Kumuondoa Waziri Mkuu Madarakani

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.

(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na
Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na
ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;

(c) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.

(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama-

(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi
na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;


(b) Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili
ya kuleta hoja yametimizwa.

(4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni
mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.

(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu
iwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

(6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri
Mkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha
azimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote
vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya

kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu
atatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua Mbunge mwingine kuwa
Waziri Mkuu.
 
Aksante sana mkuu kwa yuko mtu alikua anabishana mchana kweupe kwamba bunge haliwezi kumwajibisha waziri mkuu sasa wacha nimwonyeshe.
 
a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
Thanks, ila ungetuwekea na ibara ya 52 tujumuishe uhusiano wa sheria hizo
 
"taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;"

Hiki kifungu ni kuwa sikielewi au naforce kutokielewa izi siku 14 how wakati ni jana tuu wazo lmekuja na Jumatatu twataka asepe
 
Ongamushee Wagoshiii.......Nabisha wagosi nikaribie humu jamvini wandugu wagoshiii au nishikharibye?
 
Thanks, ila ungetuwekea na ibara ya 52 tujumuishe uhusiano wa sheria hizo

ibara ya 52 inadeal na majukumu ya PM kama msimamizi wa shughuli za serikali bungeni. a mere supervisor not an employer.
 
Nlikuana na mjadala mzito kuhusu hoja hii, ni kwa wakati gani na taarifa gani zitakazomridhisha Spika ya kuwa bunge halina imani na waziri mkuu na imfanye atoe taarifa kwa Raisi...walau nimepata nondo
 
(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

huyu waziri mkuu tayari kavunja masharti ya ibara ya 52 kwa kuwaruhusu bila ya kuwachukulia hatua mawaziri 5 ambao wamepatikana kwenye taarifa ya CAG kushindwa kuthibiti wizi na ubadhirifu kwenye wizara zao......
 
Back
Top Bottom