Kuna watu wanaojua siri ya uumbaji? Kwanini wapo kimya?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Salamu!

Natafakari sana. Hizi tafiti zote za kuhusu Mars na sayari nyinginezo, hivi haiwezekani kweli baadhi ya watu wakawa wanajua mambo yote ila wakakaa kimya?

Kitendawili cha siri ya uumbaji wa binadamu na dunia, hivi hakuna wanaoweza kutegua kitendawili hiki kweli?

Sitaki kuamini kuwa binadamu wote dunia nzima ni wajinga kwenye haya.

Hivi hawapo binadamu wenzetu wanaojua siri zote hizi na wakaka kimya tu?

Hivi hawapo binadamu wenzetu wanaojua kesho za wenzao na wakakaa kimya?

Hivi hakuna watu wanaojua mpaka siri za Mungu na wamekaa kimya?

Hivi hakuna watu wa namna hiyo?

Swali ni je, kwa nini wakae kimya?

Kipi kipo nyuma ya pazia?

Kwamba wanatu enjoy? Kwa nini?

Tafadhali tuidadavue hoja hii. Sitaki kuamini kabisa.
 
Back
Top Bottom