Luushu
JF-Expert Member
- Apr 8, 2012
- 812
- 468
Habari Wana jamvi,
Huku kwetu kumekuwa na ka staili ka KUPANDISHANA VYEO KIJANJA, kwenye kata yetu tulikuwa na weo mwenye Degree na kazi alikuwa anachapa ipasavyo akahamishwa kapelekwa kata jirani ya ulemo na kyengege akaletwa veo mwenye certificate kutoka Kijiji Cha kidaru kuja kuwa kaimu weo Sasa ni mwaka wa pili na nusu
Swali kwa mamlaka husika ni kweli hakuna waajiriwa wenye sifa mpaka akaimishwe huyu,hapa katani wapo veo Wana diploma kwa Nini hawakukaimishwa kakaimishwa veo Makala wa kidaru?
Pia mwaka huu mwezi wa pili alihamishwa mwalimu mkuu mwenye degree kutoka shule ya msingi Mugundu,akaletwa mwalimu mwenye certificate kutoka shule jirani ya kyengege kuja kukaimu ualimu mkuu wakati hapo shuleni wapo walimu wenye diploma ambao kwa uelewa wangu ndio walifa kukaimu kitu ambacho kimeleta mfarakano mkubwa Kati ya walimu.
Swali afisa elimu,mkurugenzi mmeridhika haya yanayotokea au mnapewa vi memo na mwenyekiti wa halmashauri ambae ndie diwani wa kata hii, au mnapewa vimemo na waziri wa fedha ambae ametoka kwenye kata hii na mnashindwa kukataa kwa kutetea kibarua chenu?
Kama ni hivyo basi tunaomba mamlaka za juu zaidi zije zitusaidie ikiwemo takukuru mkoa ichunguze harufu ya rushwa inayo sababisha kushuka kwa maendeleo kata ya kyengege na kushuka kiwango Cha elimu shule ya msingi Mugundu