Kulikoni Tanzania ku-export zaidi kwenda Uarabuni kuanzia mwaka wa fedha 2021/22?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Tangu mwaka 2017 tumekuwa tuki-export bidhaa zetu kwenda South Africa na India zaidi ambapo ilikuwa zaidi ya 10% ya exports zilienda katika nchi hizo. Huku nchi za falme za kiarabu zikipata chini ya 10. Kwa mwaka 2017 asilimia ya exports zilizoenda UAE zilikuwa 2.5 na mwaka 2018 ilikuwa 2.3, kuanzia mwaka 2019 zilianza kupanda na hadi kufikia 2021 zilifikia 16.5% ambayo ni nchi inayopokea exports nyingi kutoka Tanzania.

Kwenye masuala ya kuingiza bidhaa nchini, bado Tanzania inaingiza bidhaa nyingi kutoka China, hata hivyo nchi za uarabuni zimeshika nafasi ya pili ambayo ni tofauti na miaka ya nyuma ambayo nchi ya pili kutuletea bidhaa ilikuwa India. Yaani Tanzania ilikuwa ina-import zaidi kutoka China na India, lakini kuanzia mwaka 2020 tuna-import zaidi kutoka China na UAE.

Data hizi ni kwa mujibu wa Annual Report ya Benki Kuu ya Tanzania
 
Back
Top Bottom