Kumbe Wabunge Wote Pale Bungeni Ni Watoto Wa Mjini?

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Nimekuja kuona na kutafakari kwa kina sana kuhusiana na wabunge wetu wooote pale bungeni kumbe ni watoto wa mjini, nasema ni watoto wa mjini nikiwa na maana ni watu ambao wameishi mijini na biashara zao zote ziko mijini na sio vijijini. ukifika wakati wa uchaguzi ndio utawaona waheshimiwa hawa wakienda vijijini kuomba kura na kutoa ahadi lukuki kwa wanavijiji hao kuwa watawaletea maendeleo.

Sasa nini ushauri wangu kwa waheshimiwa viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kumkomboa mwanakijiji huyu ili aondokena na umasikini uliokidhiri, ni kwamba ni kwanini wabunge wa viti maalumu woote kwanini wasitoke vijijini kwakua wao ndio wenye kuelewa maisha ya huko vijijini kuliko kuteua wabunge wa viti maalum wote kutoka mjini? huu nimtazamo wangu tu kwakua wabunge wote pale mjengoni ni watoto wa mjini hapa ni mtazamo wangu tu. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom