Kuombana Msamaha Siyo Suluhisho la Changamoto za Ndoa Tafadhali Badilika

Vumbi

Senior Member
Nov 7, 2010
191
27
Wana ndoa wengi wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi sana ndani ya ndoa zao na wengi wamekuwa wakikimbilia kuombana msamaha au kusameheana kama njia ya kuokoa ndoa hizo. Lakini sidhani kama kuombana msamaha ni kigezo pekee cha kutatua matatizo ya ndoa. Kitu ninacho fikiri kama kigezo kikubwa cha kutatua changamoto wanazokutanazo wanandoa ni wanadoa wenyewe kwa uwazi kujadili yafuatayo: i) chanzo/kiini cha mwanadoa kuingia kwenye tatizo ii) kwa nini mwanandoa anadhani anaweza kuliancha tatizo ii) Njia anazodhani mwanandoa zinaweza kuzuia asirudi tena kwenye tatizo iv) mkakati wa pamoja wakuizuia tatizo lisirudie v) Hatua zitakazo chukuliwa iwapo atarudia etc. Then baada ya hapo peaneni msamaha muanze maisha mapya. Vinginevyo hata mkipeana msamaha hiyo ndoa mwisho wake umekaribia au mmoja wa wanandoa atakuwa anaishi maisha ya mateso makubwa.

Nimeamua kusema haya kwa sababu mke wa ndugu yangu ameleta malalamiko ya kuomba talaka kwasabu mume wake anatoka nje ya ndoa ameshamkamata na kumsamehe zaidi ya mara tatu. Nikumuuliza kama walishawahi kujadili na mumewe kwanini anatoka nje ya ndoa, kwa nini hawezi kuacha, mikakati gani ili aweze kuacha hiyo tabia etc huyu mama akaniambia walikuwa wanagombana then jamaa anaomba msamaha anamsamehe wanaendelea na maisha. Kwamaelezo niliyo pewa na huyu mama ninaamini kwa ujumla kwamba msamaha siyo njia pekee ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye ndoa kwani baada ya kukutana kwenye kikao na jamaa kueleza kiini cha tatizo la ndoa yao tuligundua kuwa kama wangefanya niliyo yaeleza hapo juu ndoa yao isingefika hapa ilipo. Mbaya zaidi imebidi talaka ikubaliwe. Samahani sikuzungumzia kwa undani kilichotokea ndani ya ndoa hiyo kwa maslahi ya wanandoa husika kwani ni wanachama wa hapa JF.
 
Napenda kusema mimi si mpenzi na mshabiki wa samahani, nimeshuhudia matukio kibao ya katika ndoa na maisha kiujumla, mtu anatenda kosa au anaacha kufuata magizo tena raisi kabisa zaidi ya mara moja alafu anakimbilia kusema samahani. kwa kweli sahamani hizo huwa zina kera na kuudhi sana, muombwaji wa hiyo samahani anaweza hisi anakejeriwa tu.

kwa kesi hii hapo juu nadhani watu uogoba kujadili wakizani watafufua machungu na maswali mengi hasa kutoka kwa mtendwaji; kwa mtendaji samahani huwa ni rahisi kusema, na baada ya msamaa wasingependa kurudi kwenye kikaango
 
Wana ndoa wengi wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi sana ndani ya ndoa zao na wengi wamekuwa wakikimbilia kuombana msamaha au kusameheana kama njia ya kuokoa ndoa hizo. Lakini sidhani kama kuombana msamaha ni kigezo pekee cha kutatua matatizo ya ndoa. Kitu ninacho fikiri kama kigezo kikubwa cha kutatua changamoto wanazokutanazo wanandoa ni wanadoa wenyewe kwa uwazi kujadili yafuatayo: i) chanzo/kiini cha mwanadoa kuingia kwenye tatizo ii) kwa nini mwanandoa anadhani anaweza kuliancha tatizo ii) Njia anazodhani mwanandoa zinaweza kuzuia asirudi tena kwenye tatizo iv) mkakati wa pamoja wakuizuia tatizo lisirudie v) Hatua zitakazo chukuliwa iwapo atarudia etc. Then baada ya hapo peaneni msamaha muanze maisha mapya. Vinginevyo hata mkipeana msamaha hiyo ndoa mwisho wake umekaribia au mmoja wa wanandoa atakuwa anaishi maisha ya mateso makubwa..

Ubarikiwe sana Vumbi,yaani umeongea mambo ya msingi sana na yenye mafundisho ya namna ya kutafuta masuluhisho ya matatizo si kukimbilia tu kusema samahani......na baada ya hapo hujatatua tatizo.......excellent!!:clap2:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom