Kumridhisha kila mwanadamu, ndugu au watu wako wa karibu ni shughuli ambayo hata mitume walishindwa enzi na enzi

MUBIKU

JF-Expert Member
Oct 24, 2014
276
376
Kama kichwa cha habar hapo juu kinavyojieleza, sina neno la kuongeza, kifupi namshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 31 ya umri wangu, huku nikiwa nimetimiza 85% ya malengo niliyojiwekea tangu napata balehe.

Hakika Mungu ni mwema sana, hivyo ikiwa kama maadhimio ya umri huu wa miaka 31, nimeadhimia mambo 10. Moja kati ya hayo, ni kuhofia zaidi nafsi yangu na kutothubutu kufanya jambo ili kumridhisha mtu hasa ndugu, maana hao ni kati ya kundi lenye lawama mno katika jamii.

Mengi nimehifadhi kwenye diary yangu ila la muhimu nililoleta hapa JF. Ni kuwasihi wanaume wenye umri kama wangu kamwe tusije kuishi ili kuwaridhisha watu, kwani hiyo ni shughuli ambayo hata Mitume ya imani yote huko nyuma ilishindwa (failed) kufanya hivyo hadi wanakufa.

#Tunaishi mara 1, tuishi kwa furaha na amani. #2025. Malengo 10.
 
Hongera kwa kwa kufanikisha 85% ya malengo
Wengine ngoja tujitafute
 
Ni swala la muda tu ndugu , kikubwa panga malengo alafu pambania ndoto zako.
 
Back
Top Bottom