Kuna Dunia Ya Mayele Ambayo Huenda Hujawahi Kuisikia...

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,364
9,239
Habari Wana JF...

Najua mko poa Leo nataka kuwasimulia kidogo kuhusu mtaalamu Fistoni Kalala Mayele.... Huenda yapo mengi ambayo unayajua lakini na Mimi pia mtaandika kile ambacho huenda hukuwahi kusikia kuhusu Mayele.

Mayele alivunja rekodi nyingi huko Congo kabla hajacheza ligi kuu ya nchini hapo maarufu kama League 1..

Akiwa huku kwao Mbuji-mayi Mayele aliwahi kupiga chenga watu sita wawili waliteguka nyonga, wawili wengine walipiga magoti Kwa namna walivojaribu kumkimbiza bila mafanikio na kuishia kuchoka sana na mmoja alivunjika mguu baada ya kujaribu kumchezea rafu Kwa kumchota mtama lakini Mayele aliruka juu na mpira umbali wa futi tatu na hivo Yule mchezaji alipiga mweleka vibaya baada ya kushindwa kumnasa Mayele.. hivo Mayele alifunga goli maridadi sana ambalo hadi leo huko Congo inaaminika ndio goli Bora kuwahi kufungwa. Hilo Goli ndio lilifanya timu ya timu kubwa ya As vita kumsajili Mayele akiwa na miaka 18 Tu.


Kutokana na kua Mayele hakuwahi kucheza ligi za Chini hivo As vita hawakua na uhakika na uwezo wake wa kulicheza soka hivo Kwa kuhofia kuuziwa mbuzi kwenye gunia ilibidi apewe trial Kwanza. Siku hiyo ya majaribio alifunga goli 19 kitendo kilichofanya benchi la ufundi na baadhi ya mashabiki kushangilia sana kuanzia hapo ndo akapewa mkataba na kua mchezaji halali ya As vita.

Ana ball control ya Hali ya juu sana Mayele ana uwezo wa kutuliza mpira mitatu iliyopigwa Kwa wakati mmoja kwenda kwake.

Ana uwezo wa kupiga danadana 300 Kwa dakika moja Kwa mguu wa kushoto na danadana 425 Kwa dakika akitumia mguu wa kulia.

Aliwahi kuwafunga TP mazembe Goli la Aina yake kwani alipiga mpira kuanzia golini kwao Kule Kwa kipa wa As vita shuti Kali sana lililoenda moja Kwa moja Hadi Golini upande wa mazembe.

Mayele inasemekana siku hizi hana spidi sana kwani wakati akiwa huko Kwao mazoezini alikua anakimbizwa na pikipiki Aina ya boxer lakini alikua akiiacha hatua kumi na nane nyuma. Hata Kule south Africa beki wa Marumo Gallants hatamsahau Mayele kwani baada ya kukimbizwa Sana alikiri kweli Mayele hakua mtu wa kawaida..

Mayele ndiye mkongo wa Kwanza kufunga Goli la tiktaka (acrobatic) akiwa katikati ya uwanja kwenye ligi kuu Congo.

Mwaka huu kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi yaani ngao ya jamii Mayele aliwafunga Simba Goli mbili ambazo ziliwaduwaza na kuzima ndoto Yao ya kushinda taji hilo. Inasemekana kila wiki mafoward wa Simba hua wanaangalia zile goli na kuzifanyia mazoezi lakini hakuna aliyewahi kufanikiwa kufunga huko mazoeni hata pale golikipa alipotoka golini bado walishindwa kufunga.

Hakika huyu mwamba mi balaa

Tukutane Fainali Kwa mkapa hapo jumapili Mimi kama shabiki wa Asec Mimosas naamini huyu Mayele atatulipia kisasi.






images%20(2).jpg
 
Huu ndo uzuri wa mwanamke ukimshughulikia vizuri, atakuona kama malaika, mayele's libolo linatuharibia dada zetu.
 
Maana ya janga la kimaarifa

Mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Marekani, Baraka Obama, akihojiwa na Jeffrey Goldber, mhariri mkuu wa gazeti la “The Atlantic,” aliwaonya Wamarekani kuhusu “janga la kimaarifa,” yaani “epistemological crisis,” lililokuwa linawakabili.

Katika "soko la mawazo," hii ni changamoto ambayo hujitokeza pale ambapo jamii hupoteza “uwezo wa kutofautisha kati ya ukweli na uwongo,” alisema Obama.

Kuwepo kwa janga hili huthibitishwa na utitiri wa sentensi unganifu ambazo zimebeba kauli za kweli na kauli za uwongo,” hali ambayo huitwa “mkanganyiko,” yaani, “paradox,” “mystery,” au “contradiction,” kwa Kiingereza
 
Back
Top Bottom