Kumekucha: Je, Marekani inajiandaa kuiadhibu kijeshi Syria?!

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,418
9,599
Baada ya tukio la kutumika kwa silaha za kemikali dhidi ya Raia linalodaiwa kutekelezwa na serikali ya Syria,Marekani ikiungwa na mkono na Ufaransa na Uingereza zimetoa matamko makali zote zikiunga mkono kuiadhibu kijeshi Syria kwa kitendo hicho Cha kinyama.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaa kikao Leo hii kujadili tukio hilo (la kemikali) huku kukiwa na matamshi makali Kati ya Urusi na Marekani.

Urusi imeiambia Marekani kwamba ndiye mleta vurugu nambari moja Duniani na kwamba haina Rafiki wa kweli ‘Mutant fish in murky waters’: US brings chaos to the world & has no real friends – Russia UN envoyhuku Marekani ikisema kwamba itamuadhibu 'Nduli Assad' hata Kama haitaungwa mkono na UN.US will act against ‘monster’ Assad with or without UN ‒ Haley

Rais wa Marekani Donald Trump amemtuhumu Assad kwa kutekeleza Shambulio hilo baya na kusema kwamba jibu lake linakuja hivi karibuni ndani ya masaa 24-48.Donald Trump says 'major decision' coming on Syria in next 24-48 hours

Na Sasa Kuna taarifa kwamba meli ya kivita ya Marekani yenye makombora ya Tomahawk ambayo yalitumika mwaka jana kushambulia Syria imeondoka Cyprus na kuelekea Syria.

Swali ni je, Marekani inataka tena kuishambulia Syria?!

Je,lipi litakua jibu la Urusi?!

Nini hatima ya Syria?!
 
MASWALI NINAYOJIULIZA MPAKA SASA:

Mosi,
Unahisi Marekani anaweza kupigana vita nchini Syria kirahisi wakati Uturuki hayuko upande wake ???

Pili,
Marekani kama atapigana moja kwa moja basi itabidi Israel ahusike moja kwa moja. Je, unahisi Israel atakubali kupambana na Urusi moja kwa moja wakati Waziri wake Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Avigdor Lieberman walikubaliana na Urusi kwamba hatapeleka silaha nzito Iran ambazo hazitaharibu uwiano wa nguvu kati ya mataifa hayo. Hapa inategemea sana Israel ataishije na majirani zake (Haya ndiyo makubaliano). Je, Israeli hatakuwa anahatarisha Usalama wake ???

Tatu,
Wakivamia nchini Syria bila ruhusa ya Umoja wa Mataifa unadhani Ulaya kutakuwa salama dhidi ya mashambulizi ya Ugaidi hasa hasa kipindi hiki kuna wakimbizi wengi kutoka Syria barani Ulaya ???

Nne,
Kutokana na swali la tatu hapo juu,
Je, unadhani Ulaya (Continental Europe) watakubali kushirikiana na Marekani katika Umoja wao ilhali wakijua dhahiri madhara yatakayotokea nchi kwao endapo watashirikiana na Marekani kuvamia Syria ???

Tano,
Kama Marekani taifa lililo kubwa hapa duniani limedharau Umoja wa Mataifa na kuvamia Syria kwa mwamvuli wa kutoa msaada wa kibinadamu (Humanitarian Intervention) unadhani Mataifa mengine hayatawiwa kufanya hivyo kweli ?
Maana Adolf Hitler aliwahi kuvamia Czechslovakia mwaka 1939 akisema anaenda kutoa msaada wa kibinadamu (Humanitarian Intervention) kama ambavyo Marekani anajitanabaisha leo.

Sasa hebu tuyaangalie haya mambo kwa mapana,
Kama Marekani atafanya hivi huko nchini Syria bila kuheshimu Sheria za Kimataifa.
Unadhani nini kitamzuia Urusi asivamie nchi ya Ukraine kwa mwamvuli huo huo wa kutaka kufanya msaada wa kibinadamu (Humanitarian Intervention) hasa kwa Warusi wanaoishi nchi Ukraine ??? Hapa usiseme atashindwa maana alivamia mwaka 2014 na dunia nzima haikufanya kitu chochote kijeshi kwasababu ya kuepusha vita.
Mfano wa pili unadhani nini kitamzuia nchi kama Uchina Kuvamia Taiwan kwa mgongo huo huo wa msaada wa kibinadamu (Humanitarian Intervention) ???

