KUKU WA KIENYEJI vs KUKU WA KISASA

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,194
Wapenzi wa JF, kwa muda mrefu wakati nikiwa nyumbani Tz nimekuwa nikisikia na kuona watu wengi wakipendelea kula nyama ya kuku wa kienyeji. Hata katika maeneo yale tunayokamata moja baridi moja moto, bei ya kuku wa kienyeji huwa kubwa kuliko ya kuku wa kisasa. Nilishawahi kusikia watu wakisema wanaogopa kula kuku wa kisasa kwani wanaume wanahofia kuota matiti na akina mama wanahofia kuota ndevu. Ukweli wa jambo hili siujui ingawa nimekuwa nikichukua tahadhari ya kutotumia nyama ya hao kuku wa kisasa.

Tatizo linalonikabili kwa sasa ni kwamba niko ughaibuni. Huku wale kuku wanaotafuta mende, funza na panzi mitaani hawapo kabisaaa. Na wala ukisema kuku wa kienyeji ni msamiati ambao ni mgumu kwa wenyeji wa hapa kuufahamu. Kuku wote waliopo ni wale wa kisasa. Nyama ya kuku ndiyo kitoweo kinachopatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu. Jamani mwenye uhakika wa madhara ya hawa kuku wa kisasa aniambie maana naogopa kurudi Tz nikiwa nimeota matiti!! Wakati huo huo ndiyo kitoweo ambacho gharama yake ni ndogo na kinaweza kunisaidia ku-save vi-dola kidogo kwa ajili ya matumizi ya ndugu na jamaa huko Tz.
 
kuku wa ulaya hawawezi kukuuotesha matiti,we tafuna tu ukiota matiti washtaki utalipwa uongezee kwenye vidola unasave
 
ulaya ipi unakaa?mbona kuku wa kienyeji wanapatikana..?ingia maduka ya wahindi/wapakistan ulizia 'hard chicken' utapewa?
 
Tehteh leo umenifurahisha unaposema wa kisasa unakosea mkuu. Hata wa kienyeji anaweza kuwa wa kisasa(wasikuhizi) mie naita kuku wa kienyeji na wale kwetu tumezoea kuita kuku wa kizungu na waita, kuku "matahira" wapowapo tu hawakimbii imenenepeana wazungu wao ndio kabisa wanawachoma sindano.
 
Au nenda maduka pia ya afro Caribbean au ya west african zile nadhani jina ni pluvera (kama nimekosea sipo mbali hata ukilitamka hivi) ndio watamu zaidi kampuni hiyo ni namba 1, zinapatikana kuku mzima kwa weight imepakiwa na kunyolewa kabisa. Na pia vipaketi vya vibawa au miguu. Enjoy uliza utaelekezwa na hata hao wenyeji.
 
Mkuu kuku wa kisasa anaefugwa ulaya hana shida kwani hawachakachui kama wanaofungwa huku kwetu...wafugaji wanawalisha madawa ili wakue haraka lakini mwisho wa siku zile kemikali zina madhara kwa binadamu.
wenzetu wapo makini sana linapokuja suala la afya.
 
Niko Trondheim Norway. Unaweza ukaniletea hao kuku wa kinyeji mpaka huku???

Mkuu hebu jaribu kununua høne kylling uone tofauti yake na hao wengine. Lakini pia kwenye English speaking countries nimekutana wako kuku wanaoitwa "Free range chicken" au "Organic chicken" hawa wanaaminika ni sawa na wa kienyeji! Maana wanajiokotea wenyewe chakula na hawafanyiwi de-beaking!!
 
Back
Top Bottom