blackpepper
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 381
- 16
wakenya ni Wasanii...this time tumewashtukia ina maana wanyama havuki barabara ya Lami??
Hawa wakenya siyo wenzetu kabisa, mimi nimekuwa nalifahamu hilo tangu mwaka 1977, ndiyo maana sikubaliani kabisa na huu upuuzi wa shirikisha. Juzi juzi hapa jamaa mmja kaandika kuwa Tanzania haina barabara ni chafu; tukitaka kujenga wanakuwa wa kwanza kupiga kelel tusijenge. Ngoja tuone kama serikali ya CCM itakubaliana nao, ni hapa ninapoanza kufikiria kuwa na kiongozi kama Lowasa ( minus tamaa ya mali).
Wote mnaokubaliana na madai ya kenya mnakosea kwa sababu kadhaa, nitajaribu kusema chache hapa chini.
(1) Sehemu kubwa ya mbuga ya Serengeti iko Tanzania, ni sehemu ndogo sana iliyoko upande wa Kenya ambako inaitwa Masai Mara. Kwa hiyo kufuatia mzunguko wa wanyama, ni wachache sana wanaokatisha mpaka baina ya nchi hizo. Wengi wao wanaishi Tanzania; hebu angalia ramani hii hapa.
(2) Barabara kupita kwenye mbuga za wanyama siyo jambo la ajabu kabisa; kuna mbuga nyingi ambamo barabara zinapita na wala wanyama hawajawahi kuhama. Mifano ni kama ifuatavyo:
a) Hapo Serengeti kuna barabara inayotoka Arusha kwende Mugumu kupitia humo humo Serengeti. Barabara hii ndiyo ambayo serikali inataka kuwekea lami; ni barabara ya siku nyingi sasa, na kwa miaka nenda rudi ilikuwa inatumiwa na maloli ya mzigo kusafirisha biadhaa katia ya Musoma na Arusha, Tanga na DSM. Kwa miaka yote hiyo barabara hiyo imekuwa inatumika huku ikitimua vumbi sana wakati wa kiangazi na wakati wa masika kujaa matope yanayoweza kukwamisha magari na kuhatarisha maisha ya abiria. Ubovu wa barabara hii ndio uliosababisha raia wa Tanzania wakawa wanaamua kupitia Kenya kutoka Arusha kwenda Musoma au Mwanza.
(b) Vile vile kutoka Mto Wambu kuna barabara nyingine inayopita hapo hapo Serengeti kwenda hadi Lamadi; hii nayo ni kama ile inayokwenda Mugumu.
(c) Barabara ya Bunda Musoma karibu na Lamadi ndiyo mpaka wa mbuga za Serengeti, lakini wanyama wale hutembea sehemu zote za barabara kwenda ziwani na kila ukiipta saa za jioni utakutana nao mbona hawajahama eneo lile.
(d) Huko Kenya kwenyewe, ile highway inayotoka Mombasa kweda Nairobi inapita katikati ya mbuga za Tsavo. Vile vile ile reli inayotoka Mombasa nayo inapita hapo hapo Tsavo; na barabara inayotoka Moshi kwenda Taveta nayo inapita katikati ya mbuga ya Tsavo.. Mbona wanyama wa Tsavo hawajahama.
(e) Kwa upande wa kusini mwa Tanzania, reli ya Tazara inapita katikati ya mbuga za Selous wakati Barabara ya Southern Highway nayo inapita ndani ya mbuga za Mikumi na wala wanyama wale hawajadhurika.
Hizi propaganada za kenya ndiyo changamoto kwetu watanzania kujiuliza tena kama kweli hili shirikisho lina maana yoyote kwetu. Nimesoma kelele wanazopiga kule facebook nikalinganisha na jinsi walivyotufanyia kwenye swala la uuzaji pembe za ndovu, na mgogoro wa maji ya mto nile nikaona hapa hakuna ushirika wowote; ni utapeli mtupu.
I never heard some of our leader are thinking of that, i am Tanzanian but for sure this is the issue which does not need to be kenyan or tanzanian!
There should be no tarmac road in national parks for whatever reason, infact personally i am furious with the government after it allow normal passenger buses goin to Musoma to pass across Serengeti as transit, this route should be the last alternative, all passengers should be passing to Mwanza via Singida and goin to Musoma!
This plan should be condemned by all concerned individuals!
Safari ni Safari,
Airport ya Mugumu inamnufaisha mtu mmoja tu. Tudor.
Kichuguu said:Hawa wakenya siyo wenzetu kabisa, mimi nimekuwa nalifahamu hilo tangu mwaka 1977, ndiyo maana sikubaliani kabisa na huu upuuzi wa shirikisha. Juzi juzi hapa jamaa mmja kaandika kuwa Tanzania haina barabara ni chafu; tukitaka kujenga wanakuwa wa kwanza kupiga kelel tusijenge. Ngoja tuone kama serikali ya CCM itakubaliana nao, ni hapa ninapoanza kufikiria kuwa na kiongozi kama Lowasa ( minus tamaa ya mali).
Wote mnaokubaliana na madai ya kenya mnakosea kwa sababu kadhaa, nitajaribu kusema chache hapa chini.
(1) Sehemu kubwa ya mbuga ya Serengeti iko Tanzania, ni sehemu ndogo sana iliyoko upande wa Kenya ambako inaitwa Masai Mara. Kwa hiyo kufuatia mzunguko wa wanyama, ni wachache sana wanaokatisha mpaka baina ya nchi hizo. Wengi wao wanaishi Tanzania; hebu angalia ramani hii hapa.
(2) Barabara kupita kwenye mbuga za wanyama siyo jambo la ajabu kabisa; kuna mbuga nyingi ambamo barabara zinapita na wala wanyama hawajawahi kuhama. Mifano ni kama ifuatavyo:
a) Hapo Serengeti kuna barabara inayotoka Arusha kwende Mugumu kupitia humo humo Serengeti. Barabara hii ndiyo ambayo serikali inataka kuwekea lami; ni barabara ya siku nyingi sasa, na kwa miaka nenda rudi ilikuwa inatumiwa na maloli ya mzigo kusafirisha biadhaa katia ya Musoma na Arusha, Tanga na DSM. Kwa miaka yote hiyo barabara hiyo imekuwa inatumika huku ikitimua vumbi sana wakati wa kiangazi na wakati wa masika kujaa matope yanayoweza kukwamisha magari na kuhatarisha maisha ya abiria. Ubovu wa barabara hii ndio uliosababisha raia wa Tanzania wakawa wanaamua kupitia Kenya kutoka Arusha kwenda Musoma au Mwanza.
(b) Vile vile kutoka Mto Wambu kuna barabara nyingine inayopita hapo hapo Serengeti kwenda hadi Lamadi; hii nayo ni kama ile inayokwenda Mugumu.
(c) Barabara ya Bunda Musoma karibu na Lamadi ndiyo mpaka wa mbuga za Serengeti, lakini wanyama wale hutembea sehemu zote za barabara kwenda ziwani na kila ukiipta saa za jioni utakutana nao mbona hawajahama eneo lile.
(d) Huko Kenya kwenyewe, ile highway inayotoka Mombasa kweda Nairobi inapita katikati ya mbuga za Tsavo. Vile vile ile reli inayotoka Mombasa nayo inapita hapo hapo Tsavo; na barabara inayotoka Moshi kwenda Taveta nayo inapita katikati ya mbuga ya Tsavo.. Mbona wanyama wa Tsavo hawajahama.
(e) Kwa upande wa kusini mwa Tanzania, reli ya Tazara inapita katikati ya mbuga za Selous wakati Barabara ya Southern Highway nayo inapita ndani ya mbuga za Mikumi na wala wanyama wale hawajadhurika.
Hizi propaganada za kenya ndiyo changamoto kwetu watanzania kujiuliza tena kama kweli hili shirikisho lina maana yoyote kwetu. Nimesoma kelele wanazopiga kule facebook nikalinganisha na jinsi walivyotufanyia kwenye swala la uuzaji pembe za ndovu, na mgogoro wa maji ya mto nile nikaona hapa hakuna ushirika wowote; ni utapeli mtupu.
Nitakubaliana na wewe siku nikiona uwanja huo unatumiwa na watu wengine mbali ya Tudor na wageni wake.Could be true....and untrue as well....he is clever kwamba anajenga kwa hela yake...anainflate costs...halafu ana-recover toka kwenye taxes and levies...but the airport will be there and we will all use it...akiondoka ataicha...
Watalii hawatahitajikla kushuka Nairobi au Arusha but deep into Serengeti.....mahoteli yetu yatapata mapato na watalii kupunguza travel time