Kuibuka sasa kwa kashfa ya LUGUMI ni mpango wa Mungu Watanzania wamjue waliomuamini na kumsifia

Mkuu, nina imani yataendelea kuibuka mengi na mazito ambayo Magufuli hatoweza kuyagusa. Hapa leo wameleta kisingizio cha taarifa za majeshi/usalama lakini yataibuka mengine ambayo watakosa kisingizio.Tusubiri na taarifa ya CAG maana nayo itakuja na mengine.

Si muda mrefu watu watamchoka Magufuli.
Hii Lugumi itakuwa kama meremeta na kagoda. Time will tell.
 
LUGUMI ATOROKA NCHINI ADAIWA KUPANDA NDEGE USIKU WA MANANE, HAIJULIKANI ALIKOKWENDA.

Mfanyabiashara anayemiliki Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, Said Lugumi, ametoroka nchi.

Lugumi ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kupindukia katika kipindi kifupi, aliingia mkataba tata na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Taarifa za kutoroka nchi kwa mfanyabiashara huyo, zilielezwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola, ambapo inadaiwa kuwa aliondoka nchini Jumatatu wiki hii, siku ambayo Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha mkataba huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa mujibu wa sheria.

Mfanyabiashara huyo ambaye amekuwa akitembea na msafara mkubwa wa magari ya kifahari, huku akilindwa na walinzi maalumu wa kukodi, ametoroka wakati vyombo vya dola vilikuwa vikimuwinda.

Utata wa Malipo
Pamoja na hali hiyo inaelezwa kuwa licha ya Lugumi kuingia mkataba na Jeshi la Polisi wa Sh bilioni 37, lakini bado alilipwa Sh bilioni 46 nje ya mkataba.

Katika mkataba huo, alilipwa kiasi Sh bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya fedha za makubaliano ya mkataba, lakini hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 pekee jijini Dar es Salaam ambavyo hata hivyo haijaainishwa maeneo vilipo.

Sakata hili lilibainika wiki iliyopita baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kukutana na maofisa wa jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Msafara wake Wapungua
Duru za ndani zinaeleza kuwa tangu Kamati ya Bunge ilipoibua sakata hilo na vyombo vya dola kuanza kuwahoji baadhi ya washirika wake katika biashara, msafara wa mfanyabishara huyo umepungua.

Chanzo kimoja kinasema kwa mara ya mwisho mfanyabiashara huyo alionekana eneo la Oysterbay jirani na Kanisa la St. Peter, huku akiwa na magari mawili badala ya saba hadi 10 kama ilivyokuwa awali.

Mtoa habari huyo alisema Lugumi aliopoonekana mwishoni mwa juma lililopita, alikuwa na magari mawili likiwamo Toyota GX V8 toleo la mwaka huu, ambalo lilikuwa limebeba walinzi wake, huku mwenyewe akiwa ndani ya gari la kifahari aina ya Escalade.

“Lugumi anaishi Mbweni na awali ilikuwa msafara wake ukipita magari husimamishwa ili kumpisha, na huwa na magari mengi kweli mithili ya kiongozi wa nchi, jamani kuna watu wamejua kuitafuna nchi hii, na sasa huenda unatimia usemi wa Rais Magufuli kuwa ni zamu yao kuishi kama mashetani na si kama malaika,” kilisema chanzo hicho.

Mkataba Wahamishwa
Sakata la mkataba huo wa Polisi na Lugumi limezidi kuchukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kunyang’nywa hoja hiyo na badala yake kuhamishiwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hatua hiyo inatokana na utata uliogubika mkataba huo ambao unawahusisha vigogo kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli, huku ikidaiwa kuwa huenda ikawa njia ya ‘kulindwa’.

Kutokana na hali hiyo, hadi kufikia Jumatatu saa 10 jioni, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema kuwa kamati yao haijapokea taarifa yoyote kuhusu Kampuni ya Lugumi, ambapo kamati hiyo ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo hadi kufikia leo.

Aeshi alisema wamemuomba Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, ili aweze kuwaandikia Polisi barua kwa ajili ya kuwasilisha mkataba huo.

“Tumelazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge ili awaandikie barua polisi walete mkabata huo ndani ya siku tatu kutoka leo (juzi) kama walivyotakiwa na kamati yetu,” alisema Hilaly.

