Mwalimu wangu wa somo la jiografia alinifundisha ya kuwa dunia inalizunguka jua katika mhimili wake kwa muda wa mwaka mmoja. Pia alisema mwaka mmoja huo waweza kuwa ni siku 365 na 1/4 au siku 366. Lakini katika gregorian callendar inayotumika nchini mwetu ili mwaka uwe mfupi(siku 365 na 1) au mrefu(siku 366) inategemea mwezi wa pili una siku ngapi, kama siku ni 28 ndipo tunapata mwaka mfupi na kama siku ni 29 tunapata mwaka mrefu. Kwa mjibu wa kautafiti kangu kadogo nilikofanya ambako hakakuwa rasimi nimegundua ya kuwa ili tupate mwaka wenye siku 29 katika mwezi wa pili ni lazima miaka mitatu yenye siku 28 katika mwezi wa pili ifuatane mfano mwaka 2008 ulikuwa na siku 29 katika mwezi wa pili 2009,2010 na 2011 hii yote ilikuwa na siku 28 katika mwezi wa pili 2012 utakuwa na siku 29 katika mwezi wa pili 2013, 2014 na 2015 itakuwa na siku 28 katika mwezi wa pili. Sasa huu utaratibu unatokana kweli na mzunguko wa dunia au unatokana na kuwekwa na wanadamu? Kwa anayefahamu anieleweshe juu ya umhimu wa miaka mitatu kuwa ni mifupi(yenye siku 365 na 1/4) ikifuatiwa na mwaka mmoja ambao ni mrefu(wenye siku 366). Handsome wa mama nawasilisha.