Kipunguni
Senior Member
- Jun 20, 2008
- 151
- 4
Hiyo ni photoshoped na nitawaeleza kama nilivyowaeleza kuhusu ile picha ya Mwanamama wa CUF alionekana kulala bungeni ,ila hapa inataka uone tofauti ya kivuli ,kitu ambacho wengi ya wanaotumia photoshop huwa wamejawa na jazba na factor hii ya kivuli huwaumbulisha vibaya sana.Nimegundua kuna kivuli kwa chini ya bendera kitu ambacho kisingekuwepo kwani huwa bendera imeganda na si yakutoa kivuli,vilevile ukitazama juu ya bega kuna kikoti ambacho kwa jinsi ya kivuli cha bendera kilivyoangukia basi na lile pango la kikoti ambalo ni kubwa nalo lingetoa kivuli kilichokaribia nje kabisa lakini kinaonekana kivuli chake hakipo kimemezwa kwa ndani.
Jengine huyo jamaa ni mzungu kutoka kikosi cha mizinga au kwenye magari ya deraya na ukitaka kumuona uzuri ,copy the properties of the picture .itaonekana kama inavyofuata bila ya mabano { http://www.} jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=1967&d=1218536045
na paste kwenye bar halafu kama unatumia explore 7 and above unaweza kuikuza picha mpaka kwenye 400% chini mkono wa kulia wa browser yako kipo kinakuwepo kitendea kazi hiyo ,unauona upande wa uso wa huyo jamaa kuwa ni mzungu na si mwafrika japo wapo waafrika weupe.
Rangi zetu nyeusi zinafanana na kivuli hivyo kusingetokea alama yeyote ya uso kama sikio na rangi nyeupe kwenye sehemu za mashavu au shingo ambayo imejifichaficha,halafu sidhani kama wabunge watauvaa mkenge wa kwenda kuuliza suala hilo itakuwa nao hawana muelekeo wanakotomezwa ndio huko huko.
Sasa swali linakuwa, kwa nini AP/Reuters or is it Yahoo wafanye usanii wa kuweka bendera ya TZ hapo??!!