HKBW
JF-Expert Member
- Aug 4, 2009
- 468
- 342
Nimejaribu kuelewa kile TCRA walichokieleza kwa waandishi wa habari na nimebakia na swali kama bado wana haja ya kuwepo au lah!
Malalamiko ya wananchi na majibu waliotoa ni tofauti kabisa. Najiuliza ni kwa nini hasa wanafanya hivi, kwakuwa wanatudharau na kujua hatuna cha kufanya. Au kuna kitu zaidi wanapata toka kwa hao watoa huduma.
Sioni namna nchi hii tunaweza kuendelea kama upatikanaji wa internet unakuwa ghari kwa wananchi wa kawaida.
Katika karne hii ya 21 kuna mtu anapanga bei kulingana na MB, halafu hapo hapo anasema quality picha imeongezeka, applokesheni zipo nyingi na spidi imeongezeka. Hili pekee ni sababu ya kuwafanya wao wawalazimishe watoa huduma kushusha bei kutokana na mahitaji kuongezeka.
Halafu wanatufanya wajinga kwa kufaninisha bei na nchi nyingine, hizi bei wanazozilinganisha ni za mobile data kitu ambacho tunapaswa kuwa tumeachananacho. Hilo ni mbali na hizo data kuwa za uongo.
Ule mkongo wa TAIFA unatunufaishaje sisi wananchi, mbona hatuoni nafuu ya kuwa nao. Ikiwa TCRA wameshindwa kuusimamia ili utunufaishe kwa kusambaza mtandao majumbani na kwenye ofisi kuna haja ya kuwa na hii mamlaka?
Mi naona kodi zetu zinapotea bure kwa watu wasiokuwa na maslahi na sisi wala taifa letu.