Kumbe ujuzi wa kilimo tunao sasa kwa nini tuliyoyaona nanenane shambani kwa wakulima hayapo?

kituro

Senior Member
Dec 25, 2010
176
15
Nanenane mambo yalikuwa mazuri lakini mbona kwa wakulima hayapo?


attachment.php
 

Attachments

  • DSC05880.JPG
    DSC05880.JPG
    797.2 KB · Views: 269
ni kweli mdau muda na gharama nyingi zimetumika kuonyesha maonyesho ya 88 lakini hakuna implementation yoyote huko mashambani.
Nanenane mambo yalikuwa mazuri lakini mbona kwa wakulima hayapo?
 
bongo bana.
rais anatumia mamilioni kwenda kuomba msaada ambao ni pungufu ya alizotumia.
usishangae mkuu
 
Inawezekana ila wasomi hata wale waliosomea kilimo hawataki kulima. Wanataka kazi za maofisini. Wakulima wa vijijini hawana elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha kisasa. Gharama nacho ni kizuizi kikubwa. Ili kuotesha bustani kama hiyo hapo juu unahitaji mbegu bora, madawa ya kuua wadudu, mbolea na maji ya kumwagilia. Mkulima mdogo wa kijijini hana mtaji huo. Halafu akipeleka mazao yake sokoni bei anayoikuta haiwezi kurudisha gharama zake. Kilimo cha mkulima mdogo Tanzania kinachukuliwa kama hobby na siyo biashara. Lakini mkulima mwenyewe anayo akili na uzoefu wa kujua kuwa kilimo haklilipi. Serikali yetu inatambua kilimo cha wawekezaji (wapora ardhi) lakini inadiliki kumlazimisha mkulima mdogo mzalendo kuiuza mazao yake kwa bei ya hasara. Kilimo Kwanza ati.
 
Uvivu pia unachangia hapa. Mtu yeyote mwenye bidii na nia anaweza kufanya bustani ya mboga mboga na kuuza kwa beii nzuri kumwendeshea maisha. Lakini kila mmoja wetu ni bingwa wa siasa na maneno meeeeengi. vitendo = sufuri.
 
Back
Top Bottom