Kupiga Wabunge, ni dharau kwa Watanzania

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,807
Huko siku za Nyuma, Nilishawahi Kulalamika sana Kuhusu wabunge wa Upinzani, Kukamatwa Hovyo na Kupigwa wakiwa katika shughuli zao huko Mitaani. Hiyo ilikuwa ni Katika Serikali za Kikwete. Ungelitegemea Magufuli niliyemdhania kuwa Muugwana, Mkweli, Mpenda haki, angekomesha tabia hii chafu.

Lakini sasa wahuni kama Chenge wanaleta FFU bungeni Kupiga Wabunge ati kwa Kuwa wamekataa kutoka nje. Solution ya Kitu kama hicho ilikuwa rahisi sana, kuahirisha kikao na kufanya majadiliano ya kuleta ufumbuzi wa swala lililoleta mgongano. Sasa kwa Kuwa FFU ni Jeshi la serikali, na Rais amekaa kimya, inaonekana aliagiza hilo au hata kama hakuagiza lilimpendeza. Mimi naona Linamchafua sana Ndani na Nje, Ni aibu kwa Utawala wake ni Dharau kwa wananchi.

Haya yamewezekana kwa sababu ya Utawala wa "milele" wa CCM Unaoamini kutawala kwa Nguvu za DOLA na Wizi wa Kura na Mizengwe. Tabia hii Italifikisha Taifa Pabaya na siku Moja CCM watakosa muda wa Kujutia.

UBUNGE NI DHAMANA YENYE HESHIMA SANA. KAMA ALIYEPEWA DHAMANA HIYO HAJIHESHIMU NA ANASHINDWA KULIHESHIMU BUNGE, HAKUNA NAMNA NYINGINE NI KICHAPO TU NA MIMI NASEMA WACHAPWE TU MAANA WAMEJITAKIA
 
Kuna siku utachapwa wewe ndipo utajua maana ya haki za wengine za msingi
 
Ukiona wawakilishi wetu wanaotunga sheria na kuisimamia Serikali wanatendewa hivyo ujue wewe mwananchi wa kawaida unaonekana ni nyumbu
 
UBUNGE NI DHAMANA YENYE HESHIMA SANA. KAMA ALIYEPEWA DHAMANA HIYO HAJIHESHIMU NA ANASHINDWA KULIHESHIMU BUNGE, HAKUNA NAMNA NYINGINE NI KICHAPO TU NA MIMI NASEMA WACHAPWE TU MAANA WAMEJITAKIA

What? Really Umefunikwa kwenye gunia la Tanzania ya Enzi hizo! ya Zidumu fikra za Mwenyekiti Pole sana Mzee wangu.Ni bora CCM wasome alama za nyakati la sivyo, hiyo mizegwe yao, Viburi na Kufuru zao watakuja juta! Tena Miaka si Mingi. A cigarette but can inflame to whole jangle leaving people to wonder, "allas how did this great and destructive fire started!" Msitu mzima unaweza kuchomwa moto na uzembe wa Kipisi cha sigara! Na watu watabaki kustaajabu, moto huu wa Maangamizi umeanzaje"
 
Hovyoooo! Wabunge wa namna ile wasio jiheshimu hawastahili kuheshimiwa!

Yaani Wabunge watukane kila mtu wanayeona inawafaa kutukana eti watukane tu?

Nyumbu nyie
 
Hatuwezi kuwa tunaahirisha bunge kila dakika,NASEMA WAPIGWE TU MAANA HAMNA NAMNA INGINE.

Wabunge wavuta ndumu kama halima au sugu,lema ndo lugha wanayoielewa hiyo
 
Wabunge wanajidhalilisha wenyewe,wangeacha mihemuko ya kichama na kufuata sheria kikamilifu kusingekuwa na haja ya jeshi.
Kama mtu anatukana tusi kubwa anaachwa namimi ntatukana tuu,zifungwe kamera za kutosha wanaotukana wafuatiliwe hâta baada ya kikao na adhabu ziwe nzito.
Polisi watawadharau wabunge wote,nasisi pia tutawadharau maana wanashindana matusi kama wamama wa uswahilini na wanapigwa na polisi kama wapigwavyo mateja wapigadebe.
Heshima haiji kwakuvalia suti na tai au dera,ni mkusanyiko wa fikra na vitendo mujarab, uheshimiwa wa wabunge unakaribia kufutika
 
Back
Top Bottom