Kumbe kumwaga chini mbegu ya uzazi, ni kosa kubwa sawa na kuua!

Beesmom

JF-Expert Member
May 30, 2016
17,221
28,667
Ni kitabu cha Mwanzo 38:6-10 neno linasema hivi:

6. Baadaye Yuda alimwoza mtoto wake wa kwanza Eri, kwa mwanamke aitwaye Tamari.

7. Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; hivyo Mwenyezi-Mungu akamuua.

8. Basi, Yuda akamwambia Onani, “Mchukue mke wa ndugu yako marehemu, kwani ndivyo inavyokupasa kufanya, upate kumzalia nduguyo watoto.”

9. Lakini Onani alijua kwamba hao watoto wasingekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na mke wa nduguye, alimwaga chini mbegu ya uzazi, asije akampatia nduguye watoto.

10. Tendo hilo likamwudhi Mwenyezi-Mungu, akamuua Onani pia.

😳Kumwagia nje hizo mbegu kumbe ni chukizo mbele ya Mwenyezi Mungu wajameni?🤦
 
Back
Top Bottom