Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!

huo ndio upimbi kabisa sema akina nani kama habari yako haijakuwa tayari sasa jina unalo la nini sasa kwanini husemi unatuhabarisha nini kaaa kimyaaa kama domo zege masabuli wewe.
 
Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).

huu ndioufala nisioupenda "JINA LIPO""JINA LIMEHIFADHIWA""KAMA LIPO MBONA WENGINE USISEME YAANI WATANZANIA TUNABAKI KUWA WAJINGA NA MANENO YA KIJINGA KILA SIKU
wataje kabisa sio ina unalo halafu unakaa kimya sasa tutajua lini ,unafanya siri hata hapa,,masabuli mkubwa wewe semaaa,, wanaua watoto wetu ujue..unafiki mchezo mtoto anaaza darasa la kwanza anawaza kujifunza ngumi na kula kubeli si kwa jili ya kufundishwa na hao hao wehu
 
Jibu unalo tayari, na hapo si unaona na mabaunsa wanaojifanya ni wa mujini!!! Huyu ---- anatesa sana jamii hakika. Shule yenyewe halikusoama na fujo mitaa yote mijini Enzi za ujane wake akitesa na machangu wa grade ya juu na watoto wa watu kuchezea!! Si unakumbuka jinsi habari zake za kutishia watu na bastola zilivyokuwa ninaenea mjini? Wakati ule vyombo ya habari si vilikuwa vichache? Na vya serikali havithubutu kung'ata mtoto wa kigogo? Akimtaka demu wako unalo!! Shenzi sana hili.

Alikua ni bwana wa jack ntuyabaliwe pia..haha
 
Ahhh wapi? Bongo hata uweke nini, njaa zifanya hongo mbele. Kwani siku ile hawa mabinti wanapita mbwa si walichelewa? Baadhi ya camera zilikuwa off!!!! Na kwa nini walete technology ya kuwakamata wakati watendaji wameshatiwa mkononi hawafurukuti? unasemea Bongo tunayoifahamu au mpya? Wale wanaoishi ughaibuni nafikiri Bongo hamjajua ilivyoharibika!!!!! Ombeni duo citizenship angalao muwe mnakuja mhashuhudia kuliko kuambiwa. Vijana wetu kuanzia shule za primary hasa za bweni ni victims!!!

Bana eeh, mimi siyo mgeni Tanzania na siko nje ya mguso kiasi hicho. Naijua vyema kabisa na najua tunaweza kukabiliana vilivyo na hiyo biashara ila tatizo ni nia ya kweli hakuna.
 
Wanajukwaa mi yote hayo sifikirii, kinachonisumbua ni jinsi yule msichana nkivyokuwa namuwaza siku moja nije muonja. Aisee kafungasha balaa sijali hata kama alikuwa na tabia mbaya au nzuri, NISINGEMCHOKA

Ama kweli tuko tofauti...!
 
Na Mwandishi Wetu
IMEVUJA! Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange' na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya

kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga' Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.
Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.


MATESO SAA 24
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.

USHUHUDA
"Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
"Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
"Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
"Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung'ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
"Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.
"Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.
"Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
"Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.

WALIOWATUMA
"Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8," kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.

MTOTO WA KIGOGO ATAJWA
Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea' aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.
Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini' Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.
Gazeti hili lilipozungumza na Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.

ULINZI KAMA SHEHE PONDA
Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga' Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.

WAPANDISHWA TENA KORTINI
Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.
Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.

Inafaa wanyongwe kabisa kwani hawafai katika jamii hii.
 
Hivi huyu kinje ina maana zile pesa za pale Ubungo bus terminal. Hazikumtosha mpaka akaanza kuuza na sembe? Kweli nimeamini pesa hazitoshagi...
 
Back
Top Bottom