Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Hii mijadala inayoibuliwa huku ya mara Lowassa for 2015, Prof Mwandosya kugombea 2015, Membe anafaa 2015 mara Sitta na mbio za uraisi 2015 ni upunguani!
Tunaongelea 2015 wakati 2011 inatushinda. Hao tunaowasema wamekaa tu nchi inateketea tunawajadili eti watagombea 2015. Watagombea ili nini? Sasa hivi wanatusaidiaje? Dowans wanalipwa, IPTL, TRC, Loliondo, Wizi kwenye Halmashauri na mengineyo bado tunapoteza muda kuwafikiria. Kwani kukemea maovu mpaka 2015? Mafanikio yao ni nini sasa hivi? Eti ni wasafi!! Kwani JK kabla ya 2000 alikuwa na uchafu gani tunaoujua? Si aliitwa chaguo la Mungu?
Saa nyingine tunacheka tamko la waislamu lakini na matendo yetu humu ndani hayapishani sana. Hatuweki vigezo vya kumpata Raisi bora atakayetutoa kwenye dhiki. Tunabaki kujadili watu ambao hatuoni msimamo wao kwenye matatizo yetu ya msingi! Wengine watasingizia collective responsibility, hii haikuzuii kufikiri. Haikuzuii kusimama kidete na kutetea maslahi ya watanzania. Kama waziri au kiongozi unaona unabanwa kutetea achia nafasi na tutakuamini.
Hakuna sababu ya kupoteza muda kuwajadili watu wasio na msaada kwetu. Nakereka sana viongozi wote wako kimya kuhusu dhuluma inayoendelea. Sio wa upinzani sio wa CCM. Hakuna vitendo ni maneno tu. Dowans ni ya fulani, Dowans kampuni ya kitapeli, Mkataba na Richmond feki, huu sasa ni upuuzi! Ni sawa sawa mtu anakukumbusha jina lako!!
Maneno huumba lakini siku wananchi waliochoka na porojo zetu watakapochagua msitu na kutokea huko ndio tutajua 2015 nani Raisi!