mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,772
- 2,171
Nimerudi juzi Jumapili kutoka Kigali, Rwanda ambako nilikwenda na wenzangu 3 kwa shughuli za biashara. Tulikwenda kwa usafiri wa gari binafsi. Tulikaa huko siku 3. Nilishuhudia kitu kimoja kuhusu traffic polisi wa huko, jambo ambalo lilinifanya nitafakari na kulinganisha na traffic polisi wa huku kwetu.
Mara tu tulipovuka mpaka wa Rusumo na kuingia Rwanda, hatukuwahi kusimamishwa hata mara moja na maaskari usalama barabarani kwa kuulizwa hiki wa kile kwa siku zote tulipokuwa huko. Kila tulipowaona hawa maaskari tuliona wako mkao wa kusaidia au kuelekeza mwenendo wa magari kuliko kusimamisha na kuanza kutukagua.
Hapa kwetu traffic polisi wanapoona gari lenye usajili wa nchi za nje hiyo inakuwa sababu tosha ya kukusimamisha na kuanza kuuliza kama gari imeingia kihalali, kama lina ile "Yellow Card" au maswali mengine.
Nilimwuliza mwenyeji wetu tofauti niliyoiona kuhusu hawa traffic polisi. Mwenyeji wetu ambaye ana uzoefu mkubwa na matraffic wa kwetu alicheka na jibu lake lilikuwa hivi:" Falsafa ya maaskari usalama barabarani wa huku ni kwamba wanachukulia kwamba gari lolote lililo barabarani liko sawa na halina hitilafu yoyote. Pia wanaamini dreva wake ana leseni iliyo hai, na anaendesha aikiwa hajalewa, n.k.
Hivyo basi kwa mujibu wa falsafa hii, hawa maaskari huwa hawana utaratibu wa kukusimamisha hadi, kwa mfano waone unaendesha "recklessly" au kwa sababu yoyote ile", kuna mengi ambayo maaskari usalama barabarani wanayo ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa Rwanda.