Kumi bora ya matatizo ya Tanzania

Researcher

Senior Member
Dec 15, 2010
187
48
Ndugu zangu wanajamvi.
Leo nimeguswa kutoa mawazo yangu juu ya mijadala mingi kuhusu kiini cha matatizo ya watanzania.
Yamesemwa mengi na pengine si vibaya nikayarudia kumi bora kati ya yale yaliyonigusa zaidi.

  1. Kukithiri kwa rushwa kiasi cha kupoteza usawa na haki katika utoaji wa huduma muhimu za kijamii zikiwemo afya na haki za kimahakama . vilevile rushwa imechangia kudhoofisha utoaji huduma haswa kupitia waajiriwa wasio na viwango.
  2. Mfumo mbovu wa manunuzi kukabiliwa na mianya inayoruhusu utoaji wa zabuni usio sahihi na manunuzi yasiyokidhi uhitaji na hivyo kuliingiza taifa katika hasara kubwa.
  3. Kudidimia kwa kiwango cha uwajibikaji katika ngazi mbalimbali. Ni wachache sana wanaofanywa kujutia makosa yao katika utendaji na hivyo kupungiuza hofu. Vile vile ubinafsi uliokithiri miongoni mwa wenye dhamana.Hapa kuna maswala ya epa, meremeta, Richmond n.k
  4. Kukuthiri kwa matumizi mabovu ya mali za umma kuanzia ngazi ya kitaifa hadi vitongoji. Yapo mengi katika kundi hili (serikali Dodoma na Dar, mashangingi, posho, vikao na warsha safari za nje n.k)
  5. Kukosekana uwiano katika utozaji kodi kiasi cha kuwafanya baadhi ya wafanya biashara kuumizwa zaidi na kodi hata kupelekea kushindwa kufanya biashara au kuwaumiza walaji. Wakati huo huo wengine wakikwepa kwa makusudi au kutumia mianya ya udhaifu wetu kukwepa kodi (haswa makampuni ya kigeni na katika sekta ya madini)
  6. Kukithiri kwa matukio ya kuhujumu ama kwa makusudi au uzembe mashirika ya umma na viwanda vyetu. Mfano ATCL, General tyre nk. Na vile vile kuuzwa kiholela kwa bei ya karanga kwa mashirika nyeti na rasilimali zingine kama nyumba na magari ya serikali.
  7. Kupoteza muda mwingi miongoni mwa wale waliopewa dhamana ya kusimamia maendeleo katika malumbano na migogoro isiyo na tija kwa taifa letu.Kukua kwa siasa za chuki, na kufumuka kwa sera za makundi ya kijamii (sitayataja).
  8. Kuendelea kuwepo ushirikishwaji duni wa wananchi katika mipango ya maendeleo na hivyo kusababisha kufeli kwa utekelezaji wa mipango mingi (mf. Mkukuta )
  9. Upatikanaji duni wa taarifa na uwazi miongoni mwa taasisi serikali hali inayochochea kufichika kwa madhaifu mengi, rushwa na uonevu. Mfan taarifa za utendaji , haki za mpokea huduma, wastani wa muda huduma na malipo yanayostahili kutozwa. (mfano ardhi, usajili n.k)
  10. Usimamizi duni wa mihimili ya maendeleo ya nchi haswa nishati , viwanda na rasilimali kama madini.Kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuporomoka kwa thamani ya shilingi na kuendelea kukopa kiholela.
Naamini ni yapo mengi zaidi, lakini kwa leo yangu ni hayo.
Mungu ibariki Tanzania
 
umesahau ufuska wa ma'leader wetu unaosababisha viongozi wengi wa kuteuliwa kuwa vilaza, km wakuu wa wilaya na mikoa, na wabunge vitanda maalumu.
 
Kama inawezekana, ingekuwa vizuri tungejadili na mazuri ya viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom