Kuna nini Hospitali ya Kairuki?

Mleta mada hii umenikumbusha mbali nimepata uchungu sana nilipoteza mke wangu Monica mwaka juzi na alikuwa staff mwenzao hospital hiyo haifai jamani. mwenye kupinga cku apeleke ndg yake kwenye upasuaj km atarudi.
Oooh,pole sn mkuu.
 
Why majority of the operations are not sucessful, watu wanapoteza maisha, what the heal is going on?

Ni hayo tu...kwa anaejua tatizo la pale embu afungue macho na wengine.

Watu wengi ninaowajua waliofanyiwa upasuaji pale they didn't make it, to bad.
Jamani vipi kuhusa TMJ,wenyewe wapo vizuri ??
 
Takwimuunazotakiwa kutafuta ni idadi ya walifanyiwa operatins, walikua na matatizo gani, wangapi walikufa, pia kama unahisi kuna uzembe kwa operation unazozifahamu unaweza kupeleka malalamiko Halmashauri ya Kinondoni ili yafuatiliwe.
 
With all these testimonies,it goes uncontroverted kwamba Kuna tatizo mahali hapo.Nilienda kutoa jino pale nilichofanyiwa mpaka Leo sina hamu.Acha kabisa❕
 
Hujaitendea haki Hospitali ya Kairuki.
Inawezekana wewe ndo tatizo, jamani kama kuna mtu anamjua huyu mleta mada asijaribu kuoparetiwa Kairuki.(joking)

Mleta mada ungekuja na takwimu with comparisons ingekuwa poa.
 
Watu wanakufa na kupoteza Ndugu zao alafu wewe unataka comparison? Wasomi nyie
 
ni mwaka Jana December nilimpeleka Mzee wangu pale..akiwa na tatizo la pressure na kisukari..akalazwa pale.wakamfanyia vipimo vya ct scan xray na ultra sound...majibu yakatoka Kuwa Mzee ana Kansa na tayari imeshaozesha mapafu,maini,utumbo mwembamba...nikajiuliza mbona dalili za kansa hana na anatembea na kula vizuri na pia kuongea!!tukabishana iweje viungo vote muhimu view vimeoza na Mzee haoneshi dalili za kuwa na Kansa...nikamuuliza Dr nkemerwa kairuki cjui ndo mtoto wa hay at kairuki juu ya hyo Kansa...ckujibiwa vzur baadae..wakat Niko pale naongea na Dr nkemerwa Kuna Dr mwingine wa kike alimwambia Mzee Kuwa una Kansa na imeozesha INI na mapafu...mzee pressure ikashuka na hatimae akarudi nyumbani kwa baba muumba.......mpaka Leo cna hamu na Hosp ile..

pole sana...nimeshikwa na hasira na uchungu jamani.unamwambiaje mtu juu ya ugonjwa serious kirahisi hivyo?
Poleni kwa kumpoteza baba
 
pole sana...nimeshikwa na hasira na uchungu jamani.unamwambiaje mtu juu ya ugonjwa serious kirahisi hivyo?
Poleni kwa kumpoteza baba

Watanzania mnajua kulalamika, wewe umekwenda kupima mwenyewe sasa ulitaka akwambie huna cancer ili iwaje. NA bahati mbaya kwenye medicine hakuna majibu nusu nusu. Kitu kama ni positive hakiwezi kuwa negative. Kutembea ukiwa safi haimaanishi kuwa afya yako ni bora. Msitake huruma mahali pasipo stahili. Hii issue ya operation ipo kimhemko zaidi kuliko uhalisia. Twambie huyo ndugu yako alifanyiwa operation ya nini. NA alikuwa na ugonjwa gani. Kuna magonjwa mengine kupona na kufa ni 50 50. Sasa wewe alifanyiwa nini. Tuache kulalamika. Hujaridhika na huduma kawaone wenyewe Hujaridhika nenda mahakamani simple
 
Hujaitendea haki Hospitali ya Kairuki.
Inawezekana wewe ndo tatizo, jamani kama kuna mtu anamjua huyu mleta mada asijaribu kuoparetiwa Kairuki.(joking)

Mleta mada ungekuja na takwimu with comparisons ingekuwa poa.

This is ridiculous.

Unataka mleta mada alete takwimu atazipata hizi takwimu kutoka wapi?

lin ameleta malalamishi yake binafsi na lengo lake ni kuona kama kuna watu wengine hapa wenye experiences zao (nzuri au mbaya) waziweke.

