Kumbe haikuwa Entanglement? Jada Smith aweka Wazi kulitengana na Will Smith tokea 2016

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,622
IMG_7394.jpeg
Akiongea na Jarida la People, Mwigizaji Jada Pinkett Smith ameweka wazi kuwa huu ni Mwaka wa 7 tangu atengane na Mumewe, Mwigizaji na Mwanamuziki Will Smith, waliyeoana tangu Mwaka 1997, ambapo kila mtu amekuwa akiishi Maisha yake tokea Mwaka 2016

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Kutalikiana Jada Pinkett Smith alisema kuwa ingawa amefikiria talaka halali kutoka kwa Will Smith, hajawahi kufikia muafaka. Amesema, "Nilitoa ahadi kwamba kamwe hakutakuwa na sababu ya sisi kupeana talaka"

Ikumbukwe kuwa Julai 10, 2020 katika Kipindi cha "Red Table Talk" Jada alithibitisha kuwahi kuwa na uhusiano wa Kimapenzi na Mwanamuziki August Alsina, aliouita #Entanglement wakati ambao anadai alikuwa ametengana na Will Smith. Hata hivyo Will Smith hajawahi kunukuliwa akithibitisha kutengana au Kuachana na Mkewe

Je, ungepewa nafasi, ungemshauri nini Will Smith?
 
Hapa nawaza kuhusu HOV na QUEEN BEE!!

Nao wasije kuwa wanaishi ishI tu

Ndoa ngumu sana siku hizi.

Halafu nani kaona video za katoto ka Jay-Z kale ka BLUE IVY aisee kamekuwa kakubwa halafu kazuri.

Daaah!!
 
Maisha majumbani mwa watu kuna mengi sana, na wengi wanaishi hivyo sema tu ndio hivyo hawasemi.
Laiti kama kila mmoja angehadithia yanayojiri nyumbani kwake pasingetosha, na maana ya watu kuishi pamoja ingeondoka.
 
View attachment 2779060

Akiongea na Jarida la People, Mwigizaji Jada Pinkett Smith ameweka wazi kuwa huu ni Mwaka wa 7 tangu atengane na Mumewe, Mwigizaji na Mwanamuziki Will Smith, waliyeoana tangu Mwaka 1997, ambapo kila mtu amekuwa akiishi Maisha yake tokea Mwaka 2016

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Kutalikiana Jada Pinkett Smith alisema kuwa ingawa amefikiria talaka halali kutoka kwa Will Smith, hajawahi kufikia muafaka. Amesema, "Nilitoa ahadi kwamba kamwe hakutakuwa na sababu ya sisi kupeana talaka"

Ikumbukwe kuwa Julai 10, 2020 katika Kipindi cha "Red Table Talk" Jada alithibitisha kuwahi kuwa na uhusiano wa Kimapenzi na Mwanamuziki August Alsina, aliouita #Entanglement wakati ambao anadai alikuwa ametengana na Will Smith. Hata hivyo Will Smith hajawahi kunukuliwa akithibitisha kutengana au Kuachana na Mkewe

Je, ungepewa nafasi, ungemshauri nini Will Smith?
Sister huyu mzinguaji sasa aisee.
 
Back
Top Bottom