AbasMzeEgyptian
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 407
- 312
Bodi mpya ya NSSF imeridhia maombi toka kwa Bosi mpya wa NSSF kuwa wakurugenzi na mameneja wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma mabali mbali.
Lakini cha ajabu wakati wameneja na wakurugenzi wamesimamishwa kuna huyu mwana mama (EUNICE CHIUME) ambaye ni Meneja Kiongozi ambaye alikuwemo kwenye kamati zote za manunuzi na kamati zilizokuwa zikikaa kupitisha miradi mikubwa amebakishwa na anaendelea na kazi
Hii ina maana kuwa huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF amekuwa compromised au kapigwa presha toka kwa wazazi wake huyu binti ambao ni wazito sana kwenye serikali ya Magufuli?
Hivi inaingia akilini kuwa tenda board ya watu 8 ilipitisha mambo tena kwa kutia saini lakini wakati wa hukumu wahukumiwe watu 7? Hii inaingia akilini kweli? Kuna siri gani au instructions zimetolewa kuwa huyu mama asiguswe?
Credibility ya huyu mkurugenzi na board mpya ishaanza kuwa questionable.