Nimepitia mabandiko yote hapa na mpaka sasa wanaosema hospitali ina matatizo ni wengi kuliko walioridhika na huduma. Hii pengine haiashirii chochote kuhusu ubora au udhaifu wa hii hospitali lakini nadhani ni jukumu la hospitali (au wizara ya afya) kufanya tathmini huru (independent evaluation) ya huduma zao.

This is a serious PR (public relations) problem.

Kuipuuzia tu hii shutuma na kusema "LETE TAKWIMU" ni sawasawa na kuzamisha kichwa chako kwenye mchanga ukadhani watu hawakuoni tena kwa sababu tu wewe huwaoni.
 
He, mambo haya tulikuwa tunayasikia lugalo sasa yamefika kairuki! aghakan nako watu wanalalamika, sasa tutatibiwa wapi
 
Naona wengi wenu mnaolalamikia Kairuki ni vijana na pengine mumeanza kuitumia hivi karibuni. Mimi nilishaapa hata BURE siwezi tibiwa pale na nitoka miaka zaidi ya 20 ilihopita. Na enzi zile ni wahaya na watu wa assemblies of God ndio palikuwa mahala pao pa matibabu.

Miaka ya hivi katibuni na baada ya hizi bima ya afya na pia walipoanza kutoa mafunzo Kairuki imebadilika sana. Nilitaka kuaminishwa hivyo ila nina data kibao kuhusu ile hosp.

Nina watu wawili wamefatiki pale kwa uzembe. Mmoja rafiki yangu wa karibu sana. Yeye alienda pale akiwa na homa kali ila kadri siku zilivyoenda tunaambiwa ini hadi alipokufa tukaambiwa ukimwi. Kosa ni kwamva niliambiwa hivyo tukiwa mazishini morogoro. Niliruka na kukataa katakata haiwezekani. UNAJUA KWA NINI? Nilikuwa mjamzito mwanzo wa mwaka huo na rafiki yangu alinisindikiza kupimwa VVU nilikuwa naogopa akaamua kupima na yeye majibu yalitoka tuko salama wote. Iweje ndani ya miezi 6 apate ukimwi augue hadi kufa? Ubaya ni kwamba ukiwa seropositive taarifa zako zinaandikwa kwenye charts ili Dr akiingia aweze kuwa mwangalifu katika kukuhudumia. I was perplexed! Maana nilizisoma na haikuandikwa popote. Kwenye cheti cha kifo wakaandika HIV (?) sasa alama ya kiulizo ya nini? Hawakuwa na uhakika?

Kesi ya pili ni kifo cha mke mwenzangu alienda kujifungua wakamweka muda baadaye wakamfanyia operation wakadai alipoteza damu nyingi na pia kichanga kilikufa. Well tulimwachia mungu.

Kesi ya tatu na ya mwisho inamhusu mwanangu. Watoto ni watundu sana na huyu wa kwangu ni no exception. Nilikuwa namsuka na shanga si unajua tena mtoto wa kike. Basi akaamua siku hiyo kuweka shanga puani. Basi ilipogoma akaja kunionyesha mama yake nilihangaika kweli kuitoa bila mafanikio so nikamkimbiza kwa kairuki. Kufika kule aliingizwa theatre. Mimi na baba yake tunasubiri. Madaktari wanamtoa wakasema hawajaiona hiyo shanga. Lo!!!! Walinitambua siku hiyo. Nikawaambia what are you saying? Kwamba mimi ni mwongo???? Nimtoe mwanangu nyumbani kumleta ili mumshikeshike!!!! Je na huyo daktari aliyeandika maelezo naye ni mwongo hakuiona??? Aise nikawangangania kuwa wameisukuma ndani na wakaitoe maana siondoki bila ya kuiona shanga wameniletea mkononi. Kwa aibu wakarudi ndani theartre na kumtoa shanga na kuniletea mkononi. Naona aibu hata kuwataja hao madakyari kwa majina maana mmoja ni daktari bingwa na anaheshimika sana. Niliumia na huo ndio ukawa mwisho wangu wa kwenda pale.

Kwangu Kairuki imebakia kwenda kuona wagonjwa na hata nikienda huwa nabaki kuwashangaa sana wamepachaguaje. Wengi wao wanadai kuna ndugu daktari pale au Nesi ndio maana waneenda pale.

Kwa heri Kairuki hosp!
 
BiMkubwa umenifanya niiogope kairuki na hata siijui ilipo btw choice zangu nj regency na MNH.
 
Last edited by a moderator:
Majuzi nlikua hosp ya tmj kukawa na taarifa za msiba wa dakt bingwa mmojawapo hapo tmj ambae alienda mufanyiwa operation kwa dkt kairuki.wanasema alienda mzima kabsa tena anadrive mwenyewe akiwa na familiya yake...baada ya operation the next day alifariki dunia.hii nimeikuta juzi tu nlikua hapo tmj hospitali

Hyu daktari anaitwa nani?
 
