Kuna maneno ya kiswahiki yananitatiza wanalugha nisaidieni

mbelege

Member
May 9, 2012
14
0
Wataalamu wa lugha ya kiswahili naombeni mnisaidie. Kuna baadhi ya m,aneno katika lgha ya yanapotamkwa mzungumzaji hutakiwa kuanza na ashakum, hasa kwa maneno ambayo yanaweza kudhaniwa kuwa ni matusi.(yaani mzungumzaji huanza kwa kusema ashakum si matusi), Sasa sijui ni kukua kwa lugha au ni nini kwa sababu siku hizi maneno mengi ambayo hapo mwanzo yalionekana kuwa ni ya kawaida lakini kwa yanaonekana kuwa ni matusi, hivyo naomba msaada kuwa je kuna haja ya kutumia ashakum kwa maneno kama; kuchomeka, kuingiza, kutoa,chomoa, panua, sugua, tanua,tao, chapa, gonga. Kwani maneno haya ninapoyatumia nashangaa watu hunielewa tofauti.Nisaidieni wataalamu wa kiswahili.
 
hayo maneno mbona yakawaida sana makuu na nimazuri tuu!
kama utaomba msamaha kwa hayo sema utaweka maneno gani badala yake!
 
Wewe Mbelege ninahisi umri wako ndio tatizo katika matumizi ya maneno uliyayataja. Maana ninaambiwa ninyi vijana wadogo ni mabingwa wa kubadili matumizi ya maneno ya kawaida kwa lengo la kupiga chuku hasa katika mazingira ambamo mnahisi mnahitaji faragha ya peke yenu. Sasa hayo usituulize sisi. Sana sana nikukumbushe tu kwamba hizo maana mlizozipindisha katika maneno yote uliyoyataja, hazifahamiki kwa jamii pana ya watumiaji wa lugha. Maneno hayo yasemwapo mbele ya mmilisi wa lugha awaye yote hutaona panaleta maana ya kukera.
 
kwa maneno hayo sioni ubaya wowote ila tu watu wamepanua maana na maana zipo katika fikra zao tu, wala hakuna ubaya wowote, ashakum/hashakum maana yake ni, "niwie radhi kwa nitakayosema"
 
Back
Top Bottom