Kauli ya Bunge
Alipotafutwa Mkuu wa Idara ya Habari, Elimu na Mawasiliano, Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya, alisema kama kuna hoja iliyoibuliwa na Kamati ya PAC kisha ikapelekwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, itakuwa ni kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha.

“Kama suala hilo lipo Mambo ya Nje, itakuwa si kwa hoja iliyoibuliwa na PAC na hakuna suala linaloshughulikiwa kama limeanzia PAC.

“Na kama litakuwa limekwenda huko ni kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu matumizi ya fedha, na unajua hivi sasa hizi kamati zipo katika maandalizi ya bajeti. Ila hoja kuhamishiwa kamati nyingine hutokana na maelekezo ya Spika wa Bunge. Kwa hoja hii ya PAC bado suala hilo lipo chini yao,” alisema Mwandumbya.

Chanzo: Mtanzania

Mimi nafikiri kwa ufisadi huu Wafadhili wasitishe tu misaada mpaka kwanza wahusika wachukuliwe hatua.Haya mambo jamani yanakera sana!
 
Kwa tuhuma hizi nzito nilitarajia kusikia watu fulani wamesimamishwa au teuzi zao zimetenguliwa ila cha ajabu bado wako ofisini alafu tunaambiwa tumempata Sokoine!!!
Akikamata mtu mnasema kuwa atalitia hasara taifa kwa kuwa anakurupuka, angesubiri uchunguzi kwanza!
Akisubiri, anaonekana si msafi na anaogopa watu!
sikushangai hata mimi huwa nina maoni tofauti ktk jambo moja, lkn kiukweli hatujui tunachotaka!
Tumuache atende kwa kipimo chake, kisha tutampima kwa matokeo ya kazi zake!
No wonder alilia kwa cardial Pengo kuwa angejua "angeomba kikombe hiki (cha uraisi wa Tz) kimuepuke"
 
Alafu huu mkataba wa Lugumi haukuridhiwa na Baraza la Mawaziri Magu akiwemo?
Aiseee kelele nyingi kumbe ni mweupe hivo kichwani!! Hivi unajua hata public tendering inavyofanywa?? Sasa mkataba wa mnunuaji na muuzaji unaendaje kwenye baraza la mawaziri?? Si unaishia kwenye Tender Board ya wizara tu...
 
Ukiwa, monduli, kina Kitillya team etc, bado mtatumbuliwa tu, msifanye diverting hapa ni kazi tu
Kwa hiyo wanatumbuliwa wakaskazini tu.. Basi wafukuzeni kabisa wezi hao waanzishe nchi yao wakaibiane wenyewe... Msukuma hakuna kuguswa awamu hii kama wakwere walivyopata kutamba awamu iliyopita
 
Kasi ya kumtimua Mama Kilango ilifurahisha lakini Ligumi mhaaa haaa ha aaa eti Tanzania tumempata Sokoine wetu hata 2% bado hajamfikia.
Lakini kumbuka haya ni masuala ya kimkataba yanahitaji umakini kidogo kuyaamua na ndio maana suala bado liko mikononi mwa PAC na co uteuzi kama wa mama Kilango.
 
Inasemekana Mida hii (usiku huu), yupo ofisini kwake ATC house. Mazingaombwe ya ccm yanaendelea.

I love Tanzania, Jina lako ni tamu Mno.
 
Hivi Lugumi ni dharau kwa Rais au ni shule ndogo? Tafakari kauli yake hii kwenye ukurasa wake wa facebook:

"Sio kila JIPU ni la kutumbua. Hata MTUMBUA MAJIPU ANAJUA".

This is a classic headline for a major newspaper...
 
Ni kweli hayakutamkwa naye lakini siku yalipotamkwa alikuwepo pamoja na mwanasheria mkuu wa Serikali pia alikuwepo wote hawa walikuwa na Pinda alipoyatamka maneno yale

KAMANDA BAK TOKA BAADA YA UCHAGUZI NAONA ULIAMUA KWENDA UNDERGROUND ; NILIKUWA NA WASIWASI SANA MPAKA SIKU MOJA NILIKUULIZIA HUMU LAKINI SIKUPATA JIBU!! NAFURAHI KAMA NDIO UMERUDI JANVINI!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Aiseee kelele nyingi kumbe ni mweupe hivo kichwani!! Hivi unajua hata public tendering inavyofanywa?? Sasa mkataba wa mnunuaji na muuzaji unaendaje kwenye baraza la mawaziri?? Si unaishia kwenye Tender Board ya wizara tu...
Hapa nimeulizwa kama swali kiuchokozu tu lakini ujue kuna gazeli limeandika hiki nilichohoji.
 
