Kuongezeka kwa matangazo ya kuongeza nguvu na maumbile ya kiume tatizo ni nini?

foroy

Senior Member
May 2, 2018
186
288
Mambo yanaenda kasi sana.

Kwa ujumla mambo mengi yanatembea kwa spidi ya kuogofya. Unaweza usiogope kama unayatazama kwa macho mawili, lakini ukihusisha jicho la tatu lazima utaingiwa hofu.

Habari za vita, mauaji ya kutisha ushoga, majanga ya asili nk. ni sehemu ya taarifa zinazoanza kuzoeleka masikioni mwetu kiasi kwamba hazishtui tena.

Utamaduni wa kubet umevuma kiasi cha kuwa kama fasheni mpya ya mavazi, hakuna anayetaka kupitwa. Siku hizi hadi wanawake wanabet na hakuna anayeshangaa!

Kwenye msafara huu wa mambo yanayoenda kasi kiasi kwamba watu wamechoka kushangaa ni pamoja na hili la matangazo ya nguvu na ongezeko la maumbile ya kiume.

Kama ilivyo kwenye hayo mengine; nimejikuta nikishangazwa na utitiri wa matangazo yanayohusisha madawa ya kuongeza nguvu na kuongeza ukubwa wa maumbile (nyeti). Siku hizi huwezi kuperuzi kurasa mbili au tatu mtandaoni bila kukutana na matangazo hayo. Hata watu wetu maarufu (mastaa) wamekuwa wakitumika sana kupromote madawa hayo.

Ndiposa yanapoibuka maswali kichwani mwangu;

1)Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ni kweli lipo au ni shida mpya ya kisaikolojia kwa kizazi cha leo?

2) Kama ni kweli lipo, kwanini iwe sasa na si wakati mwingine wowote?

3)Hayo madawa yanayopigiwa chapuo kuongeza maumbile na nguvu za kiume, ni kweli yanafanya kazi husika au ni utapeli? Na kama kweli yanafanya kazi vipi kuhusu madhara yake?

4) Upi msimamo wa serikali kuhusiana na madawa ya aina hii? Yamethibitika kitaalamu kutatua changamoto husika bila madhara?Kwanini ipo kimya kuhusu uhalali au uharamu wa madawa hayo kama walivyofanya katika vipodozi vyenye madhara?

5) Nani kati yetu aliyewahi kutumia madawa haya anaweza kuwa na ujasiri wa kutupa shuhuda adili kuhusu madhara ama faida ya madawa haya kwa faida ya jamii nzima?

6) Wewe binafsi, kwa uzoefu ama utaalamu wako una mtazamo gani kuhusiana na hili la kuongeza maumbile na matumizi ya madawa ya kuchochea nguvu? Unaunga mkono au unapinga? Kwasababu gani?

Tupeane uzoefu.
 
Kama mtu anataka nguvu za kiume kwa wingi ajikite kula vyakula vya asili. Sasa mtu analilia nguvu za kiume, zitatoka wapi wakati anakula vyakula feki? Ndio maana wale mastaa warembo hawaachi kutoa siri za mapenzi yao kwa wapenzi wao wanaokutana nao kushindwa kufanya penzi kwa ufanisi na ubora wake. Unajilia msosi wa kidosho halafu unaenda kupiga shoo, utaishia kuabika
 
Kama mtu anataka nguvu za kiume kwa wingi ajikite kula vyakula vya asili. Sasa mtu analili nguvu za kiume, zitatoka wapi wakati anakula vyakula feki? Ndio maana wale mastaa warembo hawaachi kutoa siri za mapenzi yao kwa wapenzi wao wanaokutana nao kushindwa kufanya penzi kwa ufanisi na ubora wake. Unajilia msosi wa kidosho halafu unaenda kupiga shoo, utaishia kuabika
hata kama unakula vyakula vya asili vya kimasai kama mwili wako haujishughulishi ,hizo nguvu zinatkuwa shida tu
mwili umeumbwa kufanya kazi za jasho
hilo la vyakula si la kupuuza pia. tunakula makapi
 
Mitandao ni adui mkubwa wa binadamu,tatizo linaweza kukuzwa na kuanza kuwepo kupitia mtandao.


Huanza wachache ila wengi wanaanza kulipata.
 
Back
Top Bottom