Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Wana Jamvi weekend hii nimepata kadi ya mchango ambayo sijawahi kuchangia mchango wa aina hiyo, kadi yenyewe ina heading isemayo "Mchango wa Maulidi" inaendelea kusema Bwana na Bi xxx wanaratajia kumtoa mtoto wao kipenzi mwanzoni mwa mwezi December, hivyo mimi kama rafiki, Ndugu au jamaa wa karibu wananiomba mchango wa hali na mali ili kufanikisha jambo hilo muhimu.
Kwasababu ni watu wa imani tofauti na mimi na nilifahamiana nao nikiwa nanunua Shamba huko bagamoyo, nimehisi pengine kumtoa mtoto si kitu kigeni ila ni mimi tu sifahamu na nikiwauliza wao wanaweza kuhisi nina dharau ilihali wao wameniheshimu kwa kunishirikisha jambo(Hivyo nimekubali kushiriki bila kujua 'kumtoa mtoto' ni nini). Sijajua wanamaanisha nini je wanataka kumfanyia mtoto Sendoff au Harusi? Naombeni anayefahamu mchango wa maulidi ni nini, na kumtoa mtoto ni nini anisaidie kabla sijachangia ili nifahamu uzito wa jambo lenyewe maana naamini humu wanapitia watu wa aina mbalimbali na exposure tofauti tofauti.