Kulikoni Mrema, Lipumba na Mbowe!?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Hivi kambi ya upinzani imekumbwa na nini? maana viongozi wanaotegemewa kuipeleka puta CCM mwakani katika kinyanganyilo cha urais, wote wanatarajiwa kugombea ubunge.

Viongozi hao ni mwenyekiti wa TLP mh Mrema, Mwenyekiti wa CUF Prof Lipumba na mwenyekiti wa CHADEMA Mh Mbowe,

Najiuliza ni nani sasa atapambana na Kikwete? au wameona kuwa kikwete ni ngangali? wakati sivyo,
 
Wanawapisha wengine nao waonyeshe uwezo kwenye ngazi hizo wakati wao wakirudi nyuma kujihakikishia uwakilishi wa wananchi katika bunge. Ni dhahiri wamegundua wananchi wanahitaji zaidi kuona impact ya wapinzani hasa bungeni kabla ya kuwapa dhamana ya kuongoza nchi.

Nitumie fursa hii kuwataka magwiji wote wa upinzani basi turudi majimbono na kila mmoja ajizatiti kuingia Dodoma. Ni kwa kuongeza idadi bungeni na kuwa na uwezo wa kuinfluence decisions bungeni ndipo wananchi watatuamini na kutupa dhamana ya kuongoza nchi.

Bila hivyo. hatma ya upinzani itaishia mwembe yanga, jangwani na kiraracha

Yetu macho
 
Namuomba na rafiki yetu Mtikila na yeye ajiunge nao.
 
Lipumba katangaza lini kuwa atagombea ubunge?Kama ni kweli mimi naona ni habari njema sana.Yanini kuhangaika na urais ambao inajulikana wazi kuwa Kikwete atashinda?
 
Lipumba katangaza lini kuwa atagombea ubunge?Kama ni kweli mimi naona ni habari njema sana.Yanini kuhangaika na urais ambao inajulikana wazi kuwa Kikwete atashinda?
we ukiona thread imewekwa na kaitaba (mimi) haina haja ya kutafuta source au kuwa na mashaka, elewa kuwa ni ukweli mtupu.
 
Nimeipenda sana hiyo ya kugombea ubunge ambao wana asilimia 90 ya kushinda.
Lakini pia hao uliowataja ni wenyeviti, yawezekana kuna watu wengine ambao watagombea!
 
Tufanye ubunge kuwa kipima joto cha kukubalika kwao, yeyeyote kati yao atakayeshindwa ubunge au kupata kura chini ya asilimia 60 ya kura zote za ubunge jimboni mwake akae pembeni kwenye uongozi wa chama awaachie wanaokubalika! Lazima watanzania tuwe na utamaduni wa kujipima kukubalika kwetu sio kulewa na siasa za kuwa mgombea pekee wa nafasi ya uwenyekiti!
 
move nzuri wakipata wabunge wa kutosha say 30% kutoka upinzani alafu ukijumlisha na radicals wa CCM, bunge linaweza kuwa na 40-45%ya wabunge mavchachari ambao angalau wanaweza kufanya maamuzi ya maana
 
Lakini wamechelewa, ilitakiwa siku za nyuma walipokuwa wanahangaika na urais
 
Najiuliza ni nani sasa atapambana na Kikwete? au wameona kuwa kikwete ni ngangali? wakati sivyo,
Ngangari ni neno wanalotumia CUF. CCM wanatumia Ngunguri! Zaidi kwa 2010 ni JK, hivyo ni bora waende kutafuta majimbo!
 
imagine bungeni kuna MREMA,MBOWE,SLAA,LIPUMBA,KAFULILA,ZITTO,MTIKILA,TUNDU LISSU,MVUNGI,MNYIKA,NADHANI INAWEZA KURUDI ENZI YA LILE BUNGE LA BAADA YA UCHAGUZI WA 1995, NI MTAZAMO TU
 
Back
Top Bottom