Hivi Lugumi ni dharau kwa Rais au ni shule ndogo? Tafakari kauli yake hii kwenye ukurasa wake wa facebook:

"Sio kila JIPU ni la kutumbua. Hata MTUMBUA MAJIPU ANAJUA".

This is a classic headline for a major newspaper...

Hii ni dharau Kubwa sana...ila mkuu wa kaya hapa anaweza gonga mwamba...tusubiri tuone..
 
Shukrani Kamanda Ndinani

KAMANDA BAK TOKA BAADA YA UCHAGUZI NAONA ULIAMUA KWENDA UNDERGROUND ; NILIKUWA NA WASIWASI SANA MPAKA SIKU MOJA NILIKUULIZIA HUMU LAKINI SIKUPATA JIBU!! NAFURAHI KAMA NDIO UMERUDI JANVINI!
 
Kwa tuhuma hizi nzito nilitarajia kusikia watu fulani wamesimamishwa au teuzi zao zimetenguliwa ila cha ajabu bado wako ofisini alafu tunaambiwa tumempata Sokoine!!!
Ataishia kutengua wanyonge wake kama mhe wa shy kuna majipu mengine hayatumbuki yako kwenye mshipa mbaya ukilitumbua ni mtu anakufa hapo ndio busara na usomi wa dr unahitajika kwa hili la lugumi na polisi jipu halitumbuki sana watu watapewa pain killer na upepo utapita bila shida yetu macho lakini na hii double standard
 
Magufuli majipu mabaya katikati ya makalio hayawezi anaweza vijipu uchungu vya usoni habari za Dau siwalikuwa wanafanya wote Magufuli akiwa ujenzi nani alisaini mikataba ya miradi kama ya Daraja la Kigamboni kwa niaba ya serikali si ni Magufuli yeye hawezi kujitumbuwa uchunguzi gani wakati wengine anawaweka ndani huku uchunguzi ukiendelea
Kama angekosa msiri wake Kitwanga kuwa wizara ya mambo ya ndani sasa hivi angeitisha vyombo vyote mpaka vya nje wamuone anavyotoa utani wa kutumbuwa waziri IGP na huyo jamaa wa nyumba 40

Kumbe huelewi. Mkataba wa ujenzi wa Kigamboni Bridge ulisainiwa wakati waziri wa ijenzi akiwa Dr Shukuru Kawambwa wakati ule Magufuli alikuwa waziri wa Mifugo na Uvuvi. Pia yakupasa uelewe Kigamboni Bridge imesimamiwa na NSSF yenyewe na malipo yote yamefanywa na NSSF moja kwa moja wizara husika haikuhusika na masuala ya malipo bali wao walihusika kwenye ukaguzi wa kitaalam tu kama user ministry.

Suala la inflation ya gharama za ujenzi wa Kigamboni Bridge limefanywa na maofisa wa NSSF wala siyo wizara ya ujenzi kwa interest zao kwa mujibu wa reprt ya CAG 2013/2014.
 
Jipu liko kwenye ngoma ya sikio,sasa ni wakati wa kuwatumbua ndugu zake wa karibu
 
Kumbe huelewi. Mkataba wa ujenzi wa Kigamboni Bridge ulisainiwa wakati waziri wa ijenzi akiwa Dr Shukuru Kawambwa wakati ule Magufuli alikuwa waziri wa Mifugo na Uvuvi. Pia yakupasa uelewe Kigamboni Bridge imesimamiwa na NSSF yenyewe na malipo yote yamefanywa na NSSF moja kwa moja wizara husika haikuhusika na masuala ya malipo bali wao walihusika kwenye ukaguzi wa kitaalam tu kama user ministry.

Suala la inflation ya gharama za ujenzi wa Kigamboni Bridge limefanywa na maofisa wa NSSF wala siyo wizara ya ujenzi kwa interest zao kwa mujibu wa reprt ya CAG 2013/2014.
Magufuli hachomoki angeweza kuubadilisha alivyo rudi ujenzi Hapo na yeye yumo kwenye kashfa kama Dau tu
 
Back
Top Bottom