Naona wengi wenu mnaolalamikia Kairuki ni vijana na pengine mumeanza kuitumia hivi karibuni. Mimi nilishaapa hata BURE siwezi tibiwa pale na nitoka miaka zaidi ya 20 ilihopita. Na enzi zile ni wahaya na watu wa assemblies of God ndio palikuwa mahala pao pa matibabu.

Miaka ya hivi katibuni na baada ya hizi bima ya afya na pia walipoanza kutoa mafunzo Kairuki imebadilika sana. Nilitaka kuaminishwa hivyo ila nina data kibao kuhusu ile hosp.

Nina watu wawili wamefatiki pale kwa uzembe. Mmoja rafiki yangu wa karibu sana. Yeye alienda pale akiwa na homa kali ila kadri siku zilivyoenda tunaambiwa ini hadi alipokufa tukaambiwa ukimwi. Kosa ni kwamva niliambiwa hivyo tukiwa mazishini morogoro. Niliruka na kukataa katakata haiwezekani. UNAJUA KWA NINI? Nilikuwa mjamzito mwanzo wa mwaka huo na rafiki yangu alinisindikiza kupimwa VVU nilikuwa naogopa akaamua kupima na yeye majibu yalitoka tuko salama wote. Iweje ndani ya miezi 6 apate ukimwi augue hadi kufa? Ubaya ni kwamba ukiwa seropositive taarifa zako zinaandikwa kwenye charts ili Dr akiingia aweze kuwa mwangalifu katika kukuhudumia. I was perplexed! Maana nilizisoma na haikuandikwa popote. Kwenye cheti cha kifo wakaandika HIV (?) sasa alama ya kiulizo ya nini? Hawakuwa na uhakika?

Kesi ya pili ni kifo cha mke mwenzangu alienda kujifungua wakamweka muda baadaye wakamfanyia operation wakadai alipoteza damu nyingi na pia kichanga kilikufa. Well tulimwachia mungu.

Kesi ya tatu na ya mwisho inamhusu mwanangu. Watoto ni watundu sana na huyu wa kwangu ni no exception. Nilikuwa namsuka na shanga si unajua tena mtoto wa kike. Basi akaamua siku hiyo kuweka shanga puani. Basi ilipogoma akaja kunionyesha mama yake nilihangaika kweli kuitoa bila mafanikio so nikamkimbiza kwa kairuki. Kufika kule aliingizwa theatre. Mimi na baba yake tunasubiri. Madaktari wanamtoa wakasema hawajaiona hiyo shanga. Lo!!!! Walinitambua siku hiyo. Nikawaambia what are you saying? Kwamba mimi ni mwongo???? Nimtoe mwanangu nyumbani kumleta ili mumshikeshike!!!! Je na huyo daktari aliyeandika maelezo naye ni mwongo hakuiona??? Aise nikawangangania kuwa wameisukuma ndani na wakaitoe maana siondoki bila ya kuiona shanga wameniletea mkononi. Kwa aibu wakarudi ndani theartre na kumtoa shanga na kuniletea mkononi. Naona aibu hata kuwataja hao madakyari kwa majina maana mmoja ni daktari bingwa na anaheshimika sana. Niliumia na huo ndio ukawa mwisho wangu wa kwenda pale.

Kwangu Kairuki imebakia kwenda kuona wagonjwa na hata nikienda huwa nabaki kuwashangaa sana wamepachaguaje. Wengi wao wanadai kuna ndugu daktari pale au Nesi ndio maana waneenda pale.

Kwa heri Kairuki hosp!

Mkuu mtaje daktari ili tumuepuke.

Nina case tatu kuhusu Kairuki
1. Ni mtoto kuachwa wazi baada ya kizaliwa na baridi ikamuathiri sana. Huyu alikufa few days after
2. Mtoto kizaliwa kuachwa wazi kiuzembe nae akapata matatizo bahati nzuri walimkwida misindano akaponea tunduni
3 . Unsuccessful operation ya titi iliyofanywa kwa uzembe. In fact hawakupaswa kufanya operation basing on the patient's age na case yenyewe. Ndio ilizidisha tatizo kwani hata uvimbe walio sema wanautoa hawakuutoa. Mgonjwa alihamia TMJ sijapata update za hali yake.

Wa kuu TMJ napo vipi?
 
Kama kaburi la mwanzilishi wa hospitali lipo mlangoni(reception) unategemea nini hapo???
 
Back
Top Bottom