Mwisho kabisa,
Unadhani Marekani anaweza kuhatarisha Usalama wake na dunia nzima na kusababisha vita ya dunia kisa tu Syria ???
Unakumbuka Professor James Steinberg, Joseph Nye na wenzao walipotumwa nchini Uchina kwenye Wizara ya Ulinzi ya Uchina mwaka 2012 walisemaje kuhusiana na Ugomvi wa Uchina na Japan kuhusiana na visiwa vya Senkanku ???
(Basi ukisoma ambacho hawa watu waliowahi kufanya kazi kwenye vyombo vya Ulinzi vya Marekani kama maafisa waandamizi unaweza kuelewa kabisa Saikolojia ya Marekani ikoje kwa sasa kuhusiana na kupigana Vita)

NB: Jana The Red Crescent wametoa habari za kitafiti kwamba wale watoto walioshambuliwa Idlib walipimwa na madaktari lakini hawakukutwa na kemikali ya Chlorine ambayo Rex Tillerson na The White Helmets walidai imetumika. Hivyo kama Shirika la Kimataifa linaloaminika na Umoja wa Mataifa limesema kwamba hakukuwa na Shambulio la kikemikali mwezi Februari. Je, tuamini kwamba kuna shambulio la Kemikali huko Douma bila uchunguzi wowote ule ??

CC: Bilionea Asigwa (Baadhi ya maswali nshapatia majibu tayari)
 
I told you many times: Marekani ikitaka kukumaliza hakuna wa kukusaidia, now watch kitu Asaad atafanyiwa, total destruction ya Syria Army using War ships & War planes kisha Asaad atamalizwa like Gaddafi au Saddam.. Just few days mtaona, nimeona Trump kachukia sana sanaaa sanaaa jana, na kasema wazi Asaad atajuta
 
I told you many times: Marekani ikitaka kukumaliza hakuna wa kukusaidia, now watch kitu Asaad atafanyiwa, total destruction ya Syria Army using War ships & War planes kisha Asaad atamalizwa like Gaddafi au Saddam.. Just few days mtaona, nimeona Trump kachukia sana sanaaa sanaaa jana, na kasema wazi Asaad atajuta
....kumbuka kuna russia na iran sio habari ndogo hiyo
 
I told you many times: Marekani ikitaka kukumaliza hakuna wa kukusaidia, now watch kitu Asaad atafanyiwa, total destruction ya Syria Army using War ships & War planes kisha Asaad atamalizwa like Gaddafi au Saddam.. Just few days mtaona, nimeona Trump kachukia sana sanaaa sanaaa jana, na kasema wazi Asaad atajuta

Unahisi Marekani anaweza kufanya anachotaka kwa kipindi kama hiki bila kupata madhara yoyote yale ???
 
Ni ukweri usiopingika Marekan ndo muleta vulugu Duniani,lakini pamoja na hayo kama Syria itashambuliwa kijejeshi dola ya kiisilamu ya Irani ijiandae kudondoshwa,Kwa mara ya kwanza katika sakata la Syria Uingereza,Ufaransa,Ujeruman,mataifa makubwa barani Ulaya na yenye Nguvu za Kiuchumi yamekubari kuungana na Marekani,Kwa vyovyote vile Urusi hawezi kutoboa hata siku moja,
 
kulitokea mauaji ya kimbari dhidi ya wahutu na watutsi hatukusikia haya...wao wanatetea utu gani?
Mmarekani mbaya hilo bomu la kemikali kalipiga yeye ili apate sapoti baraza la usalama.Kama kweli wao wanaumia mbona Yemen na Palestina watu wanakufa kama kuku lkn wamekaa kimya au kwa kuwa Israel na Saudi ni washirika wake.Marekani ndio TAIFA AMBALO LINFANYA DUNIA ISIONEKANE SEHEMU SALAMA,sababu tu analinda maslai yake na hajali usalama wa wenzake.
 
Back
Top Bottom