Kupambana na ufisadi taasisi zetu zijengewe uwezo na kupewa kinga

moshingi

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
278
92
Nimekuwa nikufuatilia "upepo" unaoendelea kuvuma bungeni ambao inasemekana
"Baba mwenye nyumba" amesema utapita tu. Lakini upepo huo sio mgeni, pamekuwepo
na matukio kama haya kila mara wakati bunge letu linapojadili mambo mbalimbali na hasa
yanayohusiana na taarifa za CAG. Lazima tujiulize ni kwanini taasisi zetu zilizopo kwa mujibu
wa sheria zimeshindwa kuitibu hali ya wizi, ufisadi, na matumizi mabaya ya madaraka iliyokithiri
katika taasisi na wizara zote za serikali? Wapo watu wanaoelekeza tuhuma kwa TAKUKURU,
lakini TAKUKURU kupitia mkurugenzi mkuu alinukuliwa akilalamika kwenye mtandao wa wikileaks
kuwa "Baba mwenyenyumba" hana nia ya kweli ya kupambana na ufisadi(labda ukweli utajidhihirisha
hivi punde kwa yanayoendelea), tena amenukuliwa akisema hadharani(Dr. Hosea) kuwa anakwamishwa
na ofisi ya DPP. Ni mawazo yangu kuwa ili kulinda fedha za uma dhidi ya wezi na mafisadi zitumike
taasisi zilizopo kisheria kama vile TAKUKURU na ofisi ya DCI lakini yafuatayo lazima yarekebishwe.
(i) Wakuu wa idara hizo mbili wapewe kinga kisheria kama aliyonayo CAG katika katiba.
(ii) Mara mtu akiteuliwa kushika madaraka katika taasisi hizo, rais akatazwe kumteua tena katika
nafasi yeyote ile kabla au baada ya kustaafu ili kumfanya asijipendekeze kwa matumaini ya fadhila
za baadaye.Sharti hili lielekezwe pia kwa majaji wa mahakama zetu.
(iii) Kwakuwa taasisi hizi zimesheheni watumishi wenye taaluma ya sheria kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje
basi zipewe mamlaka ya kushitaki wezi na mafisadi wa mali za uma bila ya kuomba kibali toka kwa DPP.(watumishi
wa ofisi ya DPP hawana sifa za ziada, ni wanasheria kama wenzao)
(iv) Ofisi ya CAG iwe na kitengo cha kuendesha mashitaka ili mara wanapobaini jinai wawafikishe wahusika mahakamani AU
(v) Sheria irekebishwe ili wakati wa ukaguzi CAG akibaini wizi au ufisadi aripoti moja kwa moja kwa DCI au TAKUKURU.
(vi) Taasisi hizo zihakikishiwe bajeti zake na ziwe huru (Independence)

Hayo ni mawazo yangu tuu, nakaribisha wanabodi wenye mawazo mazuri ili tuijenge nchi yetu bila hofu ya wizi, hatakama CCM hawatakuwako madarakani. Tuufute usemi wa Mzee wa Kiraracha "nchi hii inajengwa na wenye moyo
na kuliwa na wenye meno" Karibuni.
 
Umenena vyema! Kwenye katiba mpya, viongozi kwenye taasisi kama takukuru, dpp, dci wasichaguliwe na mtu mmoja. Nafasi zitangazwe, watu wasailiwe na ajira zifanywe aidha na bunge au "jopo kazi"na ziwe kwa mkataba wa muda maalum tu!
 
Watanzania kwa mikakati hatujambo, mikakati hii ikitumiwa na nchi nyingine inafanikiwa lakini kwetu haifanikiwi
 
Watanzania kwa mikakati hatujambo, mikakati hii ikitumiwa na nchi nyingine inafanikiwa lakini kwetu haifanikiwi

Mikakati hii itafanikiwa bila shaka kama kwa umoja wetu tukihakikisha mambo ya msingi yanakuwemo kwenye katiba
mpya ijayo...nchi hii bila ufisadi inawezekana
 
Back
Top Bottom