Kuna umuhimu wa kurejesha "operation" ya wahujumu uchumi Tanzania?

BITTY NGUZO

Member
May 26, 2009
32
4
Kwa muda mrefu serikali imeshindwa kudhibiti bei za bidhaa mbalimbali,nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 1980 aliyekuwa waziri mkuu marehemu Edward Moringe Sokoine aliendwsha zoezi la kuwakamata wahujumu uchumi.Zoezi hili liliwagusa sana wafanyabiashara ambao walikuwa wanauza bidhaa mbalimbali kwa bei ya kulangua.Nawauliza wana "jf" je,kwa sasa kuna umuhimu wa kurejesha operation hiyo ili serikali iweze kudhibiti wafanyabiashara na mfumuku wa bei?:redfaces:
 
Haja ipo lakin mmh!! PINDA au JK. ....jacli cmuon hapo labda Samwel 6.
 
haiwezekani kabisaa under CCM ya JK labda Babu wa Loliondo aweke sharti hili kwa vigigo wanaotaka dawa yake
 
Kwa muda mrefu serikali imeshindwa kudhibiti bei za bidhaa mbalimbali,nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 1980 aliyekuwa waziri mkuu marehemu Edward Moringe Sokoine aliendwsha zoezi la kuwakamata wahujumu uchumi.Zoezi hili liliwagusa sana wafanyabiashara ambao walikuwa wanauza bidhaa mbalimbali kwa bei ya kulangua.Nawauliza wana "jf" je,kwa sasa kuna umuhimu wa kurejesha operation hiyo ili serikali iweze kudhibiti wafanyabiashara na mfumuku wa bei?:redfaces:

Sasa hivi TZ inaongozwa kwa mfumo wa biashara huria, hauwezi kusema mtu anahujumu uchumi kwa kupandisha bei. Mwenye bei ghali ataondolewa kwenye soko na mwenye bei ya chini, tumeona mfano kwenye makampuni ya simu.
 
Hii sheria bado ipo na ingefaa kutumika wakati huu! Bahati mbaya sheria hii ni kama mtego wa panya; haitashia kwa Dowans na Richmod pekee, bali hata akina yakhe wenye vijimagendo vyao vidogo vidogo wataathirika.

Kwa wale wazee wenzangu walioshuhudia zoezi la hayati Sokoine miaka ya 1983, ingawa tuliandamana kumuunga mkono lakini ilifuatia miaka kadhaa ya maisha magumu sana huku ndugu zetu wengi wakiwa kizuizini bila kufikishwa mahakamani.
 
umuhimu wa kufanya safisha safisha ni mkubwa sana kwani kuna watu wamejinufaisha kwa kutuibia wananchi.
ikiwezekana wafilisiwe kabisa.
na jambo jema ni kwamba nyangumi hao wanajulikana,au hadi tutajane?
 
Wengine wanajulikana lakini wengi itabidi tutajane. Hawa wanaoandamana wangekuwa wanadai hili wengi wetu tungeingia barabarani.
 
NDIYO. Lakini nani wa kuiongoza? Wahujumu uchumi ndiyo wanaotutawala. Hao ndiyo mafisadi wenyewe. Basi, sisi wenyewe wananchi ndiyo tunaopaswa kuiongoza. Tuupuuzie mbali madai ya mafisadi na mawakala wao kuwa, kupambana na ufisadi ni UHAINI. Tumeanza tusikate tamaa...
 
Yu wapi Sokoine?nani amrithi? Wamebaki waoga na washirika tu!
 
Back
Top Bottom