Kumbe mtukula bado ipo Uganda

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209
Idd Amini Dada alipopigana na Tanzania lengo lake ilikuwa kuchukua kipande cha ardhi toka Tanzania, yaani eneo lote toka mto kagera (pale Kyaka) hadi Mtukula. Leo nashawishika kusema alifanikiwa, na hadi sasa eneo hilo bado lipo Uganda.

USHAHIDI: Kwa sasa mtu huwezi kununua kilo hamsini za mchele pale Bukoba mjini na kuzipeleka Mtukula - Tanzania. Polisi, kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya watakunyang'anya kwa madai kuwa 'unapeleka chakula Uganda'.

Ni ajabu ambayo sitakaa niisahau, hivi ni kwa nini kama kweli nia ni kuzuia uvushaji, barriers zao zisiwe Mtukula badala ya huku ndani kabisa ya Tanzania -Kyaka?

Hawaoni kuwazuia watanzania wa Bunazi hadi Mtukula ku-enjoy what is rightful to Tanzanian ni kuwabagua?

Naomba mwongozo.
 
Kwahiyo unataka kusema maeneo ya Bunazi. Igayaza, Minziro, Byamtemba, Kagera Sugar, Mtukula na maeneo mengine yaliyo upande wa pili wa mto kagera, hawaruhusiwi kununua chakula na kuvuka nacho pale kwenye daraja au pale custome. Pole kwao. Au kwa vile wanaitwa waganda kyaka wakafikiri kuwa ni waganda. Wao ni watanzania ila tu wanajua kiganda ambayo ni lugha inayotumiwa uganda. Nadhani mtatakiwa kufuatilia kwenye vyombo husika ili walitolee maelezo kama ndivyo.
 
Kama ndivyo watu wa minziro,kakindo, itala, mibembe, gabulanga, kashambya, bunazi, kagera .b., kabweera,kilimilile, nshunga, ....ni waanga!
 
Kwahiyo unataka kusema maeneo ya Bunazi. Igayaza, Minziro, Byamtemba, Kagera Sugar, Mtukula na maeneo mengine yaliyo upande wa pili wa mto kagera, hawaruhusiwi kununua chakula na kuvuka nacho pale kwenye daraja au pale custome. Pole kwao. Au kwa vile wanaitwa waganda kyaka wakafikiri kuwa ni waganda. Wao ni watanzania ila tu wanajua kiganda ambayo ni lugha inayotumiwa uganda. Nadhani mtatakiwa kufuatilia kwenye vyombo husika ili walitolee maelezo kama ndivyo.
iwapo Mkuu wa Wilaya yao amaamini ni waganda, vyombo gani husika vya kutatua hilo?
 
Mie naona tukabidhi rasmi eneo hilo kwa Museven kwa kuwa hao watu hawana msaada kwa Tanzania. Kazi yao kuuza kahawa na chakula cha mage do Uganda
 
mimi nashangaa vizuizi vimewekwa pale kyaka.yaani ukifika kyaka kama mgeni utajua ndo unaingia Uganda.mimi nafikili wale wanajeshi na polisi pale kyaka ni kwa ajili ya usalama wa lile daraja na watu wa maeneo yale.hiyo ya kukamata bidhaa ni mengineyo.wanasema kila mtu hula ofisini kwake so watu wamebuni njia halamu za kujiongezea kipato.cha ajabu zaidi watu wa mtukula wananunua sukari kg1 kwa tsh3000/-.
 
Mie naona tukabidhi rasmi eneo hilo kwa Museven kwa kuwa hao watu hawana msaada kwa Tanzania. Kazi yao kuuza kahawa na chakula cha mage do Uganda
wale ni wajanja hawawezi kuuza mazao yao kwa MATAPELI wa nji hii ni bora wahesabike wako kwa M7 kabidhi eneo kwa mwenyewe ili wananchi waneemeke!!!!!!
 
Back
Top Bottom