Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeanzisha huduma mpya ya upimaji Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini itakayofanyika nyumba hadi nyumba.
Waziri wa Wizara hiyo, Profesa David Mwakyusa, aliyasema hayo katika hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani hapa.
Hotuba ya Waziri Mwakyusa ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia.
Profesa Mwakyusa alisema wizara hiyo imeanzisha huduma hiyo baada ya kampeni ya kitaifa ya kupima virusi hivyo kwa hiari iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mwaka juzi.
Alisema katika mpango huo mpya, wahudumu wa afya watatembelea kila mwananchi nyumbani kwake na kumshawishi kupima VVU kwa hiari.
Alisema kwa kuanza huduma hiyo inatolewa wilaya za Bagamoyo mkoani Pwani, Mvomero (Morogoro), Kilolo (Iringa), Temeke (Dar es Salaam) na Arumeru (Arusha) na inatarajiwa kusambazwa wilaya zote nchini.
Alifafanua kuwa lengo la kuanzisha mpango huo ni kuwezesha Watanzania wengi kupima virusi, hivyo kujua kiwango halisi cha maambukizi nchini.
Alisema takwimu zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka huu, idadi ya watu waliopimwa VVU kwa hiari nchini imefikia milioni 7.3 na kusisitiza kila Mtanzania bado anahitaji kupima aweze kujua hali yake na kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yake.
Akihutubia taifa katika kilele hicho, Pinda aliwatahadharisha wananchi kuwa Ukimwi bado ni tishio kutokana na takwimu kuonyesha unaua watu wengi.
Pinda alisema hali hiyo inawatahadharisha Watanzania kutobweteka kwa kujipa matumaini kuwa maambukizi ya VVU yanazidi kushuka, bali wanapaswa kutambua kila mwaka unaua idadi kubwa ya watu.
CHANZO: NIPASHE
hongera waziri na wizara yako kwa kijitihada hizo.
hapo me naona inaweza kupunguza kasi ya maambukizo kama watu watajitambua kuwa wako salama au la.
watanzania tuunge mkono jitihada hizi, kwani ni kwa manufaa yetu wananchi, itachekesha pale watu watakafuatwa makwao halafu wakagoma kupima..