Elections 2010 KUMBE POLISI WANAMDAI JK bilioni 4?

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Waraka wa kudai Sh 4 bilioni wasambazwa

Monday, 25 October 2010
Mwananchi

Mwandishi Wetu, Mwanza


WARAKA unaodaiwa ni wa polisi wa kawaida umepatikana jijini hapa ukiihoji serikali ya awamu ya nne ni lini itawalipa mafao yao mbalimbali yanayofikia Sh 4 bilioni kama ilivyoahidi kuwalipa kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu.

Katika waraka huo askari hao wanaiomba serikali kutimiza ahadi yao ya kulipwa madai yao mbalimbali ambayo walisema kwa nchi nzima yanafikia Sh 4 bilioni.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Simon Sirro alipoulizwa kuuona waraka huo na kuyatambua madai hayo, alisema hajauona na kwamba ofisi yake haijapokea madai yoyote.


Sirro alisema hajawahi kuyasikia na kwamba kila mara amekuwa akifanya vikao mbalimbali na kuzungumza na askari wake, lakini hakuna ambaye amewahi kuelezea madai yake.


"Wanatambua utaratibu wa kudai, na sidhani kama wanaweza kulalamika katika vyombo vya habari, ndiyo maana ninakwambia jambo hilo nalisikia kwako. Nimefanya nao vikao na kuzungumza nao sana askari wangu lakini sijawahi kuona mtu akilalamika," alieleza kamanda Sirro.


Hata hivyo kuenea kwa waraka huo kunadaiwa kuzua mambo jijini Mwanza ambapo inaelezwa kwamba polisi katika eneo la Mabatini walifikia hatua ya kuhoji kwa viongozi wao kuwa ni lini wanatarajiwa kulipwa madai yao ambayo waliahidiwa kulipwa kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu.


Ilielezwa kwamba viongozi walishindwa kujibu jambo ambalo walilazimika kuwasiliana na mhasibu wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kujua iwapo fedha za madeni kwa askari hao zimewasili mkoani humo.


Ilifafanuliwa kwamba mhasibu aliwajibu kwamba fedha hazijafika jambo ambalo wengi wanadaiwa kutoamini.


Ukifafanua zaidi waraka huo ulisema uamuzi wao wa kudai maslahi yao usichukuliwe ni wa kiasiasa na kufafanua kwamba wameamua kudai wakati huu baada ya kuona muda walioahidiwa kwamba watalipwa kabla ya uchaguzi umefika na ukielekea kumalizika bila ya wao kuanza kulipwa.
 
Kiongozi wa POLISI lazima apinge kuuona waraka huo.............. Hana kingine cha kufanya zaidi ya hicho
 
polis nao wazushi sana na huwa hawana msimamo hawachelewi kulowanisha
 
Labda watie mgomo baridi siku ya kura wasitekeleze amri ya kuchakachua kura na wasipige wananchi
 
Nasikia, Wameapa hawatowapiga mabomu wananchi watakao fanya vulugu kwa madai kuwa wamechoka kuutumiwa kuwapiga Watanzani wenzao wanaodai haki zao wakati nao wanastaili kufanya kama wanaodai.
 
Polisi wasiwe na wasiwasi watalipwa pamoja na wazee wa east africa community dr. Slaa atakapoingia madarakani
 
Leo nimesikia kwenye habari kuwa Chuo cha Kijeshi Monduli kimefungwa ghafula kwa hofu kwamba watapigia chadema kura. Je, wanajeshi wengine msimamo wao ni wazi kiasi hicho?
 
sidhani kama kuna polisi yupo sisiem labda wale wakubwa..! lakini wadogo ...mie nakanao jirani ...wengine ni chadema..!

kama huamini nenda pale POLISI JAMII kurasini kwenye bia za chee ujionee wakilewa..!
 
Back
Top Bottom