Kuna baadhi ya nafsi katika siasa na serikali zinawafaa makapera

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
nape.jpg

Baadhi ya majukumu ya kikazi kwa baadhi ya wanasiasa na sekta fulanifulani za umma serikalini zinawafaa zaidi makapera kwa vile muda mwingi wako njiani na sidhani kama wana muda wa kutulia katika nyumba zao za kuishi.

Picha ninayopata kama wana familia lini watatulia katika familia zao wakati muda wote ni mizunguko tu huku na kule.
 
Mizunguko dili Mkuu; jamaa wanapiga hela hawana lingine. Hela tamu kuliko mke na familia kaka.
 
Mizunguko dili Mkuu; jamaa wanapiga hela hawana lingine. Hela tamu kuliko mke na familia kaka.

Mtu unapofikia kiwango cha kuona utamu wa maisha ni pesa badala ya familia na kutulia maishani kuna tatizo lisilo la kawaida.

Kuna mwanamke mmoja mcheza Tennis huko Marekani kutoka jimbo la Florida, alipofikisha umri karibu miaka 30 aliamua kuacha kucheza tennis kwa hoja kwamba kujaza vikombe nyumbani hakutampa furaha kama kuwa na mtoto anayecheza kando yake. Alipopata mtoto akarudi uwanjani na kushinda vikombe kadhaa.

Ukweli maisha ya kuzunguka muda mrefu hivi kuna kitu ambacho mzungukaji anaathirika kitabia hali kadhalika kimwenendo na huwa vigumu kusetirika katika maisha yake hapo baadaye. Familia ni dawa ya uwajibikaji na kusetirika.
 
Back
Top Bottom