia? Mbona hata niliogombea nao 2010 wa oposition niliwapa mafuta ili kampen ziendelee! Shida wengine mnadhan kwenye siasa hatuongei
 
Back
Top Bottom