Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Ikulu yahusishwa kutorosha Twiga
Wingu zito bado limezingira utoroshaji wa wanyamapori hai wakiwemo Twiga kwenda Doha nchini Qatar huku baadhi ya maofisa waIkulu na wale wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakitajwa kufahamu mpango huo.
Kutajwa kwa maofisa wa Ikulu kunatokana naukweli kwamba ndege iliyotumika kutorosha wanyama hao inadaiwa kuwa ni ya Jeshi la Qatar jambo linaloibua maswali kuwa iliingiaje anga la Tanzania bila Ikulu kufahamu.
Ndege iliyobeba ni ya Qatar Emir Air Force na kwa ufahamu mdogo ni kwamba ili ndege hiyo ije nchini ni lazima kuwe na mawasiliano kati ya nchi na nchi, kilidokeza chanzo chetu.
Habari zilizofikia Mwananchi Jumapili ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa kulikuwa na mawasiliano kati ya Ikulu, ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na utawala wa kifalme wa Qatar hadi ndege hiyo kupata kibali cha kutua nchini.
Ukitazama sakata zima hili, bado kuna watu wazito hawajakamatwa ambao walishiriki ama kwa kujua au kwa kutofahamu kwa sababu si jambo la kawaida ndege ya nchi nyingine kutua nchini bila ya mawasiliano, kimedai.
Habari hizo zinadai kuwa ndege hiyo ilipewa kibali cha kutua nchini kwa kile kinachodaiwa kuwa ilikuwa imebeba familia ya kifalme, hali iliyofanya isitiliwe shaka hata ilipokuwa ikipakia wanyamapori hao Novemba mwaka jana.
Ofisa mmoja mwandamizi katika uwanja wa ndege wa KIA amedokeza kuwa yupo Afisa mmoja wa TRA aliyesaini hati kuidhinisha kupakiwa kwa wanyamapori hao lakini hadi sasa hajakamatwa.
Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro Patience Minga alikaririwa akisema ofisa anayetajwa katika nyaraka hizo alishastaafu mwaka jana hivyo TRA haizitambui nyaraka hizo na haziwezi kutambuliwa kama za mamlaka hiyo ..
Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili Uk 2.
My take:
Hili sakata bado asubuhi, kwa maoni yangu litaiyumbisha sana serikali ya CCM, hasa Ikulu. Linatarajiwa kutinga Bungeni wiki hii na yule mama mkuubungeni bila shaka anafanya rehearsal (zoezi) la kuli-punch kama ilivyo kawaida yake.