Kumbe uchawi upo! Soma hii toka kwenye blog ya mwanamke nyumba

yaani hata hiyo thread ni ndefu siiwezi kuisoma yote...ila uchawi haupo?

Mi si mlokole kiviiiiiiiiile kwani natendaga dhambi na tafsiri ya wenzetu walokole eti hawatendi dhambi kabisa hata kama wanatenda kwa kujificha. Dawa ya uchawi ni kuukataa kwa nguvu zote usiuendekeze wala kuuamini jua tu upo, ila kwa upande wako jitahidi kukemea kwa nguvu zote. Ukishaanza kuuogopa tu jua unalo
 
anatakiwa awajibishwe yule alietoa vitisho..jamaa aweke issue wazi..watu waelewe ili aonywe....dah wanaume kumbe ni wachache sana...wanawake wanalizimisha kuolewa.
 
Dah kwa kweli hapa hakuna ustaarabu uliotendeka....wamemlazimisha bi harusi aingie ukumbini ili wapige menu.....sema bwana harusi nae kachemsha kulikuwa hakuna haja ya kuconfess mbele ya hadhara yote hiyo labda kama ni bongo movie ingependeza.

Baba Sharon, ukitaka toba ya kweli unatakiwa kukiri kwa dhati, na haijalishi uko wapi.
Jamaa kateleza kidogo na katambua kosa lake na kukiri, kilichobaki ni maombi tu. Hakuna kimshindacho Mwenyezi Mungu, hakuna mwenye maarifa zaidi kumshinda yeye.
 
Oooh! maskini bint wawatu inshallah mwenyezi mungu atamuondolea kila maradhi na husda afurahie harusi yake..
 
huyu bwana alitakiwa kumwacha yule mwanamke wa pembeni kwa staili tofauti hakukuwa na sababu ya kumeleza na inawezekana alimshirikisha kila hatua.. kwa maana hiyo huyo mwanamke leo hii tutamuona mbaya lakini inawezekana alikuwa anamtawala au anaaminiwa sana na huyo mwanaume kiasi kwamba alikuwa kama msiri wake ..
huyo bwana anatakiwa akaongee na yule mwanamke akiwa na ujumbe ili kulimaliza hili suala
 
sasa mkuu sijakuelewa,ndoa ilifungwa?nini kiliendelea au ni hadithi tu?na kwa nini bwana harusi alikuwa analia?au ndio uchawi wenyewe?
 
Sasa uchawi ni kuumwa siku ya sendoff au?
Mi nafikiri aliipania sana siku ile akawa affected kiakili. Hata kwenye mitihani na interview inatokea.
Kama uchawi upo hata sendoff yenyewe isingefanyika
huyo dada wa mpango wa kando alikua anapiga mkwara tu
 
Duu haya mambo yapo kabisa na masister dooo wa siku hizi ndio zao cjui nani kawafundisha ..ila cha msingi bora jamaa hajadatishwa maana wengine wanafanya kanisani mtu unapagawa ..Dawa ni Yesu tuu na kuacha uzinzi
 
nini ngumu kueleweka?

acheni kumshambulia TB bana,
flow ya story iko sawa ila maelezo ya mwisho hayaeleweki ...
huyo dada alijua anaumwa kawaida tu au alijua ni nani amemroga??
what was the response/reaction ya mumewe baada ya kuambiwa hivyo na mkewe (mme akiwa anajua the whole picture)
kifupi .... mwisho wake ulikuwa ni nini??
 
mwisho ilikuaje sasa,mbona mmetuacha njia panda,how ever mie siamini km uchawi upo,kama upo nawaruhusu mniloge nishindwe kuiona JF lol....
 
Back
Top Bottom